Lowassa: Mjadala wa Katiba usivuruge amani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa: Mjadala wa Katiba usivuruge amani

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Speaker, Jan 17, 2011.

 1. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Lowassa alitoa tahadhari hiyo jana wakati akifungua studio ya muziki ya FLEM, jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa hivi sasa inaoneka kuwapo kwa mashindano ya kuharibu amani kutokana na mjadala huo kupamba moto.

  Note:Huyu mtu kwa nini kila sehemu yupo?
  ufisadi yumo,kanisani yumo ndo tuseme nini sasa?


  Hiyo studio ni ya flora mbasha!
   
 2. S

  Shiefl Senior Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usisahau jamaa anatafuta hizo fora yaani sehemu zenye matukio kwa nguvu ili na mwenzenu akauze sura. Kwani hamjui kuwa jamaa anausubiri uraisi wake 2015 kwa ndoto zake. Japo binafsi nasema hizo ndoto zake zitimie ndani ya ccm
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  FLEM = Flora Emmanuel Mbasha
   
 4. n

  niweze JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  "I am Calliing out Lowasa" Amani Inachafuliwa na CCM Kutaka Kushikilia Uchaguzi na Kulipa Dowans. Lowasa Wewe Ndio Umechafua Taifa Letu Kutokana Wizi Wako....
   
 5. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  MBUNGE wa Monduli, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ametahadharisha mjadala kuhusu Katiba nchini kuwa chanzo cha kuharibu wa amani iliyoko nchini.

  Lowassa alitoa tahadhari hiyo jana wakati akifungua studio ya muziki ya FLEM, jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa hivi sasa inaoneka kuwapo kwa mashindano ya kuharibu amani kutokana na mjadala huo kupamba moto.

  Alisema kuwa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo moyo wa kuharibika kwa amani unavyozidi kuongezeka.

  Alisisitiza kuwa hata katika mijadala mbalimbali inayoendelea nchini hasa ya Katiba, wananchi wanatakiwa kupingana kwa hoja na si kwa kuhatarisha amani.

  "Tunatakiwa kutunza amani yetu kama mboni ya jicho maana hata nchi jirani za wenzetu ikiwamo Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi hawajawahi kuwa na amani kama tuliyonayo sisi, hivyo tunatakiwa kuhakikisha tunaitunza kwa uwezo wetu wote," alisema Lowassa. Katika kusisitizia hilo, aliwashauri waimbaji wa Injili kuamka la kutunga nyimbo zinazohamasisha na kuchochea utunzaji wa amani, ili iendelee kudumu.

  "Waimbaji wa Injili wanafanya kazi nzuri sana ingawa katika maisha kuna mahali unayumba, unaanguka na kupanda, lakini yote hayo ni kwa uwezo wa Mungu.

  "Hakikisheni mnatunga nyimbo za kutetea amani maana kwa sasa kila mtu ana lake analosema, vyombo vya habari vinachochea kwa njia yake, hivyo tuilinde hii amani," alisema.

  Alisema kuwa bila kuwa na amani hakuna taifa linaloweza kufikia maendeleo, hivyo jamii inapaswa kupingana bila kusababisha mvurugano.

  Alisema amani ni tunu pekee aliyotuachia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hivyo tunatakiwa kuitetea kwa nguvu zetu zote.

  Alisema kuwa ni kipindi cha ajabu sasa, kwani kila mtu amekuwa akiamka na jambo lake linaloonekana kuhatarisha amani.

  Kwa upande wake, mchungaji wa kanisa la FPCT la Mtoni Kijichi, Joseph Malundo, aliwataka wamiliki wa studio hiyo kuacha kubweteka na mafanikio hayo bali wazidi kumuomba Mungi ili azidi kuwapandisha juu zaidi.

  Alisema hatua hiyo itawezesha vijana wengi kupata ajira hasa kwa kumtumikia Mungu.
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Lowassa: Mjadala wa Katiba usivuruge amani


  na Betty Kangonga

  MBUNGE wa Monduli, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ametahadharisha mjadala kuhusu Katiba nchini kuwa chanzo cha kuharibu wa amani iliyoko nchini.

