Baada ya sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kumalizika ktk uwanja wa Taifa (Uwanja wa Uhuru), kulifanyika sherehe nyingine ktk viwanja vya Ikulu Dar es salaam, sherehe hiii ilikuwa ni ya kuwatunuku NISHANI viongozi mbali mbali wastaafu waliolitumikia Taifa hili.
Nishani hii yenye HESHIMA kubwa iliyopewa jina la Mwl. J. K. Nyerere ilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete. Aliwatunuku Marais wote wastaafu, Makamo wa Rais wote wastaafu, Mawaziri Wakuu wote wastaafu, na viongozi mbali mbali. Idadi ya Nishani zilizotolewa ilikuwa ni 40.
Sherehe hizi zilizoanza majira ya saa kumi jioni zilifana sana ktk viwanja hivyo vya Ikulu, nyuso za waliotunukiwa zilionekana kujaa furaha kubwa sana, na ni dhahiri zilionesha ni kiasi gani pengo la Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere lilivyo.
JAMBO lililoushtua umati mkubwa ulioalikwa kuhudhuria na kupamba sherehe hii ilikuwa ni pale jina la Mh. Edward Ngoyai Lowasa kutokuwepo ktk orodha ya viongozi hao. Watu waliokuwa wamejikusanya ktk makundi mbali mbali walisikika wakisema kuwa "huu ndio mwisho wa Lowasa ktk medani za siasa". Wengine walisikika wakisema kuwa "Lowasa hakupaswa kukimbilia ktk kipindi maalum kilichorushwa na TBC1", kwani kufanya hivyo ni kuonesha Umma wa Watanzania kuwa anashindana na viongozi wake Wakuu, yaani Waziri Mkuu na Rais.
Baada ya mahojiano na TBC1, wananchi wengi kutoka ktk viunga vyote nchini walilipuka kwa mshangao dhidi ya kituo hiki cha habari kinachomilikiwa na Serikali kutojua au kwa makusudi kuvunja itifaki. Wengi wamekosa imani na chombo hiki, na kuona kama ni cha Mh. Edward Lowasa.
Ninaamini kuwa tutapata mawazo mengi mazuri juu ya matukio hayo mawili yaliyotokea jana, na hasa ukizingatia kuwa, mara kadhaa Mh. Lowasa amekuwa akitamba hadharani kuwa Rais Kikwete ni rafiki yake aliyetoka nae mbali, na wawili hao hawakukutana mitaani. Lakini jambo jingine hapa ni kuwa, CCM inajiandaa na uchaguzi wa viongozi wake ktk nafasi mbali mbali mwaka kesho. Uchaguzi huu utaunda timu ya ushindi wa chama hicho kikongwe utakaofanyika mwaka 2015. Kuna tetesi kuwa Mh. Lowasa anautamani saana URAIS, na hivyo ANAJIANDAA KUGOMBEA.
Viongozi wastaafu ambao bado wanaendelea na nyadhifa nyingine serikalini nao hawakupewa nishani maana si wastaafu, na Lowassa si mstaafu ni "mjiuzulu".
Kutoka gazeti la Mwananchi Disemba 11, 2011: