Lowassa: Kuimarika kwa UKAWA kunawatia hofu kubwa CCM

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
WAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, amesema kasi ya kuimarika kwa umoja na mshikamano miongoni mwa vyama vya upinzani nchini, kunaitia kiwewe CCM kiasi cha kuanzisha mbinu chafu za kisiasa.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Kahama katika Hoteli ya Gaprina ambapo alifikia kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani Kagera katika ziara ya kuimarisha chama chake.

Alisema kuimarika kwa mshikamano huo chini ya mwavuli wa Vyama Vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ni hatua kubwa katika kuelekea kuing’oa CCM.

“Wameanza mbinu zao za kutaka kutuondoa katika umoja wetu, wameanza kuwalisha viongozi wetu maneno, mfano gazeti (nalitaja jina) la leo (jana) wamenilisha maneno ya kwamba eti nimeitabiria CCM ushindi katika uchaguzi mdogo wa udiwani kule Arumeru.

“… mambo ya ajabu kabisa hili gazeti linaishi kwa kodi zetu sisi wananchi leo linaamua kutumika kuvunja demokrasia inasikitisha sana.

“Wanaandika uongo mchana kweupe kuwa nilikuwa katika kampeni kwenye kitongoji Ematasia..mimi sikwenda huko..lakini mbinu zao hizi wananchi wameshazijua na hawako tayari kuona hamu yao ya kupata mabadiliko inapotea,” alisisitiza.

Wakati huo huo mamia ya wakaazi wa mji wa Kahama waliizingira Hoteli ya Gaprina alikofikia Lowassa, wakiwa na nia ya kutaka kumwona.

Akiwa njiani kuelekea Bukoba, Lowassa na msafara wake alipata nafasi ya kusalimiana na wananchi katika mnada wa Lusaunga wilayani Biharamlo, ambako wananchi hao walimwambia kuwa hali yao ya maisha ni ngumu pamoja na hali mbaya ya ukame inayowakabili.

Hata hivyo Lowassa hakutoa kauli yoyote kwao zaidi ya kusema kwa sasa mikutano ya hadhara imepigwa marufuku na asingependa kuvuja sheria kwa kile alichodai amri kandamizi.
 
2017-01-13-09-30-27-2073905467.jpeg

Raisi wangu.

swissme
 
Hili swali sijawahi kulipatia jibu, hivi kweli ipo siku ccm itaachia madaraka,tena kwa katiba hii iliopo ............Mwenye uwezo wa kutabiri hili aniambie tafadhari.
 
Hili swali sijawahi kulipatia jibu, hivi kweli ipo siku ccm itaachia madaraka,tena kwa katiba hii iliopo ............Mwenye uwezo wa kutabiri hili aniambie tafadhari.
CCM haitatoka madarakani kwa karatasi kamwe haitakuwa hivo
 
Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa, amesema kuimarika kwa umoja na mshikamano miongoni mwa vyama vya upinzani nchini kunawatia kiwewe Chama cha Mapinduzi (CCM), wanaoongoza serikali na kufanya waanzishe mbinu chafu za kisiasa.

Aidha, Lowassa amesema kuimarika kwa mshikamano huo chini ya mwamvuli unaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ni hatua kubwa katika safari ya kuiondoa CCM madarakani na kuingia Ikulu ili waweze kuongoza dola.

“Wameanza mbinu chafu za kutuondoa kwenye umoja wetu kwa kuwalisha viongozi wetu maneno, kuna gazeti moja limenilisha maneno likidai kuwa eti nimeitabiria CCM ushindi katika uchaguzi mdogo wa Udiwani kule Arumeru, haya ni mambo ya ajabu kabisa, linaishi kwa kodi zetu wananchi leo linatumika kuvunja Demokrasia,hili ni jambo la kusikitisha,”amesema Lowassa.

Lowassa amesema lengo la ziara hiyo wanayofanya ni kuimarisha chama na kuimarisha mshikamano miongoni mwa wapinzani wa CCM ambao wanapata kiwewe na kusisitiza kuwa hata iweje mabadiliko ni lazima.

Hata hiyo Lowassa alipata nafasi ya kusalimiana na wananchi mbalimbali akiwa njiani kuelekea mkoani kagera kwaajili ya ziara ya kuimarisha chama.
 
