Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,559
- 3,748
Uzi huu udumu uje kuwa ukumbusho huko twendako
Ukomo WA ukijana ni miaka ngapiEti sisi kama vijana usikute hapo umeshakata miaka 40 lkn bado unajiita tu kijana!
Ukomo WA ukijana ni miaka ngapi
45Ni swala la common sense tu inawezekanaje Mtu wa miaka 40 ajiite Kijana? Kumbuka kuna utoto, halafu Ukijana ndiyo unaanza baada ya utoto, sasa iweje mtu wa miaka 40 awe kijana na mtu wa miaka 20 tumuitaje? Au unataka kuwaweka wote kundi moja? Miaka 40 ni mtu mzima na siyo kijana!
Mkuu kwani ungekaa kimya Lumumba wangekukata posho yako?Eti sisi kama vijana usikute hapo umeshakata miaka 40 lkn bado unajiita tu kijana!
------------------------
Pengine Zama za Kina Augustine Lyatonga Mrema, kuhama kutoka CCM kwenda Upinzani (NCCR MAGEUZI) ni zamani Sana kiasi cha vijana wa umri wangu na Nape kukumbuka sawasawa.
Lakini inatosha kusema kwamba Mrema hakuwa mtu Mdogo ndani ya Serikali ya CCM
Mrema amepata kuwa na nafasi kadhaa za uongozi ndani ya serikali ya Tanzania,
Mrema amekuwa Waziri wa Kazi, Mrema amekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mrema amewahi mpaka kuwa Naibu Waziri Mkuu cheo ambacho hakijawahi kuwepo ndani ya katiba ya nchi hii.
Kwa waliomshuhudia Mrema akipigiwa Saluti na Viongozi wa Polisi, akisafishiwa barabara ili apite kuwahi majukumu hakuna aliyeamini kama mrema angeweza kwenda upinzani.
Sio tu hakuna aliyeamini kwamba Mrema atahama CCM, Lakini zaidi hakuna aliyewahi kuwaza kuwa mrema angekuja siku moja kupigwa mabomu ya machozi na Polisi aliowaongoza kama waziri wake Kwa ufanisi mkubwa.
Tuachane na Mrema, si tunasema ya kale hayanuki? .
Juzi hapa yametokea mambo mengine yanayopaswa kuwa FUNZO kubwa Kwa wanasiasa vijana hasa waliopo madarakani hivi Sasa kupitia CCM.
Edward LOWASSA Kwa Sasa anaweza kuwa ndiye Mtanzania maarufu kuliko wote hapa nchini,
LOWASSA amekulia CCM, LOWASSA amelelewa CCM.
LOWASSA amekuwa mkurugenzi wa Taasisi za serikali,
LOWASSA amekuwa Mbunge wa CCM,
LOWASSA amekuwa Naibu waziri wa serikali ya CCM,
LOWASSA amekuwa waziri wa serikali ya CCM,
LOWASSA amekuwa waziri Mkuu wa serikali ya CCM,
Lakini LOWASSA Leo si mwanachama wa CCM.
LOWASSA Leo Sio tena mwanamkakati wa Chama cha mapinduzi. Sasa hivi miongoni mwa maadui wa kisiasa wa CCM basi ni Edward LOWASSA.
Zipo sheria nzuri alizoshiriki kuzitunga LOWASSA akiwa waziri na mwana CCM,
Zipo sheria mbaya ambazo LOWASSA ameshiriki kuzitunga akiwa CCM,
Japokwamba zote hizi alishiriki kuzitunga akiamini anakipigania Chama chake, Leo Sio MWANA CCM tena.
Leo hapigiwi tena ving'ora na Leo akifanya mchezo tu anakamatwa na Polisi kama anavyokamatwa Mbowe wa Chadema na Mchange wa Act.
Sio LOWASSA tu, Fredrick Turway SUMAYE halikadharika, yeye tofauti na LOWASSA, SUMAYE amekuwa waziri Mkuu Kwa miaka 10 mfululizo Lakini Leo si mwana CCM tena na hata sheria alizoshiriki kuzitunga zikipigiwa kelele na wapinzani anaziona zikimminya na yeye.
Sisi kama vijana lazima tujifunze Kwa wanasiasa hawa wakubwa waliotutangulia.
Nape na vijana wenzake waliopo serikalini Leo lazima wajue kuwa Kuna kesho.
Nape na vijana wenzake walioko serikalini Leo lazima wajue kuwa *Politics is Dynamic* siasa hubadilika.
Nape na vijana wenzake walioko serikalini Leo lazima wajue kabla ya wao kuwepo Leo Kuna wenzao walikuwepo katika nafasi hizo na hivi Sasa hawapo na hata wao hawatakuwepo milele humo.
