Lowassa kuua ndege wawili kwa jiwe moja?

Lowassa kuua ndege wawili kwa jiwe moja?

ni mtazamo wako.

lowassa amewashika pabaya wanachama wa vyama viwili hasimu nchini.

Moja
kwa ccm huyu jamaa amewekeza kwa wajumbe wengi iki wampitishe kugombea urais,kamati kuu ikimtosa basi ccm itakuwa vipande vipande.hili ni tishio dhahiri.Nadhani kamati kuu inaogopa kumpitisha kwani chadema yaweza kutumia kampeni dhidi ya ufisadi kumuangusha mwaka 2015.
Pia kambi za sitta,mwakyembe na membe zitachukia na kukimega chama hapo 2015.

Pili
kwa upande wa chadema mheshimiwa huyu amewahakikishia kuwa akitoswa na kk ya ccm basi ataingia chadema na washirika wake kutoka ccm na hivyo kuihakikishia chadema ushindi 2015,tujikumbushe ile kauli ya 'upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm'
Kimsingi chadema kama kilivyo vyama vyote vya siasa kina lengo la kushika madaraka kwa njia yoyote ile halali au hata ikibidi iwe haramu.kuungwa mkono na mtu mwenye nguvu ndani ya ccm ni karata muhimu sana katika kushika dola.

Anachokifanya lowassa kwa sasa ni vitu viwili...

Kuitishia ccm kwamba 'msinipopitisha nitahama chadema'

Pia kuwahaidi wanachadema kuwa ccm wakimtosa basi atagombea na kuiingiza chadema madarakani,ataserve kipindi chake na kuwaachia dola!

Hii karata ya lowassa nailinganisha na kuua ndege wawili kwa jiwe moja.

Mods tuache tujadili hii siasa !

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Unawezekana ikawa hivyo. Its win win situation. Ccm waki
lileta udini,
 
Naona wafuasi wa VIBAKA mnajaribu kuigeuza nyeusi kuwa nyeusi!

LOWASSA hasafishiki hata kwa TINDIKALI!

Hakuna watanzania wa kumchagua KIBAKA kuwa rais wa nchi,labda watanzania wa kijijini kwenu huko!
 
Naona wafuasi wa VIBAKA mnajaribu kuigeuza nyeusi kuwa nyeupe!

LOWASSA hasafishiki hata kwa TINDIKALI!

Hakuna watanzania wa kumchagua KIBAKA kuwa rais wa nchi,labda watanzania wa kijijini kwenu huko!
 
Binafsi mpaka Leo sielewi kwa nini watanzania ni wepesi sana kusahau. Kilichomfanya huyu Mhe. Lowasa kujiuzulu PM ni kwa sababu ya ufisadi, Richmond. Kitu kinaendelea hadi Leo hii tumepandishiwa umeme kwa unit moja Tsh 306 hacha charge nyingine Kama rea, vat, ewura...Je akishika nchi si tutakula majangili?

Tanga 1995 Baba wa Taifa alisema huyu jamaa hafai kuwa Rais maana ni fisadi. Miaka ya 85, baba yake mzazi alimshtaki kwa uongozi wa nchi, kisa kujenga nyumba Kubwa monduli wakati akiwa aicc. Kama baba yake mzazi amemuona ni fisadi kwa nini sisi watz tunamgombania?

KWA NIABA YA FAMILIA YANGU NAKUSHUKURU SANA kwa KUWEKA FITNA KANDO NA KUAMUA KUWA MKWELI .
 
Boys2men unawakumbuka hao mwaka 1995 urais wa wote lazima wakabidhiane vijiti
 
Invisible sielewi kwa nini threads kama hizi hazionekani jukwaani na kwa mleta thread
 
Last edited by a moderator:
Ndg, ni saidieni nielewe! Lowasa anahusishwa vp kuongoza nchi wakati aliondoka madarakani kwa kashfa ya ufisadi (Rich)?
NGOJA TUKUELEWESHE - HAKUONDOKA KWA KASHFA YA UFISADI - ALIONDOKA KWA KUWAJIBIKA KWA MAKOSA YA WATU WALIYOKUWA CHINI YAKE KAMA AKINA NAHODHA WALIVYOONDOKA MAJUZI. HATA MAKYEMBE ALISEMA HIVYO......, KAMA KWELI UNATAKA UELEWESHWE ENDELEA KUSOMA CHINI HAPA....

