BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Lowassa matatani zaidi
Waandishi Wetu Februari 27, 2008
Raia Mwema
Spika aagiza kanda za matamshi yake zitafutwe, zichunguzwe
SAKATA ya kampuni hewa ya kufufua umeme ya Richmond bado inachemka na sasa kuna uwezekano mkubwa wa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na madini, Nazir Karamagi kubanwa na Bunge kwa matamshi yao.
Raia Mwema imethibitishiwa kwamba matamshi mengine ambayo yanalianika Bunge vibaya ni ya Waziri wa Sheria, Mathias Chikawe, ambaye ameelezwa kuwa alimtetea Mwanasheria Mkuu Johnson Mwanyika aliyetajwa kuhusika katika sakata hiyo ya Richmond.
Chimbuko la hatua hiyo ya Bunge linatokana na hatua ya Lowassa kueleza, katika vyombo vya habari na katika mkutano wake jimboni kwake Monduli, Jumamosi wiki iliyopita, kwamba hakuhusika katika mkataba wa Richmond na kwamba alilazimika kujiuzulu kwa sababu ya uwajibikaji wa pamoja yeye kama mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali.
Kwa upande wake, Karamagi amekuwa akisema kwamba yeye alipohamia Wizara ya Nishati, mkataba na Richmond ulikuwa umekwisha kukamilika na kwa ajili hiyo kueleza kwamba anahusika ni suala ambalo atalipinga kwa nguvu zake zote.
Spika wa Bunge, Samuel Sitta aliliambia Raia Mwema mwanzoni mwa wiki kwamba hakuwa amepata kwa undani kuhusu matamshi ya Lowassa, Karamagi na Chikawe na hivyo asingweza kwa hakika kusema ni hatua gani inaweza kuchukuliwa dhidi yao.
Lakini alieleza, katika mahojiano ya simu kutoka jimboni kwake Urambo kwamba kwa hakika Bunge litachunguza matamshi hayo kama hayaliondolei Bunge hadhi.
Alisema kwamba yeye pia amepewa taarifa hizo na watu mbali mbali, akiwa jimboni kwake Urambo, Tabora, na kwamba hawezi kutoa tamko kwa kuwa hana ushahidi kamili wa kuona wala kusikia yeye mwenyewe.
Alisema kwamba kutokana na kukosa ushahidi huo, ameagiza wasaidizi wake watafute vielelezo vya matamshi au maandiko yanayotolewa na Lowassa na watu wengine kuhusu Kamati Teule ya Bunge iliyoichunguza Richmond.
Raia Mwema imedokezwa kwamba kuna uwezekano mkubwa watu hao wakahojiwa katika kikao kijacho cha Bunge, kutokana na kukinzana na Azimio la Bunge kuhusu Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge.
"Kwa mfano Lowassa alikuwa na fursa ya kupewa muda mwingi wa kujieleza bungeni kama kiongozi wa shughuli za Bunge. Alitakiwa ayaseme haya anayoyasema sasa, ndani ya Bunge. Sasa kuyasema nje kutamletea matatizo", anasema mwanasheria mmoja maarufu jijini ambaye pia ni mbunge.
Anaongeza: "Bunge limetoa Azimio. Ripoti ya Kamati Teule imepitishwa na Bunge. Suala lililobaki hivi sasa ni utekelezaji tu. Kujadili hilo nje ya Bunge ni contempt of Parliament (kuingilia shughuli za Bunge), Raia Mwema ilielezwa.
Kuhusu suala la Waziri Mkuu Lowassa kuhojiwa na Kamati ya Bunge, Raia Mwema iliambiwa kuwa nafasi ya Waziri Mkuu inapatikana kutokana na mwafaka unaopatikana kati ya pande mbili, yaani Rais na Bunge.
"Rais anapendekeza jina, Bunge linapitisha. Kwa hiyo, Bunge lingeamua kumhoji na kumwadhibu, basi, nafasi ya pili ya Rais inaweza kuingia kwenye chuki na Bunge, na hapa kunaweza kuwa na msuguano," alisema mwanasheria huyo.
Kamati teule inaundwa na chombo kimoja-Bunge. Angeitwa Lowassa, akahojiwa na kukutwa na hatia, angeadhibiwa, asipate hata mafao. Kutokana na hilo, Rais akikasirika inabidi avunje Bunge, kwa kuwa Waziri Mkuu ni sehemu ya uteuzi wake, Raia Mwema lilielezwa.
Wataalam wa masuala ya Bunge na sheria wanasema kwamba kwa kawaida ripoti kama hiyo ikishawasilishwa bungeni, na kuundiwa azimio, inakuwa ni mwisho, na kinachobaki inakuwa ni utekelezaji tu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, iliyoichunguza Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe aliiambia Raia Mwema wiki hii kwamba yeye hakuwa na la kusema katika suala hilo kwa vile kazi waliyotumwa na Bunge ilikwisha kukamilika.
Lowassa, Karamagi na waziri mwingine ambaye naye alilazimika kujiuzulu, Dk. Ibrahim Msabaha waliipinga ripoti iliyowatuhumu ya Kamati hiyo Teule ya Bunge.
Na juzi Jumatatu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Emmanuel ole Naiko, alisambaza taarifa kwa vyombo vya habari ikidai kwamba kuhusishwa kwake na TIC katika sakata hiyo kunatokana na njama dhidi ya wazaliwa wa Monduli.
Yeye na Lowassa ni wazaliwa wa Monduli na alipata kuwa msaidizi mkuu wa Sitta wakati Sitta alipokuwa Mkurugenzi Mkuu wa TIC.
Ole Naiko anaituhumu Kamati ya Dk. Mwakyembe kwamba ilijenga mazingira ya kuihusisha TIC na Richmond mapema.
"Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere) aliwahi kuasa kwamba chuki za namna hii ni sawa na mtu kula nyama ya mtu haishii hapo. Kama nia ni kuondoa watu wa sehemu fulani ya nchi yetu tufanye hivyo kwa kuwatendea haki na si kuwajengea mazingira ya namna hii," alisema Ole Naiko.
Baadhi ya waliozungumza na Raia Mwema wanasema maneno yanayoibuka sasa kuhusiana na Ripoti hiyo ya Bunge, ambayo tayari ina maazimio yaliyokwisha kufikishwa serikalini, ni kielelezo tu cha jinsi mgawanyiko ulivyo mkubwa serikalini na ndani ya chama tawala cha CCM.
Raia Mwema ina taarifa za vitendo vya kuchimbana kati ya makundi na wafuasi wa mawaziri waliojiuzulu na ya wale ambao wamebaki.
Habari zinasema kuchimbana huko kuna sura nyingi, lakini za dhahiri ni za kupakana matope, kwa pande zote mbili, kupitia katika vyombo mbalimbali vya habari (si Raia Mwema).
Kuna taarifa pia kwamba suala hilo la kupakana matope limemfikia Rais Jakaya Kikwete na kuna uwezekano kwamba maofisa wake wa masuala ya habari wamekuwa na mawasiliano na baadhi ya waandishi wa habari juu ya jambo hilo.