WATANZANIAWANATAKIWA KUMPUUZA EDWARD LOWASSA
Name:1429008174963.jpg Views: 0 Size: 63.1 KB
Nduguwanahabari, poleni na hongereni sana kwa kutimiza majukumu yenu mazuri ya kilasiku katika ujenzi wa nchi yetu.
Ndugu zangu nimewaita hapa ili kutoa maoniyangu kwa taifa nikiwa kama mwanachama hai wa UVCCM na CCM, pia kama raiamzalendo wa nchi yangu,
Napenda nichukue fursa hii kutoa wito wangukwa wanaCCM wenzangu na wananchi wote wa Tanzania, waliopo ndani na nje ya nchiyetu, wa kumpuuza ndg Edward Lowassa na timu yake kutokana na historia yakeisiyoridhisha na ukikwa ji wake wa taratibu za uchaguzi ndani ya chama chamapinduzi na hata tume ya taifa uchaguzi.
Hii ni Kutokana na hali ilivyo ndani ya nchiyetu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, yametokea mamboambayo kimsingi sio mazuri kwa mustakabali wa nchi yetu, ambayo kwa kiwangokikubwa yameanza kusababisha mgawanyiko baina yetu na hata kutishia upotevu waamani, umoja na mshikamano wetu kama watanzania.
Mambo haya yamekuwa yakifanywa sana na ndgEdward Lowassa ambaye kwa muda mrefu ameonyesha kuitafuta nafasi ya uraisi kwanguvu na hata kwa kuvunja taratibu za chama chake na nchi kwa ujumla, jambohili sio jema na nikiwa kama mwanachama wa muda mrefu wa chama cha mapinduzi,kiongozi na raia mwema wa nchi yangu, nimeona nichukue nafasi hii
Kama mzalendo ili niweze kuwakumbusha na kutoarai yangu kwa wananchi wenzaangu kwamba wawe makini na wasihadaike napropaganda zake bali wanahitajika kumpuuza ili kuweza kudumisha umoja wa nchiyetu.
Napenda kuwakumbusha wananchi wenzangu kwambawanapaswa kuikumbuka historia ya ndg Edward Lowassa vizuri na kwa kina sana,historia ya maisha yake na siasa zake kwa ujumla,
Mara nyingi amekuwa ni mtu anyetajwa kuhusikana ubadhirifu pia ufisadi mbalimbali unaofanyika ndani ya nchi, ukiwamorichmond ambapo mara zote amekuwa akiwaadaa wananchi kwamba alijiuzulu ilikulinda heshima ya serikali na chama chake jambo ambalo sio kweli, taarifa yatume ambayo iliundwa na bunge kufuatilia sakata hilo iliweka wazi namna wazirimkuu alivyohusika moja kwa moja katika ubadhirifu huo vikiwamo viambatanishovya vinote vyake, mawasiliano, na namna jinsi zoezi zima la ugaviulivyoendeshwa. Lakini pia amehusika na ufisadi katika ujenzi wa jengo laukumbi wa mikutano ya kimataifa AICC.
Lakini pia watanzania wanapaswa kufahamu nakukukmbuka namna jinsi alivyokuwa mtu mwenye kutumia vibaya madaraka yake,akiwa waziri mkuu alikuwa ni mtu mkorofi na mwenye maamuzi ya kukurupuka,alikuwa ni mtu mwenye kuwafukuza watu kazi kwa uonevu papo kwa papo bila hatakuwapa haki ya kuwasikiliza (right to be heared au natural justice)hasawanapokataa kulinda maslahi yake , aliwah kumdhalilisha na kutaka kumfukuza kazidc aliyekuwa ameteuliwa siku tatu tu na sasa ni mkuu wa mkoa, ndg mongela.
Ametumia madaraka yake vibaya kwakujilimbikizia mali mbalimbali ikiwamo umiliki wa ardhi mkubwa hasa jijini dares salaam kwa mfano eneo la peninsula pale masaki ambapo amejipatia viwanjakadhaa na ushahidi amejenga nyumba ya ubalozi wa south africa, AKiwa wazirimkuu alishiriki kuamuru uvunjaji wa ghorofa masaki kwa sababu linaziba nyumbayake kukosa upepo kutoka baharini, huku akidanganya umma kuwa ghorofa lilelimejengwa kinyume na utaratibu, amekuwa mtu mbadhirifu wa mali za umma sanakwa kutumia madaraka yake kwa mfano amejimilikisha majengo ya ppf na kumpamtoto wake.