Dr. Mwakyembe alimsafisha Lowassa kuhusu ufisadiKampuni ya Richmond
Pamoja na baadhiya wabaya wake Lowassa kung’ang’ana kwamba Ripoti ya Dr. Mwakyembe ndiyoiliyomhukumu Lowassa kwamba alitumia ufisadi kwenye upatikanaji wa kampuni fekiya Richmond, ukweli ni kwamba Kamati Teule ya Dr. Harrisson Mwakyembeilimsafisha Lowassa kwa ufisadi kwenye ripoti yao ya mwaka 2008. Kwa hiyoinashangaza kwamba kwa muda wote huu baadhi ya wanasiasa, wananchi na vyombovya habari vimeendelea kuitaja ripoti ya Mwakyembe kwamba ndiyo iliyomtiaLowassa kwenye hatia ya ufisadi kwenye sakata hilo.
Mtu yeyote aliyesikilizamajadiliano hayo Bungeni au anayeweza kutafuta Taarifa Rasmi ya Bunge (Hansard)wakati wa hitimisho la mjadala huo Bungeni mwaka 2008, ataona ukweli kwamba KamatiTeule ya Dr. Harrison Mwakyembe iliyokuwa inachunguza sakata la mkataba wakufua umeme baina ya TANESCO na kampuni ya Richmond ilimsafisha Edward Lowassa,kwamba hakuwajibika na kujiuzulu kutokana na ufisadi wake katika sakata hilo,bali aliwajibika kisiasa kwa makosa ya watu waliokuwa chini yake.
Tarehe 15Februari 2008, kwa mujibu wa taarifa rasmi za majadiliano Bungeni (Hansard),Dr. Harrison Mwakyembe, wakati akihitimisha hoja ya Kamati Teule iliyochunguzasuala la Richmond, alisema:
“MheshimiwaSpika, ninaomba nianze na utangulizi mfupi na rahisi; uwajibikaji kwa viongoziwaandamizi katika nchi zinazolinda na kuenzi demokrasia kama vile Tanzania, unasura mbili; sura ya kwanza, kiongozi anawajibika kwa makosa yake mwenyewe yakiutendaji. Kiongozi anafanya maamuzimabaya, pengine kwa kishawishi cha pesa, maamuzi yake yakaleta hasara aukiongozi ameshindwa kutoa ushauri mzuri kama kiongozi, kwa kukiuka kanuni,kukiuka taratibu na kadhalika, matatizo yakatokea, anawajibika. Sasa sura hii ya uwajibikaji, inahusishauvunjwaji wa maadili, kanuni, sheria, miiko ya uongozi na kadhalika. Chini ya uwajibikaji wa aina hii, kiongozianaweza akashitakiwa, akaadhibiwa mbali na kuachia ngazi. Nitarejea kwenye sura hii hivi punde. Suala la msingi hapa ni kuwa, kuna element ya adhabu katika sura hii ya kwanza.
“Suraya pili; kiongozi anawajibika kwa makosa ambayo si yake moja kwa moja ilayaliyofanywa na watendaji chini yake. Kitendo cha kuwajibika kwa aina hii, kunaijengea Serikali au taasisiheshima na imani ya pekee katika jamii, kunatoa picha ya kwamba, uongoziunajali, unalielewa tatizo kwa kubeba lawama wao wenyewe. (Makofi)
“MheshimiwaSpika, katika suala hili la Richmond, viongozi wa Wizara ya Nishati na Madinina Waziri Mkuu, walikuwa wanakabiliwa na uwajibikaji wa aina hizo mbili. Kwanza, uwajibikaji unaotokana na makosa yaviongozi wenyewe katika maamuzi yao, maelekezo yao, maagizo yao nakadhalika. Mawaziri wote wawili waNishati na Madini; aliyetangulia na aliyefuatia baadaye, Katibu Mkuu naKamishina wa Nishati, wote tukawaona wana makosa ya moja kwa moja, waliyoyafanyawao kwa njia moja au nyingine. Kwa kuwauwajibikaji wa aina hii, unatokana na ukuikwaji wa kanuni, taratibu, maadili,sheria na kadhalika, Kamati Teule ikahakikisha inawahoji wote ili kusikia their side of the story kabla ya kutoa pendekezo la kuwawajibishakwa makosa waliyofanya. Ndiyo maanabaada ya kuwahoji, tumependekeza hatua za kuchukuliwa dhidi yao.
“Halihaikuwa hivyo kwa Waziri Mkuu; Kamati teule ilikuwa na ushahidi wa mawasilianoya karibu kati ya Waziri Mkuu na Uongozi wa Wizara. Ushahidi huo haukutosha kwa uwajibikaji wasura ile ya kwanza wa kiongozi kukutwa na makosa ya moja kwa moja, aliyoyafanyayeye mwenyewe kwa njia moja au nyingine, lakini ushahidi huo ulitosha kwauwajibikaji wa sura ya pili, ambao hauhitaji mahojiano, kusikilizwa walautetezi. Unawajibika kwa makosa yawatendaji walio chini yako. Hiyo ndiyodemokrasia. Wabunge wengi wametoa mifanomingi hapa, ukiwemo wa Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, alipokuwa waziri wa Mamboya Ndani; aliwajibika kwa makosa ya askari huko Shinyanga wakati yeye alikuwaDar es Salaam; hatukumsikia akidai apewe nafasi ya kusikilizwa na hata kamaangepewa, bado angewajibika yeye mwenyewe. (Makofi)
“MheshimiwaSpika, Kamati Teule inatamka ukurasa wa 37 wa taarifa yake kuwa, ninanukuu‘Ushiriki huu wa karibu wa Waziri Mkuu katika kila hatua ya zabuni ya umeme wadharura si lazima uwe ushahidi wa kwamba, kiongozi huyo wa Kitaifa alihusikakatika kuibeba Richmond. Unaweza piaukawa ushahidi wa style yake ya kawaida kabisa ya Waziri Mkuu katika kufuatiliamasuala yote ya Kitaifa kwa karibu sana, tukizingatia kwamba, nchi wakati huoilikuwa katika kipindi kigumu sana cha ukosefu wa umeme…..”
Ni wazi basikwamba Mwakyembe alimsafisha Lowassa kwamba makosa yake hayakuangukia kwenyesura ya kwanza ya uwajibika, ya kiongozi kuwajibika kwa makosa yakemwenyewe. Sura hii ndiyo unayoweza hata ukamwitamtu fisadi. Lakini Lowassa aliwajibikakwa makosa ya watendaji walio chini yake kama alivyoeleza vizuri Dr.Mwakyembe. Anayewajibika kwa aina hii yapili huwezi kumwita fisadi. Akisifu ainahii ya Edward Lowassa kuwajibika, Dr. Mwakyembe alisema, “…Kitendo cha kuwajibika kwa ainahii, kunaijengea Serikali au taasisi heshima na imani ya pekee katika jamii,kunatoa picha ya kwamba, uongozi unajali, unalielewa tatizo kwa kubeba lawamawao wenyewe”. (Makofi). Mwakyembe anakwenda mbali na kuhusishauwajibikaji huu wa Lowassa na ule wa Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Naye Waziri MkuuMizengo Pinda, akiwasilisha utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu suala hilotarehe 28 Agosti 2008 alisema yafuatayo kuhusu azimio na. 16 la Waziri Mkuukupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huo, “Mheshimiwa Naibu Spika, hatuazilizochukuliwa ni kwamba, Azimio hili lilitekelezwa mwezi Februari, 2008 kwakuwa aliyekuwa Waziri Mkuu aliamua kujiuzulu kwa kuwajibika kisiasa kwa maslahiya Taifa.”
Kwa kauli hiyoya Waziri Mkuu, ni wazi hata Serikali ilikubaliana na Kamati Teule kwamba Mhe.Lowassa aliwajibika, siyo kama fisadi bali aliwajibika kisiasa kwa maslahi yaTaifa. Ndiyo maana Azimio na. 16lililomhusu Waziri Mkuu halikuendelea kujadiliwa Bungeni. Hata wanaodai kwamba baadaye Spika aliondoahoja hii Bungeni kabla halijakamilika, wanajua kwamba suala la Waziri Mkuukuwajibika (Azimio na. 16) halikuwemo tena, na kwa hiyo hata hoja ya Richmondingeendelea kuwa Bungeni Lowassa asingeguswa tena.
 
