LOWASSA MWEUPE, PE-Na Emanuel Mbondo a.k.a Kiboko yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LOWASSA MWEUPE, PE-Na Emanuel Mbondo a.k.a Kiboko yao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMBOTA, May 23, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Makala ya Emanuel Mbondo,
  Ukishagundua umefanya ujinga inakulazimu utumie nguvu nyingi kuutetea ujinga wako wa awali, na ukishatetea ujinga kwa nguvu uta oneka na unafanya ujinga zaidi ya ule ujinga uliokuwa unautetea. Namaanisha LOWASA alitumia nguvu nyingi kuutetea wizi wake na sasa utetezi wake aliyekuwa akiutoa umemfanya ajione na aonekane mpumbavu na asiyejali watu wake.

  Kwa mfano LOWASA alisema anaonewa wivu kuwa waziri mkuu, sasa jiulize ni nani aliyekuwa anamwonea wivu LOWASA, huu ndo ujinga ninaosema, akaibuka tena akadai hakufanya makosa na hata leo hii angepewa tena uwaziri au urais angefanya kama alivyofanya kwenye Richmond.

  Huyu ndo LOWASA ambaye haoni kama alitumia cheo chake kuila nchi wakati wagojwa na mama zetu wakijifungulia kwenye vibaraza, mahospitalini kukikosekana madawa, ndugu zetu wakifa kwa ukosefu wa madaktari.

  Binafsi sikushangaa haya ya LOWASA kwa sababu najua yeye, mkewe, watoto wake, vimada wake, wapambe wake, marafiki zake, na ndugu zake wote hakuna mwenye kuathirika na hayo yote, wanatibiwa ulaya na Marekani, umeme wanatumia majenereta na TANESCO hawawezi kuwakatia umeme maana kazi zao zipo mikononi mwao ( wakina LOWASA ).

  Pia LOWASA hajaanza kuiba leo toka enzi za nyerere kama unakumbukumbu vizuri baba wa taifa alishawahi kumchana LIVE....LOWASA na watoto wake wanaogelea kwenye ukwasi wa hajabu huwezi amini kama ni watanzania wa Tanzania hii hata chama chake kinajua umuhimu wa LOWASA kipesa.

  Sasa jiulize mtumishi wa serikali iliyo maskini anapata wapi ukwasi wa namna hii? Jamani LOWASA kaiba toka zamani nani asijejua hili labda wanaotumia tumbo kufikiri badala ya kichwa. Na mtu anayesema LOWASA alikuwa mchapa kazi anachekesha, kwani aliteuliwa ili afanyeje?

  Alitaka kazi, akapata kazi na ilimbidi afanye kazi aliyotaka maana hakulazimishwa kuitaka kazi. Binafsi sioni na sidhani kama alikuwa mchapa kazi maana sikuona mabadiliko yoyote aliyofanya wizara ya maji, wala kilimo maana hadi anatoka kwenye wizara hizo bado matatizo yako palepale. Shida za maji, wakulima kukosa pembejeo na masoko ya uhakika ndo nlichokiona kwake.

  Ninachoona nikwamba LOWASA alikuwa anacheza sana na media ( vyombo vya habari) akisikia mafuriko huyo kashafika, akisikia mapigano huyo kasha fika lakini hakuna maamuzi ambayo aliyafanya kwenye hayo matukio yaliyoleta mambo ya maana zaidi yakupiga domo hapo nahakikisha kupanda shangingi lake la millioni 350 nakuchapa mwendo.

  Binafsi namuona LOWASA kama mtu aliyekuwa akisifiwa tu na vyombo vya habari na kusababisha watu waamini ni mchapa kazi kumbe ni mwizi aliyekubuhu ambaye anaweza hata kujiibia yeye mwenyewe mfuko wa kulia akaamishia wa kushoto.

  Naam huyu ndo LOWASA wa MONDULI mwenye hisa kwenye makampuni utitiri vodacom ni mfano tuu. Mtafute mwangalie mweupe nywele mweusi rohoni na matendo, hata kwa shetani hana nafasi.
   
 2. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duhh! Lowasa kakukosea nini mkuu?
  Shetani hakuwa mchafu wala mbaya kama unavyotaka kutuaminisha. Alikuwa malaika wa Nuru na kiongozi wa sifa. Mungu hakunyanganya sifa zake alipoasi hivyo si vyema kumlinganisha shetani na rangi nyeusi au kitu chenye sura mbaya. Hayo ni mawazo ya giza na kutofahamu neno la uzima.

  Lowasa kama alikosea msaidie atubu lakini kumtukana na kufanya ufanyayo havimsaidii wala havijengi ufalme wa mbingu.
  Pamoja na Dowans mie namuona Lowasa is far better than Pinda.
   
 3. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  some topics bwana.... kha!
   
 4. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sijakuelewa punguza jazba
   
 5. B

  BENTA Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa lipi yuko far better than Pinda fafanua mkuu.
   
