LOWASSA, MAALIM SEIF KUTOA TAMKO LA MUSTAKABALI WA ZANZIBAR LEO

News TZ

Senior Member
Jun 17, 2015
132
75
Siku moja baada ya baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(ZEC) kuitangaza Machi 20 kuwa siku ya marudio ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar,mgombea urais, Maalim Seif Sharif Hamad na Edward Lowassa leo wanakutana na wabunge wote kutoka vyama vinavyounda UKAWA kutoa *tamko zito* litakalotoa mwelekeo wa hali halisi ya kisiasa visiwani humo.

Awali mwenyekiti wa (ZEC) Salim Jecha alitangaza juzi kuwa marudio ya uchaguzi hayatakuwa na kampeni za wagombea wa nafasi ya Urais, uwakilishi na udiwani na wala hakutakuwa na mabidiliko yoyote ya wagombea. Habari zaidi zinathibitisha kuwa viongozi hao walitua Dodoma jana jioni tayari kwa kikao hicho ambacho kitaanza leo asubuhi.

"Ni maazimio ambayo yanayolenga kueleza ukweli ya kuhusu kinachotaka kufanyika Zanzibar. Yatakua maazimio mazito", alisema mpashaji wa habari hii.
 
watoe tu...Zanzbar siyo ya Nyanya Yao,inabidi ianzishe kampeni ya hashtag kupinga uchaguzi wa zanzibar..kwa anayejisikia kkufanya hivyo...#sayNotoReelectionZanzibar.
 
Kwanini Wazuie wasifanye kampeni? Huyo Jecha mbona anatafuta laana ya wazanzibar?
 
Back
Top Bottom