Lowassa na Seif waligombania Urais au nishani za amani?

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Viongozi wakuu wawili wa UKAWA (Lowassa/Seif) waliosimamishwa kuwania urais wa Jamhuri ya muungano na ule wa Zanzibar wameangukia pua.

Lowassa ameyakubali matokeo haraka bila ya kujali kuwa uchaguzi wa upande wa mshirika wa muungano ulifutwa kutokana na dosari kadhaa.

Wakati mwenzake Seif akifurukuta furukuta, Lowassa ameshajinyakulia nishati ya amani. Hongera.Kuna muelekeo mkubwa kuwa ikiwa Seif ataridhia status quo na kuidumisha iliokuwepo amani iliokuwep basi nae pia atafikiriwa pia kutunukia Tuzo ya Amani

Hivi hali hii ipo haja ya kuiweka katika katiba kuwa mshindwa wa uachaguzi ataunukiwa tuzo ya Amani na alieshinda iwe kwa hila au kwa mbinde atunukiwe Urais?

Basi bora zitolewe kwa wakati mmoja na hii itainyanyua hadhi ya kidomokrasia
 
Nimechukizwa sana na wagombea wangu wa ukawa kukubali matokeo gafla na mwingine kulizia marudio ya uchaguzi
 
Seif ameridhia kurudiwa kwa uchaguzi?naomba kujuzwa kwani nilikuwa mbali na media kidogo!
 
Sio kuritdhia ni kutekeleza, Chama cha CCM cha wapenda Amani kimeamua! Seif nae hana budi kukubali kurejewa uchaguzi wa kihuni mara baada ya sherehe za mapinduzi matukufu
 
Back
Top Bottom