mkuu ronaldo nimekukubali,we ndo ronaldo kweli japo cyo mchezaji wa mpira wa miguu ni mpira wa kisiasa!!nafikir sahv atakuwa amekusom baada ya kumchambulia
 
Unawezaje kuthibitisha tuhuma za lowassa kama mahakama yenye jukumu hilo haijafanya?yy kwa sasa ni mtuhumiwa tu na haijathibika kuwa na hatia,,,,,,pili kwa swala la chadema kumshinda kirahisi hilo sahau pia maana si rahisi kama unavyofikiria..kwa sasa hakuna mpinzani madhubuti wa Lowassa
 
Nani msafi ccm kama mkulu mwenyewe c msafi?kwa chadema sahau..kama mnaweza kubadili katiba ya chama ili kuondoa ukomo mtashindwaje kwenye katiba ya nchi...napata shida na chadema ingaje siingi mkono ccm
 
Lowassa ana tamaa tu ya kuishi magogoni lakini system ndio inayomuweka mtu madarakani na sio chama wala cc kwani mwaka 1995 cc ya Ccm haikuwa inamfahamu Mkapa lakini ndie aliyekuwa Rais wa 3. Lakini Lowassa afya yake ina dhoofu kila siku hata kama anapata kampani kubwa kutoka kwa Rostam na harambee zao za kuungwa mkono na marafiki ni strategies za kizamani kidogo

Pole sana kwa ugonjwa uliona put that in ur mind lowassa z da best a.k.a the nxt president 2015.
 
