LOWASSA kuiambia CCM "Mwenye Nguvu Mpishe" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LOWASSA kuiambia CCM "Mwenye Nguvu Mpishe"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kashaijabutege, Mar 16, 2012.

 1. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Edward Ngoyai Lowassa (fisadi pacha) amerudi kwa kishindo kutoka ughaibuni alikoenda kwa ajili ya matibabu ya macho. Amewajulisha adui zake wa kisiasa, nafikiri ndani ya CCM, kuwa yuko tayari kwa "mapambano". Alikunja ngumi kama ishara ya kuonesha kuwa yuko "fit and fine" (buheri wa afya); na akatamba kuwa atayathibitisha hayo huko Arumeru Mashariki.

  Nape na wenzake wamekuwa wakipiga kelele kwa kumtaja Lowassa kuwa ni kati ya "wanachama wachafu" wanaopaswa kuacha nafasi za uongozi ndani ya CCM, kama njia mojawapo ya kukisafisha chama; au kama wenyewe wanavyosema, "kujivua gamba". Rostam Aziz, aliyekuwa Mbunge wa Igunga, yeye katangulia kujivua nafasi zake zote za uongozi katika chama ili "aachane na siasa uchwara". Pacha mwingine Andrew Chenge, maarufu kama Mzee wa Vijisenti, yuko kimya anasubiri yeyote amguse ili alianzishe; yaani wamwage ugali, naye amwage mboga. Lowassa yeye amewazidi wote kwa ujasiri. Ana roho ya paka. Ameonesha wazi kuwa anataka kuwa "Rais ajaye". CCM kimeonesha kumgwaya. CCM kiko kimya.

  Lowassa aliporudi jana, ametamka wazi wazi kuwa anayemzushia kuwa afya yake ina mushkeli basi akaone kuwa yuko "fit and fine" huko Arumeru Mashariki. Ninahisi alimaanisha kwenda kumpigia debe mkwewe, ambaye amempigania kwa "remote ya rushwa" mpaka akapata nafasi ya kugombea kwa tiketi ya CCM.

  Ni wazi kuwa CCM, hii ya sasa, haitakuwa na uwezo wa kumzuia mtu iliyemtangaza mchafu kupanda jukwaani kumnadi mgombea wao. Nape na "walokole" wenzie watafyata mkia. Nina imani kuwa Jumamosi hii, watatuma ujumbe mzito wa kwenda kumpa pole "mzee" na safari na kumtaka hali, na ZAIDI, kumuomba asaidie kutoa chochote ili wakabiliane na "chama ambacho William Sarakikya hakipendi". Watamsifu; watamwambia uko "fit and fine"; mzee unaonekana "una afya kuliko wakati mwingine wowote". Watampamba; naye atawapa chochote. Mwisho kabla ya kuaga watamwomba wiki ijayo akawasidie jukwaani. Watamwambia "mzee tumechunguza na kuona unakubalika". Atacheka kidogo, na atawajibu "sawa".

  Lowassa wiki ijayo atapanda jukwaani. Atamnadi mkwewe. Nape na wenzie watakula matapishi. Watakaa kimya. Ila moyoni watajisemea "MWENYE NGUVU MPISHE".

  Mie nikimwona Lowassa jukwaani wiki ijayo nitakumbuka maneno ya kwenye kitabu cha KULI; "YANA MWISHO".
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Lowassa si fisadi kama unavyotaka kutuaminisha. 2015 utajuta.
   
 3. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Uko sahihi kwa mtazamo wako kwani "mwenye nguvu mpishe".
   
 4. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 10,189
  Likes Received: 10,378
  Trophy Points: 280
  Ndugu unajitahidi kumfagilia Lowassa lakini atakuwa kiongozi tu wa CCM na sio Rais wa Tanzania. Na kama huamini utaona kama Ocampo hatatia team hapa bongo. Tusubiri tuone.
   
 5. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ocampo?????:A S 13:
   
 6. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ahsante kwa kulijua hilo.
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  2015 Lowassa atakuwa His Excellency, The President Of United Republic Of Tanzania. Ukweli mchungu eeh, utaumeza tu.
   
 8. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  "Niko fit and fine kuliko wakati mwingine wowote ule na niko tayari kwa mapambano"-ENL
   
 9. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Upuuzi tu hakuna kitu!!

  Stroke imemkomesha huyu masai!!
  Akubali tu kuwa ni mgonjwa lakini anaendelea vizuri!!
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
 11. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,544
  Likes Received: 10,475
  Trophy Points: 280
  mtu alie fiti anatembe kama amekakamaa huyo atakuja kufia jukwaani
   
 12. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,298
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Aliyekuwa wa kwanza kumchafua mh. Lowasa ndiye atakayemchana nyewele na kumpa mh. Lowasa kioo ajiangalie kama kweli amependeza na atamfungulia mlango na Lowasa atatoka kwenda kugombea urais kwa tiketi ya CCM.
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Utakufa wewe na utamwacha Lowassa akidunda.
   
 14. m

  mharakati JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  hawezi kua Rais wala mgombea wa CCM 2015 hata kama asipokufa now and then
   
 15. a

  african2010 Member

  #15
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  14 " ‘Ninapomwambia mwovu: "Hakika utakufa," naye kwa kweli ageuke na kuiacha dhambi yake na kuendelea kutenda haki na uadilifu, 15 naye mwovu arudishe kitu kile kilichowekwa rehani, alipe vitu vile vilivyochukuliwa kwa unyang'anyi, naye kwa kweli atembee katika sheria za uzima kwa kutotenda ukosefu wa haki, hakika ataendelea kuishi. Yeye hatakufa. 16 Hakuna yoyote kati ya dhambi zake alizozitenda itakayokumbukwa juu yake. Yeye ameendelea kutenda haki na uadilifu. Hakika ataendelea kuishi.' Ezekieli 33.14
   
 16. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280

  Duuh umenikumbusha mbali sana! Ila ni kweli kila kitu kina mwisho tupende tusipende
   
 17. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ocampo atakuja kumkamata Ali Hassan Mwinyi kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1987 katika eneo la Mkomazi game reserve, kwa eti sababu ya kuunda mbuga aliamura majeshi yaue, yachome miji, ubakaji na vitendo vingine vingi vya uvunjaji mbaya wa haki za binadamu... naona na mwanae anatumaliza kwa mabomu Dar na hata ndoto ya kujiuzulu hamna.
   
 18. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  mkali uniPM unistue kama washaanza kugawa noti! unipe na mchoro wa prosija!
   
 19. PakiJinja

  PakiJinja JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 834
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 80
  Dah nilimuona akitembea kwa tahadhari kama vile anashuka ngazi au tumbo limechafuka...
   
 20. commited

  commited JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,619
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  sisiemu wote ni wawa kuny .nga tu hakuna aliye msafi hata mmoja. Waliibia taifa mpaka limebaki mifupa nashangaa tuvyoendelea kuwa chekea was..zi hawa wasio na chembe hata moja ya huruma kwa walalahoi
   
Loading...