Lowassa: Ni ngumu upinzani kushinda Arumeru

Ukweli ni kuwa ulafi wa madaraka unasababishwa na chadema, kama wameshapata madiwani wa kutosha kwa nini wasipige kura kuamua kati ya cuf na NCCR mmoja ndio angesimamishwa hapo, hili la kujiona kuwa wanakubalika sana kaskazini ndio linawafanya wanyime nafasi vyama vingine kukua ukanda huo.
 
Chadema ni wabinafsi sana. Kama wanasimamia Usawa, Haki na Demokrasia kwa nini wasiwaachie CUF na NCCR wasimamishe wagombea!?
 
Mkuu, umewasababishia UKAWA kuharisha asubuhi asubuhi bila matarajio. Isitoshe leo ni maadhimisho ya sherehe za mapinduzi Zanzibar, yaani ndio wanaharisha mfululizo.

Lowasa walimalizana na Mbowe na wanajua wao tuu walikubaliana nini, hawa wengine UKAWA wanahangaika tuu. yaani wanatumika bila kujitambua.
 
Nilishasema toka mwanzo kuwa Lowasa hakustahili kukaa chadema. Lowasa kashakuwa kama mwenyekiti wa chama. Mwenyekiti wa chama kashakuwa kama member tu wa kawaida. Nashangaa napoona anajitayar kugombea urais tena 2020. Chama kimempitisha????
So sad. Mwenyekiti wetu(mbowe) kapoteza Dira.
Mbowe usirudie kosa 2020
Nakaribisha washambuliaji
eti nakaribisha washambuliaji!
 
Tanzania hakuna upinzani. Hawa kina Lowasa na Mbowe wanawauza tu kisiasa.
 
eti nakaribisha washambuliaji!
Nimesema hivo maana kuna watu wanamahaba ya ajabu sana. Tukisema Lowasa hakufaa ba hafai wanaleta matumbo juu.
Hili kosa mbowe hatakiwi kabisa kurirudia.
Mwananchi usirudie kosa 2020
 
Naona mnajitekenya na kujichekesha team Lumumba, aliposema aliyeshinda alimaanisha aliyeshinda kihalali ambaye ni wa chadema na ndo maana huyo ******** akatenguliwa na mahakama
 
Na ubinafsi huo ndio ulisababisha Julius Mtatiro aangukie pua

Yaani nchi hii sio ccm wala upinzani wana afadhali wote washenzi tu
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Mimi sijakuelewa mleta mada. Alishinda halafu akatenguliwa na mahakama,baada ya kutenguliwa si akapewa ushindi mtu mwingine au!? Na huyo aliyepewa ni wa ccm au cdm!?
 
Lowasa bado n mwanachama wetu halali..anafanya kaz tuliomtuma baada ya kumuona mrema amezeeka
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Lowasa ni agent wa ccm na hawezi kuikana ccm, airudishe kadi ya ccm kwanza,

Yupo kwaajili ya kuuwa upinzani
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Kuna jambo wengi hawajui siasa zaidi ya vijembe. Katika kata zote za uchaguzi kwa udiwani CUF wamesimamisha wagombea sehemu karibu zote. ACT na Chadema pia. Hapo wenye akili wanasema ukweli tu.

=======

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema uwezekano wa vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kushinda katika uchaguzi wilayani Arumeru, mkoani Arusha ni mdogo.

Amesema hali hiyo inatokana na uamuzi wa vyama hivyo kila kimoja kusimamisha mgombea udiwani katika Kata ya Matevesi, kinyume na makubaliano.

Lowassa alisema hayo katika kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa kata hiyo. Alisema kilichofanywa na vyama vya upinzani ni kugawa kura, wakati upinzani ulikuwa na nafasi kubwa ya kushinda.

Alisema vyama vinavyounda Ukawa vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, kila kimoja kimesimamisha mgombea udiwani katika kata hiyo, kwa hali hiyo uwezekano wa kushinda ni mdogo sana, hivyo kukipa mwanya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda kiti hicho.

Akizungumza katika kampeni za Chadema zilizofanyika katika Kitongoji cha Ematasia, Lowassa alisema vyama hivyo tayari vimeshafanya kosa la kiufundi, linaloweza kusababisha vyama hivyo ‘kuangukia pua’ katika uchaguzi huo na kuiwezesha CCM kuibuka na ushindi asubuhi na mapema.

Alisema CCM ina nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi huo, kutokana na kuwa na uhakika wa kura zake, kutokana na kutokuwa na upinzani wa chama kingine chenye mrengo wake, kama ilivyo kwa vyama hivyo vya Ukawa, ambavyo viko katika hatari ya kugawa kura.

“Nyie tayari mmeshafanya makosa makubwa ya kiufundi kwa kila chama cha Ukawa kusimamisha mgombea wake, hapo ndipo CCM wanaposhindia, kwa hiyo mwendelee mkijua mna kazi kubwa kushinda,” alisema Lowassa.

Katika hali ya kushangaza Lowassa alijikuta akimuombea kura mgombea wa CCM, Julius Savoyo aliposema wananchi wa kata hiyo wanapaswa kumpa kura na kumuweka madarakani mgombea aliyeshinda katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2015, pasipo kujua diwani aliyeshinda wakati huo na kutenguliwa na mahakama ni wa CCM.

“Wananchi wa kata hii hamna kazi ngumu katika uchaguzi pamoja na makosa yaliyofanywa na vyama vya Ukawa, hakikisheni mnamrejeshea udiwani yule aliyeshinda wakati ule ili aendelee na kazi yake,” alisema Lowassa.

Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Shaaban Mdoe alisema kitendo kilichoonekana na Lowassa kuwa ni kosa kusimamisha wagombea wa vyama vya Ukawa ni utabiri mzuri wa ushindi kwa CCM, kama alivyosema tena katika kampeni za uchaguzi wa Urais mwaka juzi.

Hata hivyo, Mdoe alisema suala la Ukawa kwa sasa halipo tena, bali ni Ukiwa na ndiyo maana kila chama cha muungano huo, kinajaribu bahati yake kutokana na kuvunjika kwa ndoa hiyo ; na wa mwisho kuondoka katika ndoa hiyo, alikuwa ni Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Mdoe alisema kitendo cha Lowassa kumnadi mgombea wa CCM, si bahati mbaya bali ni ukweli uliopo ndani ya moyo wake, kwa kuwa hata akijifungia chumbani kwake peke yake, anakubali kazi nzuri inayofanywa na serikali ya Rais John Magufuli.


Chanzo: Habari Leo
Ni ngumu kama mama janeti kuambatana na mumewe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom