Lowassa na Sumaye kabla hamjafanya hili, mtuombe kwanza msamaha watanzania na wanademocrasia wote.

Mar 17, 2016
193
188
Nadhani wote mmepata habari ya oparesheni kabambe ya kupinga kile kinachoitwa kugandamizwa kwa democrasia kunasemekana kufanywa na serikali ya awamu ya tano. Oparesheni hii inafanywa na vyama vya upinzani, Act wameanza Leo.CHADEMA/ UKAWA nao wametangaza kuanzia wiki inayoanza kesho, mm sina tatzo na hilo kwa kuwa ndo democrasia ya vyama vyingi, naamini hoja ya kuvunjwa katiba kama kweli ipo basi ingependeza kama wangeenda mahakamani.

Kilichonifanya nilete hapa Uzi huu ni watu hawa wawili ambao inasemekana ndio watakaoongoza oparesheni hiyo, namanisha Lowassa na Sumaye ambao watakuwa bega kwa bega na Mbowe na makamanda wengine kibao bila shaka ambao hata mm sina wasiwasi nao maana niwanamapambano, shida yangu ni hawa wawili.

Nikianza na Sumaye, huyu amekuwa waziri mkuu kwa miaka 10 mfululizo kwenye awamu ya 3 na bila shaka ndo waziri mkuu aliyekalia kitu hicho kwa mda mrefu zaidi. Sumaye ni moja ya watu ambao waliidumaza democrasia ya Nchi hii, mwaka 1995 ulipofanyika uchaguzi mkuu wa kwanza ulioshilikisha vyama vingi baada ya mfumo huo kurejeshwa, nuru ya ukuaji democrasia ilionekana, wote mnakumbuka timbwili la mzee wa Kilalacha Agustino Lyatonga Mlema.

Kilichofata baada ya hapo ni Sumaye na wenzake kuanza kuuvuruga upinzani, kutumia hila na nguvu, kuwatisha wapinzani na kuwadhoofisha, kuwatisha rsia kuhusu kujiunga au kusapport upinzani. Namkumbuka sana Aman Waridi Kaburu alivonyanyaswa kipindi hicho, lupango kwake ikawa kawaida. Ni kipindi cha Sumaye akiwa waziri mkuu, ilikuwa ni kama kosa la jinai kugundulika we ni mpinzani au unashabikia upinzani, yeye alienda mbali hadi kusema mfanyabiashara anayetaka kufanya biashara zake vzr lazima awe mwanaccm, mnajua kilichotokea zanzibar mwaka 2000, Sumaye alikuwa waziri mkuu, mnakumbuka kitendo cha mbwa kuingizwa ndani ya sehemu za swala, huyu ndo alikuwa mtendaji mkuu wa serikali.

Kwa upande wa Lowasa yeye amekuwa kiongoz mwandamizi ndani ya CCM amekuwa waziri kwa mda mrefu na amewahi kuwa waziri mkuu. Huyu ni mtu ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa sana, je? ni wapi alitumia ushawishi wake huu kuhakikisha democrasia inastawi. Huyu ni mmoja wa watu walioshiriki kuchakachua katiba ya wananchi akishilikiana na akina Kingunge, na Chenge akiamini angekuwa rais wa inchi hii, mungu ameepushia mbali, katiba hii anayoenda kuipinga kesho kutwa yeye ndo angekuwa anaitumia kuongoza, ndio! hansard za bunge zinatueleza aliikata katiba ya wananchi sasa anarudi kwa wananchi kuwaomba wamuuunge mkono, amesahau yeye walipomhitaji aliwakana, akaangalia masilahi yake, kwake ilikuwa kama ndoto ya mchana kuwa ipo Siku angevaa gwanda japo hajawahi, ila ipo Siku atavaa.

Ni kwa mukitadhaa huu mm nadhani unapogundua umefanya kosa na ukaamua kujirudi ni vzr, lkn ni vzr zaidi ukiomba kwanza msamaha kwa Yale mabaya uliyofanya, ndo maana nasema Lowassa na Sumaye waombe kwanza msamaha kama moja ya watanzania ambao wameshiriki kudumaza ukuaji wa democrasia wanayoenda kuidai kwa wananchi hapo kesho kutwa, vinginevyo hawana tofauti na wale walioambiwa ambaye anadhani yu msafi aanze kumrushia jiwe mtu huyu.
 
Mkuu hapa nimewazungumzia hao, unaweza ukaanzisha hoja juu ya hilo.
Nina uhakika huu uzi hautakuwa na wachangiaji wengi kwa sababu umesema ukweli tena ukweli mchungu. Nilishawahi kusema hapo nyuma kwamba ni "FISI mlafi tu ndo huweza kutafuna utumbo wake baada ya kuchomwa mkuki"
Ulafi wa madaraka unamfanya mtu kusahau ghafla hayo yote. Na hawa viongozi wanatumia uelewa mdogo wa kuchambua maswala ya kisiasa tulionao watanzania kuendelea kutuaminisha katika propaganda zao ambazo hazina uthabiti ndani yake na kiukweli Magu amekalia watu vibaya. Tumuungeni mkono ili hii nchi iwe ya watanzania WA kawaida. Changamoto huwa hazikosi katika mabadiliko ya kweli.
 

Attachments

  • Screenshot_2016-06-03-07-38-23.png
    Screenshot_2016-06-03-07-38-23.png
    231.3 KB · Views: 25
Nina uhakika huu uzi hautakuwa na wachangiaji wengi kwa sababu umesema ukweli tena ukweli mchungu. Nilishawahi kusema hapo nyuma kwamba ni "FISI mlafi tu ndo huweza kutafuna utumbo wake baada ya kuchomwa mkuki"
Ulafi wa madaraka unamfanya mtu kusahau ghafla hayo yote. Na hawa viongozi wanatumia uelewa mdogo wa kuchambua maswala ya kisiasa tulionao watanzania kuendelea kutuaminisha katika propaganda zao ambazo hazina uthabiti ndani yake na kiukweli Magu amekalia watu vibaya. Tumuungeni mkono ili hii nchi iwe ya watanzania WA kawaida. Changamoto huwa hazikosi katika mabadiliko ya kweli.
Mkuu tumezoea mambo ya umbeya umbeya Fulani hv, mambo yanayofikirisha hatupendi kabisa.
 
Back
Top Bottom