Ni mtu msanii sana na si mkweli hasa kwautaratibu wake wa kukwakupua mipango ya serikali na kusema amefanya yeye,akiwaaminisha watu kwamba amekuwa anaisimamia ama kuanzisha yeye jambo ambalolimekuwa likifanywa na serikali kama timu, mara nyingi anazungumzia shule zakata ambazo zimeanza tokea enzi za mkapa wakati wa waziri ndg joseph mungai,pia amekwapua mradi wa maji ziwa victoria akisema ameanzisha yeye jambo ambalosio kweli kabisa, mradi ule ulisainiwa na ndg benjamini mkapa mwaka 2002 wakatihuo waziri wa maji akiwa ndg pius ng'wandu.
Ndg wanahabari nashangaa kuona mhe lowassaakijinasibu kwa hoja yake ambayo sio nzuri kwake lakini yeye amekuwaakiwadanganya wananchi kwamba ana maamuzi magumu, maamuzi yake hayakuwa magumubali ni ya kukurupuka na yasiyokuwa makini yaliyolenga kujikampenia uraisiambayo yamelitia taifa hasara sana, kwa mfano kuvunja mikataba kinyume chasheria ambayo baadae ameitia hasara serikali kwa kulipa fidia mfano mradi wamaji wa jiji (city water) amevunja majengo masaki ambayo hayo yote serikaliilibidi kutoa kodi za wananchi ili kulipa fidia amelitia hasara taifa, hayo nikwa ufupi tu lakini yapo mengi sana.
Kwa hakika wananchi wanapaswa kukumbuka kwambahii sio mara ya kwanza kwa ndg edward lowassa kugombea urais, aliwahi kufanyahivi mnamo mwaka 1995 lakini jina lake liliondolewa katika mchakato na baba wataifa mwl nyerere kutokana na rekodi zake za utumishi wa umma kujaa dosarinyingi na kupoteza uaminifu zikiwamo kujipatia utajiri mkubwa akiwa bado kijanasana huku vyanzo vyake vya utajiri vikiwa havijilukani na havifahamiki.
Wananchi wanapaswa kukumbuka kwamba ndg edwardlowassa amejidhihirisha wazi kuwa ni mtu mwenye tamaa kali ya mali na madaraka,wakumbuke ni wastani wa miaka ishirini sasa ndg Lowassa amekuwa akiutafutaurais wa nchi hii kwa tamaa zake binafsi, na mara zote amekuwa akiutumiautajiri wake na marafiki zake kufanya kampeni na kuyashawishi makundimbalimbali ya watanzania kumuunga mkono ili kufikia malengo yake binafsi,anatumia baadhi ya vyombo vya habari hasa vile vya habari coorperationvinavyosimamiwa na ndg Hussein Bashe kumsafisha na kumtangaza nchi nzima iliaweze kuonekana anakubalika, lakini pia amekuwa akitumia fedha alizoliibiataifa letu kufanya harambee mabalimbali hususani kwnye taasisi za kidini namakundi mengine ya kijamii, kuchapisha fulana, kununua watoa matamko nakuyatengeneza makundi mbalimbali yafike kwake kusema yanamshawishi nakumchangia achukue fomu za kugombea urais, kumbe ni uwongo na maigizoyaliyopitiliza kwakuwa makundi hayo na fedha anayaandaa yeye mwenyewe na rafikizake.