Nape na vijana wenzake waliopo serikalini Leo ni lazima wajue kwamba hatutungi sheria Kwa mahitaji yetu ya Leo, hatutungi sheria kudhibiti ama kusimamia ama kunyoosha jambo Kwa Leo tu, bali sheria inatungwa Kwa ajili ya Leo, kesho Kwa watoto wake na keshokutwa Kwa wajukuu zake.
Nape na vijana wenzake waliopo serikalini lazima ajifunze kwamba yeye bado ni kijana na hivyo bado ana kesho nyingi, nyingi nyingi zaidi.
Lazima ajifunze kutokufanya jambo la kumfurahisha yeye tu, zaidi litakaloishi Kwa matumizi ya vizazi vyetu.
Tuwatumie wanasiasa waliotutangulia kama kioo chetu cha kujitabiria kesho zetu
Tuwaangalie kina LOWASSA kama walimu wa kweli wa somo la siasa, somo linalosema Kwenye siasa lolote linaweza kutokea.
Nani aliwahi kufikiri Mzee Kingunge Angewahi kuihama CCM Leo? . Nani anaweza kusema alitabiri hili? ..
Naomba niishie hapa Kwa Leo.
Ndimi
Habib Mchange.
Km hutak sikulazimishi....Miaka 45 kama vile miaka 40 huyo mtu siyo Kijana bali ni Mtu mzima!
Km hutak sikulazimishi....
Ukiiangalia sana wenye matatizo haya ya kuhama ccm na kuutaka uraisi kwa udi na uvumba ni jamii ya watu wa eneo fulani Katika nchi yetu. Mbona Salim ahmed Salim hakuhama pamoja na fitina zote alizofanyiwa 2005?
Watanzania tuwe makini sana.
Tafakari chukua hatua.
Wakati Nape, Samweli Sita, Mpendazaoe Makonda, na wenzao walipoanzisha CCJ ilikuwa kwa ajili ya kucheza mdundiko? Elewa kila mwanasiasa ana uchu/uroho wa madaraka. Hakuna mwanasiasa asiyetaka kuwa na madaraka, wote ni waroho tu. Katika uroho huo Ccm ni vinara,
Uvumba tupo wengi mkuu ila hatuwazidi Nyumbu mkuu. Nyie ni wengi zaidi mkuu.Uvumba wako wengi, je wa push up umemsahau! Uliona wapi mtu mzima anafanya hivyo mbele ya kadamnasi kama siyo udi na uvumba
Kwa hiyo mlipomuita Kikwete kijana alipokuwa anagombea mwaka 2005 mlikuwa mnamaanisha nini?Siyo swala la kutaka au kutokutaka bali ni swala la common sense, kama unataka kumuita mtu wa miaka 40 kijana, je unataka kumuweka kundi moja na Mtu wa miaka 21?
K
Kwa hiyo mlipomuita Kikwete kijana alipokuwa anagombea mwaka 2005 mlikuwa mnamaanisha nini?
Yaelekea hujaelewa vizuri nini mtoa mda anachomaanisha! Rudia kusoma upya.Kipi unataka kutuaminisha hapa?Bila shaka ni kwamba hata Nape naye IPO siku atahama CCM.Hilo linategemea na yeye na sababu itayomwondoa.Lkn tofauti na uliowataja,wao waliondoka Kwa kusukumwa na roho yao ya uchu wa madaraka na Utapeli wao wa siasa!Kwalo wao ndiyo hasa eti walikuwa watu sahihi kuwa pale magogoni jambo ambalo si kweli.Ingetosha uwatambulishe km matapeli na walio na uchu wa madaraka na si uongozi ndicho hasa baada ya kuikosa fursa hiyo ikawalazimu wakajaribu na kuendeleza hiyo nia yao huko kwingineko.Ndiposa hata huko walikoelekea unatambua fika kwamba kwa sababu hizo nilizodhiainisha walitumia pesa za kifisadi kwa waliojifanya WATAKATIFU na wasio na mawaa kuwapatia na hatmaye utaratibu zikakiukwa na wao wakawa wagombea na bado wakakosa tena!
Hahaha. Jf kibokoUvumba tupo wengi mkuu ila hatuwazidi Nyumbu mkuu. Nyie ni wengi zaidi mkuu.
Haswaa HaswaaUshauri nzuri sana huu kuwahi kutokea so Nape usijosahau sana hata kama usipohama chama ila fauta sana ushauri huu utakusaidia huko uendako...
DefinitelyThis is the post of the day, I close the deal and call it a day.