CCM haitatoka madarakani kwa karatasi kamwe haitakuwa hivo
Uko sahihi,tena kuna uwezekano hata wapinzani wanalijua hili kwamba hawataingia madarakani kwa karatasi ila tu wameamua na wenyewe kujiajiri kwa kupata posho. Wapinzani wanajua fika kuwa kwa KATIBA ILIOPO haiwaruhusu wao kuingia madarakani na hawaonekani kulipigania hilo,ila wako wanapambana na kauli za "mtukufu" tu. Kwa KATIBA HII,tena ukiangalia na mwenendo wa muheshimiwa "mtukufu" KAMA WAPINZANI HAWAJAFANYA MOJA KATI YA HAYA. (1) KUPIGANIA KATIBA "WEZESHI" AU (2) KUFANYA MAAMUZI KAMA YA WAARABU.
 
Na Mwandishi Wetu-KAHAMA

WAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, amesema kasi ya kuimarika kwa umoja na mshikamano miongoni mwa vyama vya upinzani nchini, kunaitia kiwewe CCM kiasi cha kuanzisha mbinu chafu za kisiasa.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Kahama katika Hoteli ya Gaprina ambapo alifikia kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani Kagera katika ziara ya kuimarisha chama chake.

Alisema kuimarika kwa mshikamano huo chini ya mwavuli wa Vyama Vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ni hatua kubwa katika kuelekea kuing’oa CCM.

“Wameanza mbinu zao za kutaka kutuondoa katika umoja wetu, wameanza kuwalisha viongozi wetu maneno, mfano gazeti (nalitaja jina) la leo (jana) wamenilisha maneno ya kwamba eti nimeitabiria CCM ushindi katika uchaguzi mdogo wa udiwani kule Arumeru.

“… mambo ya ajabu kabisa hili gazeti linaishi kwa kodi zetu sisi wananchi leo linaamua kutumika kuvunja demokrasia inasikitisha sana.

“Wanaandika uongo mchana kweupe kuwa nilikuwa katika kampeni kwenye kitongoji Ematasia..mimi sikwenda huko..lakini mbinu zao hizi wananchi wameshazijua na hawako tayari kuona hamu yao ya kupata mabadiliko inapotea,” alisisitiza.

Wakati huo huo mamia ya wakaazi wa mji wa Kahama waliizingira Hoteli ya Gaprina alikofikia Lowassa, wakiwa na nia ya kutaka kumwona.

Akiwa njiani kuelekea Bukoba, Lowassa na msafara wake alipata nafasi ya kusalimiana na wananchi katika mnada wa Lusaunga wilayani Biharamlo, ambako wananchi hao walimwambia kuwa hali yao ya maisha ni ngumu pamoja na hali mbaya ya ukame inayowakabili.

Hata hivyo Lowassa hakutoa kauli yoyote kwao zaidi ya kusema kwa sasa mikutano ya hadhara imepigwa marufuku na asingependa kuvuja sheria kwa kile alichodai amri kandamizi.
 
Hata kuiba kuna kiwango chake.

Wananchi wakiamua kama walivyoamua Dar, Arusha na Mbeya, hata kuiba hakutawasaidia.
 
Huyu Mzee ni wa ajabu sana ! Wenzie wanamwaga mitusi kwa wananchi lakini yeye walaaaa !!!!
 
Lowasa sio muongoni mwa wana ukawa,na hawezi kuimarisha ukawa bali kubomoa tu.huyu ndio chanzo cha Dr.slaa kuacha siasa na ndio chanzo cha mgogoro Cuf.huyu hawezi kuongea kitu mbele ya waasisi wa ukawa
 
Kwa KATIBA HII,tena ukiangalia na mwenendo wa muheshimiwa "mtukufu" KAMA WAPINZANI HAWAJAFANYA MOJA KATI YA HAYA. (1) KUPIGANIA KATIBA "WEZESHI" AU (2) KUFANYA MAAMUZI KAMA YA WAARABU.
Umeongea sahihi hasa hilo la pili Mapinduzi kama ya waarabu. Maana hilo la kwanza Mtukufu hawezi kulikubali alishalikataa hata kwenye kampeni hakulinadi japo lipo kwenye Ilani ya CCM, ni muhimu wapinzani wangejito kwenye uongozi na uchaguzi zote ili wananchi wapiganie haki zao wenyewe kama waarabu nchi itakomboka hii.
 
Back
Top Bottom