Wewe usafi wako uko wapi?Thibitsha tuhuma zake
 
ni mtazamo wako.
CCM wakimpitisha Lowassa wanashinda urais, pia hata wasipo mpitisha sina hakika kama anaweza kuhama chama na kusupoti upinzani maana kwa wana CCM maslahi ya chama huwa mbele kuliko ya mtu binafsi. Pia anaogopa akiunga mkono upinzani CCM ikashinda atashughulikiwa kuhusu mali zake. Kama ingekuwa rais kuhama chama hata kikwete 1995 alipo enguliwa kura za maoni na kuwekwa Mkapa angechukia na kuhama chama lakini kwa kuweka mbele maslahi ya chama alijikaza kiume.
 
Jamani umeme umepanda beiiii,umeme unakatika kila siku

Ingekuwaa vizuri zaidi Lowassa akawekeza pesa zake kwenye umeme ili umeme ushuke sio kila siku kugawaa pesaa hovyo hovyoo tu
 
CCM wakimpitisha Lowassa wanashinda urais, pia hata wasipo mpitisha sina hakika kama anaweza kuhama chama na kusupoti upinzani maana kwa wana CCM maslahi ya chama huwa mbele kuliko ya mtu binafsi. Pia anaogopa akiunga mkono upinzani CCM ikashinda atashughulikiwa kuhusu mali zake. Kama ingekuwa rais kuhama chama hata kikwete 1995 alipo enguliwa kura za maoni na kuwekwa Mkapa angechukia na kuhama chama lakini kwa kuweka mbele maslahi ya chama alijikaza kiume.
mkuu siipendi ccm ila kangu mimi kikwete ni kiongozi wa aina yake.
kumbuka hata 1995 alikuwa na kundi lake lakini baada ya nyerere kumpitisha mkapa bado aliweza kulivunja kundi lake na akafanya kazi na mkapa bila kumsumbua. kumbuka kikwete alikuwa na ushawishi mkubwa sana katika chama. lakini angalia hao waliokuwa na makundi baada ya yeye kushinda kama waliyavunja. kelele zote tunazozisikia ccm ni kwa sababu ya makundi.
 
lowassa amewashika pabaya wanachama wa vyama viwili hasimu nchini.

Moja
kwa ccm huyu jamaa amewekeza kwa wajumbe wengi iki wampitishe kugombea urais,kamati kuu ikimtosa basi ccm itakuwa vipande vipande.hili ni tishio dhahiri.Nadhani kamati kuu inaogopa kumpitisha kwani chadema yaweza kutumia kampeni dhidi ya ufisadi kumuangusha mwaka 2015.
Pia kambi za sitta,mwakyembe na membe zitachukia na kukimega chama hapo 2015.

Pili
kwa upande wa chadema mheshimiwa huyu amewahakikishia kuwa akitoswa na kk ya ccm basi ataingia chadema na washirika wake kutoka ccm na hivyo kuihakikishia chadema ushindi 2015,tujikumbushe ile kauli ya 'upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm'
Kimsingi chadema kama kilivyo vyama vyote vya siasa kina lengo la kushika madaraka kwa njia yoyote ile halali au hata ikibidi iwe haramu.kuungwa mkono na mtu mwenye nguvu ndani ya ccm ni karata muhimu sana katika kushika dola.

Anachokifanya lowassa kwa sasa ni vitu viwili...

Kuitishia ccm kwamba 'msinipopitisha nitahama chadema'

Pia kuwahaidi wanachadema kuwa ccm wakimtosa basi atagombea na kuiingiza chadema madarakani,ataserve kipindi chake na kuwaachia dola!

Hii karata ya lowassa nailinganisha na kuua ndege wawili kwa jiwe moja.

Mods tuache tujadili hii siasa !

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!


Woga huu kwa upinde wa CCM ndio uliowafanya tupate raisi tulienaye hivi leo
 
Back
Top Bottom