Lowassa, kifo cha CHADEMA

Lowassa, kifo cha CHADEMA

Kifo cha chadema wamekitengeneza wenyewe kwa kuwa wameamua kukiuza chama chao kwa mafisadi wachache wenye uchu wa madaraka,nasikitika kuwa genge hilo limeishiwa na kuna dalili kuwa mgombea wao anataka kujitoa kabla ya oktoba 2015.
 
CHadema unayoisikia sasa hutaisikia tena ndio inakwenda kufa hv
 
Yaaan kushindwa kw lowasa October 25 chadema na vyama vingine vya ukawa ndo kushney
 
Nasikia baadaye wanaongeza list ya mafisadi na wastaafu....

Hahahahaaa
 
Kwa taarifa tu ni kwamba CHADEMA inajengwa zaidi na udhaifu wa CCM! Udhaifu wa CCM na kushindwa kutekeleza mambo ya msingi yanayowafanya watanzania waendelee kuwa masikini ndicho kinachoijenga CHADEMA. Sote tunalala gizani, sote tunakunywa maji ya tope, sote tunalala chini tukienda mahospitalini, sote tunasota na foleni Dar, sote tunaishi kwenye mitaa michafu yenye harufu kali ya uozo na makelele kila mahali. Tumekuwa kiishi hivi kwa miaka 50 iliyopita, na ninaweza kukuhakikishia kwamba kama CCM itachaguliwa tutaendelea kuishi katika hali hiyo. Si kwamba CCM haijafanya kitu, hapa ndipo mashabiki wa CCM wasipoelewa wanapokosolewa. Miaka 50 ni mingi sana katika kutatua matatizo ya msingi kama elimu, maji na afya. Kama asilimia zaidi ya 70 ya watanzania wanakunywa maji ya tope, kama asilimia zaidi ya 50 ya wanafunzi wanakaa mavumbini, kama asilimia zaidi ya 70 wanatumia vibatari kwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru, je bado tuseme CCM imefanikiwa? Watanzania TUAMKE kutoka usingizini!
 
Hatimaye ujio wa Lowassa umesababisha kuwe na kila dalili ya CHADEMA kupotea katika Ulimwengu wa siasa za Tanzania.

ACT wazalendo kinaweza kuwa chama kikuu cha Upinzani.

CHADEMA wamevurugana washapotea
 
Hatimaye ujio wa Lowassa umesababisha kuwe na kila dalili ya CHADEMA kupotea katika Ulimwengu wa siasa za Tanzania.

ACT wazalendo kinaweza kuwa chama kikuu cha Upinzani.
Kwa hiyo act haitafuti dora, inatafuta kua chama kikuu cha upinzani?
Huo uchaguzi wa kugombea chama kikuu cha upinzani unafanyika wapi?
 
Back
Top Bottom