 6. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2011
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Na Emanuel Mbondo,

  Ukishagundua umefanya ujinga inakulazimu utumie nguvu nyingi kuutetea ujinga wako wa awali...na ukishatetea ujinga kwa nguvu uta oneka na unafanya ujinga zaidi ya ule ujinga uliokuwa unautetea!Namaanisha LOWASA alitumia nguvu nyingi kuutetea wizi wake na sasa utetezi wake aliyekuwa akiutoa umemfanya ajione na aonekane mpumbavu na asiyejali watu wa...ke. Kwa mfano LOWASAa alisema anaonewa wivu kuwa waziri mkuu,sasa jiulize ni nanai aliyekuwa anamwonea wivu LOWASA..huu ndo ujinga ninaosema,akaibuka tena akadai hakufanya makosa na hata leo hii angepewa tena uwaziri au urais angefanya kama alivyofanya kwenye Richmond...huyu ndo LOWASA ambaye haoni kama alitumia cheo chake kuila nchi wakati wagojwa na mama zetu wakijifungulia kwenye vibaraza,mahospitalini kukikosekana madawa,ndugu zetu wakifa kwa ukosefu wa madaktari...binafsi sikushangaa haya ya LOWASA kwa sababu najua yeye,mkewe,watoto wake,vimada wake,wapambe wake,marafiki zake,na ndugu zake wote hakuna mwenye kuathirika na hayo yote,wanatibiwa ulaya na marekani,umeme wanatumia majenereta na tanesco hawawezi kuwakatia umeme maana kazi zao zipo mikononi mwao ( wakina LOWASA ).Pia LOWASA hajaanza kuiba leo toka enzi za nyerere kama unakumbukumbu vizuri baba wa taifa alishawahi kumchana LIVE....LOWASA na watoto wake wanaogelea kwenye ukwasi wa hajabu huwezi amini kama ni watanzania wa Tanzania hii hATA chama chake kinajua umuhimu wa LOWASA kipesa!! Sasa jiulize mtumishi wa serikali iliyo maskini anapata wapi ukwasi wa namna hii?Jamani LOWASA kaiba toka zamani nani asijejua hili labda wanaotumia tumbo kufikiri badala ya kichwa. Na mtu anayesema LOWASA alikuwa mchapa kazi anachekesha !kwani aliteuliwa ili afanyeje!!?Alitaka kazi,akapata kazi na ilimbidi afanye kazi aliyotaka maana hakulazimishwa kuitaka kazi!!!Binafsi sioni na sidhani kama alikuwa mchapa kazi maana sikuona mabadiliko yoyote aliyofanya wizara ya maji,wala kilimo maana hadi anatoka kwenye wizara hizo bado matatizo yako palepale..shida za maji,wakulima kukosa pembejeo na masoko ya uhakika ndo nlichokiona kwake...Ninachoona nikwamba LOWASA alikuwa anacheza sana na media ( vyombo vya habari) akisikia mafuriko huyo kashafika,akisikia mapigano huyo kasha fika lakini hakuna maamuzi ambayo aliyafanya kwenye hayo matukio yaliyoleta mambo ya maana zaidi yakupiga domo hapo nanakisha kupanda shangingi lake la millioni 350 nakuchapa mwendo.Binafsi namuona LOWASA kama mtu aliyekuwa akisifiwa tu na vyombo vya habari na kusababisha watu waamini ni mchapa kazi kumbe ni mwizi aliyekubuhu ambaye anaweza hata kujiibia yeye mwenyewe mfuko wa kulia akaamishia wa kushoto....naam huyu ndo LOWASA wa MONDULI mwenye hisa kwenye makampuni utitiri vodacom ni mfano tuu...Mtafute mwangalie mweupe nywele mweusi rohoni na matendo,hata kwa shetani hana nafasi!!

  HUYU JAMAA SIJUI ALICHOANDIKA MAZEE MMEONA HII NIMEIKUTA HUKU Nova Tzdream
   
 7. s

  sativa saligogo Senior Member

  #7
  May 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  YAP! :A S 103:Huyu ameaandika kwani, hamna upuuzi ulliokuwa upuuzi mtupu!!!!!!
  Mmmmh! YAMETIMIA!!! kwani hayo ni malipo halali kwa matendo aliyoyafanya, hukumu ni hapahapa duniani haki mbinguni!!!!
  MWL ALISEMA ASIYESIKIA LA MKUU!!!!:A S 103:
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  unajua Lowassa akisoma vitu hivi anawaona wapumbavu sana...hivi kwa nini msijadili mambo mengine ......mnapiga makelele weee yeye anaona poa tu
   
 9. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Kweli mweupe kwani alishindwa hata kujibu swali la mtoto wa Primary kule kanda ya ziwa
   
 10. M

  Marytina JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  lowassa mweupe kama jk
   
Loading...