shikulaushinye
JF-Expert Member
- Aug 29, 2014
- 828
- 456
Lowassa kiongozi asiyetufaa?
Na M. M. Mwanakijiji - Imechapwa 21 July 2010
Kisima cha Mjadala
MBUNGE wa Monduri, Edward Lowassa ameibuka.
Amedai tena kwamba hata akiamshwa usingizini leo hii na kuulizwa kama angebadili maamuzi yake na jinsi alivyoshughulikia suala la Richmond, bado maamuzi yake yatakuwa yaleyale. Anasema, hajutii alichokitenda. Ndivyo alivyonukuliwa na vyombo vya habari mwishoni mwa wiki iliyopita.
Lowassa hataki kutambua hata kosa moja ambalo alilifanya kwa sababu amejiaminisha kuwa hakufanya kosa lolote; kujiuzulu kwake kulitokana na makosa ya âwatendaji walio chiniâ yake. Kwa maneno mengine, kama leo angekuwa waziri mkuu na bado nchi inakabiliwa na tatizo la nishati ya umeme, basi angelishughulikia vile vile na kwa namna ile ile.
Sasa yumkini Lowassa hakuwa fisadi katika sakata la Richmond, yumkini hakunufaika kifedha na mkataba ule. Na yumkini alifanya yote âkwa nia njema.â
Na kwa ajili ya mjadala wangu leo naomba tukubaliane kuwa Lowassa hakuwa fisadi. Wala hakufanya jambo kwa nia ya ufisadi. Lakini hata tukimkubalia hilo, bado ukweli unasimama kuwa alikuwa ni kiongozi mbaya na ambaye hakutufaa.
Maamuzi yake kama kiongozi yanathibitisha kuwa alistahili kujiuzulu kabla ya Kamati Teule ya Bunge kuundwa kwa sababu alikuwa na maamuzi yaliyoongozwa na hisia na siyo utaratibu wa sheria.
Kwanza, anataka kuhalalisha uamuzi wake kwa kile alichokiita, âdharura ya umemeâ na kutokana na dharura ile aliamua kufanya mambo kinyemela. Ukimsikiliza Lowassa vema utagundua kwamba suala la dharura ya umeme lilingundulika mara baada ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuingia madarakani Desemba 2005.
Hilo si kweli. Dharura haikuanza wakati wa Kikwete na siyo kina Lowassa waliyoigundua. Tatizo la uhaba wa nishati ya umeme lilijulikana wakati wa utawala wa rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Mara baada ya kugundulika huko, serikali ilianza mchakato wa kupata kampuni ya kufua umeme ambapo kampuni ya CDC Globeleq kutoka nchini Canada ilipewa tenda ya kufua umeme wa megawati 74 katika eneo la Ubungo, Dar es Salaam. Kampuni ya CDC Globeleq ni kampuni mama ya Songas; iliahidi kuingiza umeme wake katika gredi ya traifa kabla ya Aprili 2006. Mkataba kati ya CDC na serikali ulitamka wazi, kwamba mitambo itakayoagizwa itakuwa mali ya serikali mara baada ya mkataba kumalizika.
Tatizo lilianza pale Kikwete na serikali yake walipoingia madarakani. Baraza la mawaziri likaja na hoja, kwamba âCDC Globeleq ikubali kuiuzia serikali mitambo yake au iikodishe kwa bei ambayo serikali ingeridhika nayo na siyo kwa kipindi cha miaka mitano, bali kipindi kile tu cha matatizo ya umeme kutokana na ukame.â
Lakini aliyetumwa kupeleka ujumbe huo kwa CDC Globeleq akapeleka ujumbe mwingine. Akasema serikali imeamua kutoendelea na mkataba na kampuni hiyo. Hilo lilikuwa ni kinyume na maekelezo ya Baraza la Mawaziri ambalo Lowassa alikuwa mjumbe. Hadi leo hii, Lowassa hajaeleza ni kwanini alipindisha maamuzi ya baraza.
Maana hawezi kudai alikuwa hajui kilichopelekwa CDC Globeleq, kwa sababu barua zote zilinakiliwa kwake. Jambo hili ni muhimu kueleka kwa sababu mbili kubwa. Kwanza, kama mkataba wa CDC Globeleq ungetekelezwa ipasavyo na kama na kama Lowassa angemsahihisha waziri wa nishati na madini wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha kwa kumwaambia uamuzi wa baraza la mawaziri haukulenga kuifuta kazi CDC, basi Richmond isingekuwapo.
Pili, kama mkataba usingesitishwa, tuhuma za ufisadi dhidi yake zisingetolewa, Kamati Teule isingeundwa na Lowassa angeendelea na nafasi wazifa wake na bila shaka kelele hizi za sasa zisingekuwapo. Lakini leo anapokuja na kutuambia kuwa angeweza kushughulikia suala la Richmond namna ileile na kuwa hajutii maamuzi yake, basi ni wazi ana tatizo katika uongozi.
