mchakachuaji1
Senior Member
- Nov 4, 2010
- 104
- 7
Nimefuatilia nyendo za mbunge mchaguliwa wa jimbo la Monduli Edward Lowassa tangu alipofika Arusha saa chache kabla NEC haijatangaza mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Arusha mjini. Inaonekana kuna njama za kutaka kupandikiza watu wao katika ngazi mbalimbali za uongozi, sijui ni kwa manufaa ya nani ila inatia shaka kwa sababu hii inaonekana si kwa maslahi ya Taifa. Kwa sasa naona Chenge anapata support kubwa kutoka katika kundi hili ili afanikiwe kupata uspika wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania ili waweze kuwafunga mdomo watanzania kwa kuzima hoja zenye kutetea maslahi ya Taifa. Kwa haya yote nalazimika kuuliza hivi hawa kina Lowassa wana lengo gani na nchi yetu?