Likiwa ni jimbo masikini mkoani Arusha chini ya ubunge wa lowassa kwa miaka zaidi ya 20 bado sijasikia cha maana alichoahidi mgombea urais wa Ukawa ndugu lowassa.
Inaonesha lowassa anapata wakati mgumu kuwashawishi wana Monduli kumchagua hali iliyomfanya kurudia kampeni mara mbili ndani ya kipindi cha majuma mawili katika jimbo hili.
Inaonesha pia lowassa amekasirishwa kuona binti wa aliyekuwa waziri mkuu mchapa kazi na aliyependwa katika jimbo hili Namelok Sokoine.
Kumekucha! CCM haina uwezo tena wa kupata ushindi kihalali kupitia sanduku la kura, CCM imepoteza kabisa tumaini la ushindi na imekata tamaa...lililobakia ni kupanga namna ya kubaki madarakani kwa namna yoyote ile na kwa gharama zozote zile. Pamoja na ukweli huu kuleta sintofahamu kubwa ndani ya jengo la Lumumba, patashika kubwa pia imeiandama CCM jinsi kila mipango inayofanyika kisiri inavyovuja na kuwafikia wapinzani wao.
Hali hii imekuwa mbaya hadi kuleta kutokuaminiana baina ya watu walioaminiwa na chama kupanga na kusimamia harakati za kampeni kumnadi mgombea wao John Pombe Magufuli. Imefikia wakati hata watu wawili wakikaa, kila moja anakuwa na wasi wasi na mwenzie na sasa haijulikani hali ikiendelea hivi mambo yatakuwaje mbele ya safari. Kutokuaminiana huku kumefanya wengi wakae kando baada ya wenzao kuanza kuwatuhumu wazi wazi bila kificho.
Wote tunakumbuka ile orodga ya watu 32 wa kumsaidia John Pombe Magufuli, jinsi ilivyosambaratika hata kabla ya kuanza kazi. Hali hii pia ilisababishwa na mgombea kuamua kujinadi mwenyewe kama vile ni mgombea binafsi na si mwakilishi wa chama chake cha CCM. Habari za ndani zinaeleza kuwa tuhuma zake kwa chama na viongozi wake kimewafanya wagombea wa nafasi mbali mbali wapate wakati mgumu kujitambulisha kama wagombea wa CCM.
Sababu nyingine ni ile ya wapambe wa Magufuli kutumia lugha za matusi kila wanapopanda jukwaani kitendo kinacholalamikiwa na wasikilizaji kwamba hakioneshi uungwana wala adabu. Mambo yote haya kwa ujumla wake yamefanya wananchi walio wengi kupoteza kabisa imani na CCM na hivyo kuamua kukitosa. Kwa hali ilivyo kama uchaguzi huru na wa haki ungefanyika hivi leo, ingekuwa bahati sana kwa CCM hii kuambulia hata asilimia 30% ya kura zote.
Habari za ndani zinasema CCM kwa kukata tamaa kabisa ya ushindi kihalali imeamua kutumia mamlaka ya dola kuhujumu uchaguzi mkuu ujao mwezi Oktoba. Kwenye hili tatizo linalowakabili ni kwamba hawana namna ya kuzuia mipango yao kuvuja...Wakikaa watatu, moja ama wawili watatoa siri, wakikaa watano, wawili au watatu watatoa siri na wakikaa kumi wanne au watano watatoa siri, wakikaa mume na mke mambo ni yale yale; kweli sikio la kufa halina dawa!