Kama waziri mkuu hasimamii maamuzi ya baraza la mawaziri kama yalivyo kutokana na kisingizio cha dharura, huyo hawezi kuwa msaidizi sahihi wa rais. Leo hii anatuambia kwa kiburi cha kiuongozi au kujiamini kuwa kama hali hiyo ikitokea tena atarudia maamuzi yaleyale, na kwamba hayuko tayari kuona makosa yake, basi huyo hatufai.
Si kwa sababu ni mtu mbaya, mume mbaya, mzee mbaya, au mbunge mbaya. Bali, ni kwa sababu ni kiongozi asiyefuata maadili.
Kwa kuendelea kuwabebesha lawama watumishi waliokuwa chini yake kuwa ndio waliofanya makosa na kuwa yeye aliwajibika kutokana na makosa yao, Lowassa amefumba macho kabisa hataki kuangalia makosa yake yeye mwenyewe.
Na kwa vile sasa anajifanya hajui alichokosea wakati inajulikana wazi kuwa yeye ni âmhusika mkuu,â hatuna budi kubakiwa na hitimisho moja tu: Huyu hatufai.
Ni kwa sababu taifa hili linahitaji viongozi ambao wako tayari kujua makosa yao; kuyakiri na kutuhakikishia kuwa hawatarudia. Suala la Richmond hata lipambwe vipi linafungamana kabisa na ofisi ya waziri mkuu na Lowassa kama waziri mkuu alikuwa ni mtu sahihi kabisa kuwajibika. Lakini kwa vile amekataa kukiri makosa na kwa vile ameahidi kuwa hata tukimkurupusha leo, ataturudishia âRichmond yakeâ na kwa mtindo uleule, basi tunabakiwa na uchaguzi mmoja tu wa kiakili, uchaguzi ambao hauhitaji utaalamu mkubwa wa siasa na uongozi kuelewa â Lowassa hatufai.
Jaribio lake hili la kujisafisha kwa wale wanaonifuatilia niliandika 4 Julai 2010 katika mtandao wa JamiiForums. Nilisema, âNimemuota njozi siku ya mwisho ya mkutano wa Bunge, kwamba Lowassa amezungumza kwa undani sana na hatimaye aliamua kuzungumza kwa vipengele...â
Kwamba Lowassa angezungumza siku ya mwisho ya kikao cha Bunge. Sikumuona akifanya mahojiano na TV, lakini alikuwa katika ukumbi wa Bunge. Ndivyo ilivyotokea. Ninachofahamu sasa ni kuwa mstari umechorwa na ukuta wa ulinzi wa taifa letu umevunjwa. Lowassa kama aliyejeruhiwa ameamua kuja na mashambulizi mapya huku akijua kwamba sasa hakuna mahali pakimbilia.
Bunge limeshavunjwa na vyombo vingi vya habari ni dhaifu; vingi vimewekwa mfukoni na wenye fedha. Vichache vilivyosalia, vinatishwa na mawakala wake. Wakati wananchi walitakiwa kujadili hotuba ya Rais akiahirisha Bunge TBC (kwa baraka za Ikulu) wakaamua kurusha matangazo ya Lowassa na kuyarudia tena kesho yake.
Vyovyote vile ilivyo, tunaitwa na historia na dhamira zetu kupinga jitihada zote za Lowassa kutufanya taifa zima kuwa hatuna uwezo wa kuona mbali. Yawezekana ni mtu mzuri na kama nilivyosema, yumkini hakuwa fisadi katika suala la Richmond, lakini jinsi alivyolishughulikia na anavyolishughulikia sasa, kunabitisha tu hofu yangu kuwa hatufai kama kiongozi. Nilitamani sana nimsikie akikubali makosa yake kama kiongozi na kuacha kuilamu mbingu na dunia kwa kuangukia kwake, nasikitika hakufanya hivyo.
Hakuwataarifu mashabiki na wapenzi wake mimi nikiwamo, kutambua makosa na kujisahihisha, kwamba hana nafasi ya uongozi katika taifa zaidi ya ubunge anaoutaka. Kwa vile ameamua kusimama dhidi ya taifa letu, basi tunawaita âmahoka na mizimu ya waasisiâ waliolipigania taifa hili, akiwamo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wasimame dhidi yake na wale wanaomuunga mkono. Lengo ni kuja kutuonyesha sura halisi ya Lowassa.
Hata hivyo, Lowassa bado ana nafasi moja ya kujisafisha. Kukubali makosa yake ambayo yameligharimu taifa na kuomba radhi taifa hili. Nje ya hapo hawezi kusameheka
Chanzo: Mwanahalisi