  Lowassa alitoa tahadhari hiyo jana wakati akifungua studio ya muziki ya FLEM, jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa hivi sasa inaoneka kuwapo kwa mashindano ya kuharibu amani kutokana na mjadala huo kupamba moto.

  Alisema kuwa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo moyo wa kuharibika kwa amani unavyozidi kuongezeka.

  Alisisitiza kuwa hata katika mijadala mbalimbali inayoendelea nchini hasa ya Katiba, wananchi wanatakiwa kupingana kwa hoja na si kwa kuhatarisha amani.

  "Tunatakiwa kutunza amani yetu kama mboni ya jicho maana hata nchi jirani za wenzetu ikiwamo Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi hawajawahi kuwa na amani kama tuliyonayo sisi, hivyo tunatakiwa kuhakikisha tunaitunza kwa uwezo wetu wote," alisema Lowassa.

  Katika kusisitizia hilo, aliwashauri waimbaji wa Injili kuamka la kutunga nyimbo zinazohamasisha na kuchochea utunzaji wa amani, ili iendelee kudumu.

  "Waimbaji wa Injili wanafanya kazi nzuri sana ingawa katika maisha kuna mahali unayumba, unaanguka na kupanda, lakini yote hayo ni kwa uwezo wa Mungu.

  "Hakikisheni mnatunga nyimbo za kutetea amani maana kwa sasa kila mtu ana lake analosema, vyombo vya habari vinachochea kwa njia yake, hivyo tuilinde hii amani," alisema.

  Alisema kuwa bila kuwa na amani hakuna taifa linaloweza kufikia maendeleo, hivyo jamii inapaswa kupingana bila kusababisha mvurugano.

  Alisema amani ni tunu pekee aliyotuachia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hivyo tunatakiwa kuitetea kwa nguvu zetu zote.

  Alisema kuwa ni kipindi cha ajabu sasa, kwani kila mtu amekuwa akiamka na jambo lake linaloonekana kuhatarisha amani.

  Kwa upande wake, mchungaji wa kanisa la FPCT la Mtoni Kijichi, Joseph Malundo, aliwataka wamiliki wa studio hiyo kuacha kubweteka na mafanikio hayo bali wazidi kumuomba Mungi ili azidi kuwapandisha juu zaidi.

  Alisema hatua hiyo itawezesha vijana wengi kupata ajira hasa kwa kumtumikia Mungu.
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hivi Lowasa anadhani kumsema yeye ni fisadi ndio kuvunja amani? au anadhani kumsema Rostam Aziz yule fisadi mwenzie ndio kuvunja amani?
  Na kama hilo ndilo kuvunja amani na amani ivunjike lakini tutawasema wazi kila sehemu! Asitutishe bana.
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Huyu naye!!!
   
 9. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kutunga nyimbo za Amani??
  Mamruki

  Sasa anataka watu watunge nyimbo na kuweka neno Amani huko ndani as if hajasoma Biblia vizuri.

  Yesu alisema.


  "Nawapa Amani itokayo kwa Mungu si Amani ya kidunia"

  Hapa Duniani ukifanikiwa kuzima mdomo mtu asemaye ukweli juu ya Wizi wako Uzinzi wako na Uongo wako unatoka na kutangaza kwamba sasa kuna Amani.
  Hapa Duniani Amani inapatikana kwa kuua watu wasio na hatia.

  Amani kutoka kwa Mungu ni moto wa roho uchomao maovu yote na kukuacha mweupe.
  Sasa ukiomba Amani kutoka kwa Mungu uwe tayari kushuhudia dhambi zako zikiteketea mbele ya macho yako.

  Waimbaji waimbe Imani itokayo kwa Mungu muumba wa vyote aliye asili ya yote na si mungu wetu mdogo mtakatifu mwenye enzi yote ya Pesa Tanganyika na Zanzibar aliyeenda kuhiji kinafiki Israel MH Lowassa.
   
 10. M

  Mutu JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  amani wakati wanachukuwa mali na kodi zetu ..........!!!??
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni miaka mingi mno wakua wakiwekeza katika 'Amani bila Haki' huku wakiipora nchi kila kona.

  Sasa wananchi kupiga kelele ndio anaona balaa na kuanza kutuvutisha li-blaketi la amani bila haki ili tuendelee kulala huku wakijikita kubaka uchumi.

  Lowassa mrudie Mungu na utubu ufisadi wako kwa mdomo wako. Watu wanauaua kwenye maandamano ambayo ni haki kwao ili mafisadi kuendele kulinwa. Kila roho inayopotea ni nyinyi.
   
 12. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Haki haiwezi kuwapo palipo na njaa na kiu ya haki!Leo matendo yenu mafisadi ndo yanaondoa amani tulio nayo, badilikeni na muone Tanzania ni ya wote then Amani itakuwepo. Baba wa Taifa hakutuachia amani tuu, pia madini na raslimali zote aliziacha kwa ajili ya kizazi cha kesho.
   
 13. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Rowassa anatusanii watanzania,hivi alivyo iingiza tanzania kwenye mkataba tata wa richmond hakuona anahatarisha amani ya Tanzania? Ila mjadala wa katiba anaona unahatarisha amani kwa kuwa itawashughulikia wao na wizi wao.
   
 14. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #14
  Jan 18, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Last week The guy was at mlimani city with boys and girls cheering THT, yesterday with Flora Mbasha. This same guy was in Kigamboni raising the money for mosque, then he went to Arusha to raise the money for the KKKT. As a citizen and a leader he has all the right to participate in public activities. Unfortunate we know him well, Mr want to be a president at any any cost. He is now building a foundation for the same. This is the liberine guy who doesn't deserve any chance to make public comment.

  How on the earth could he talk of peace and harmony, understandably that he is at the center of all heated debate raging the country today. Mr L colluded with Saboteur to loot the country through dubious Richmonduli deal, yet he want us to forgive him. Something intriguing about L is that, after he had the news that Dowans has been awarded tax payer money, suddenly L is on every media commenting ABC.

  Wananchi are aware that Richmonduli and Dowans are one and the same. The fact that the debate is skewed toward Dowans does not exonerate mr L for the blunder and pain he has inflicted in this nation. L should be made aware that his perseverance to shape the damaged image through the media will not help him iota. In this context I admire Nyerere for his vision, otherwise L could be a president!!

  God forbid.
   
 15. T

  Thesi JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Pesa za mafisadi kwenye uchaguzi zimewezesha kujenga studio ya nyimbo za injili?
  Hizi nyimbo za kurukaruka kama Kandabongoman au Twanga Pepeta eti watu wanamuimbia Mungu zinauharibu na Kuuahibisha ukristo. Nyimbo zimefanywa biashara ndio maana hata hatuchagui nani tunamwimbia. Badala ya kumwimbia Mungu mwenye haki tunaimba KIKWETE KIONGOZI BORA, Rostam Azizi Kiboko yao ili mradi wanamwaga pesa walizodhulumu wananchi maskini.

  Kumkaribisha fisadi EL kufungua studio iliyojengwa na pesa za uchaguzi na ufisadi si dili lingine hilo na wachungaji wanachekelea pesa zimeingia hewala.

  Kama tunataka kuwa tofauti na upande wa pili ambao kijadi ni dini inayostawisha utawala wa kiimla na dhuluma ili mradi mikono inaenda kinywani, tumbo kufura huku watu wanaimba Mungu mkubwa wakristo waache kushabikia wanasiasa mafisadi kama EL hata kama ni wakristo.
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Jan 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,971
  Trophy Points: 280
  ..itafika wakati tutaambiwa tusiende makazini na mashambani maana tunaweza kuvunja amani aliyotuachia Baba wa Taifa.
   
 17. m

  matawi JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Bravo Nguluvi Sijui kwa nini watu wanajiita wakristo au waislamu lakini wameshindwa kuwa na matendo kama ya Yesu au Mtume Muhamad. Hivi ni kweli Flora hajui Lowassa ni Mwizi? Je ni kweli studio yake haiwezi kuwa ya Maana bila ya kumwita Lowassa? Shame on you short minded Matz
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  alafu hawa viongozi wa dini wanaomkaribisha kwa nini wasimpe live kuwa anatakiwa kutubu ili aende mbinguni? Wanamuogopa nini? hu mtego wanaomwekea hadi anakwenda kwenye makanisa yao au misikiti ilikuwa ni nafasi nzuri ya kushughulikia uovu wake.
   
Loading...