Na ndio maana mara nyingi yamekuwa yakipingwana mamlaka husika, kwa mfano ndani ya siku nne makundi yote yamekusanyika kwakehii inaonyesha ni nmna gani jambo hili lilivyotengenezwa kwa maigizo, kibayazaidi wanawadanganya wananchi kuwa kuna vijana wa bodaboda wametoka mbalalikuja kumshawishi dodoma, hivi ni kweli ndg wananchi inawaingia akilini kwambavijana wetu hawa waache kutafuta ridhiki ya kujikimu na kuwalipa vipande mabosiwao bali waweke mafuta na kutembea kilometa nyingi kuja dodoma, lakiniwalipitia njia gani kwa msafara mkubwa huo hadi usionekane hata na traffic.
sasa ni hatari kwetu wananchi kuachakuyaapuuza mambo kama haya ya mtu anayetafuta uraisi kwa uwongouwongo, uraisini jambo kubwa sana, imeshangaza sana kuona wachungaji kutoka mikoa mbalimbalina mabango yao ghafla wanakutana nyumbani kwa ndg lowassa, walijipanga mudagani, ni vigumu saana wachungaji kutoka sehemu tofauti wakawa na wazo mojakwenda kwa lowasa wakawa na wazo moja kuandika bango, harafu wakawa na wazomoja la kwenda tarehe moja na kwa pamoja wakakutana inaonyesha dhahiriwanawanadanganya wananchi na kuyatumia majina ya mashekh na wachungaji kwauwongo ili kupata madaraka,
nataka wananchi watambue namna ambavyo ndglowassa amekuwa anafanya utapeli wa kuungwa mkono huku akiyaita mafuriko kwambahawezi kuyazuia, ndg wananchi yale sio mafuriko bali ni mazingaombwe ama kiinimacho, yote anayafanya ili kufuta madhambi yake na aonekane ni mtu anayetakiwana kukubalika na wananchi. Napenda kuwakumbusha watanzania wenzangu kukumbukausia wa baba wa taifa alivyosema "muogopeni kama ukoma mtu anayetafutakwenda ikulu kwa kutumia fedha, hatufai" sasa tuziipuuze hizi propagandazake za hovyo ili kulisaidia taifa letu, hauwezi kusema nilikuwa mwizi na sasasiwezi kuibaa tena la hasha! wizi ni tabia na wahenga walisema tabia haina dawa.
Lakini pia ndg Edward Lowassa bado anatumikiaadhabu ya kifungo cha kutokujihusisha na maswala ya kampeni za urais , adhabuhiyo imetolewa na kamati kuu ya ccm baada ya kuanza kampeni kabla ya muda nampaka sasa adhabu hiyo bado haijaisha, wananchi wanapaswa kumpuuza nduguLowassa kwakuwa tayari mpaka sasa ameshakiuka masharti ya adhabu hiyo dhahirikwakuwa ameendelea na kampeni chafu ambazo umma umeshuhudia, sikukuu yachistmas iliyopita, ndg lowassa aligawa fedha kwa wajumbe wa nec na mkutano mkuunchi nzima, katika hali ya kushangaza ndg lowassa aliwagharamiaa vijana wa ccmwasiojitambua kwenda lituhi kijijini msibani kwa komba, aliwapa usafiri,malazi, posho na fulana walizozivaa msibani kama sehemu ya kampeni zake, ndgwatanzania wenzangu hili ni jambo la kusikitisha sana kwa mtu anayegeuza msibawa mpendwa wetu kuwa sehemu ya kampeni zake.
Hivi juzi amekuwa akifanya matendo ya kuigizaya kuandaa makundi mbalimbali aliyoyaita yanatekeleza agizo la mkt kwendakumshawishi, mkt alisema watu washawishiwe kwa kufuata utaratibu na sio kwauongo na uvunjaji wa kanuni, yale ni mazingaombwe kwakuwa makundi hayo ni fekina ameonyesha dharau kwa chama chake hivyo basi moja kwa moja atakuwa amepotezasifa za kuwa mgombea wa ccm. Lkn pia ndg lowassa amekiuka hata taratibu za tumeya taifa ya uchaguzi ambayo bado haijatangaza rasmi kuanza kwa uchaguzi, yeyeameanzisha movement inaitwa 4u ambayo inafanya kampeni kwa niaba yake nchinzima, hii si sawa na haitendi haki kwa wagombea wengine wenzake wanaofikiria kugombeawa ndani na nje ya chama chake , inapoteza usawa na haki ya kidemokrasia (fairpolitical grounds ) pesa anazotumia kufanya kampeni zake zinatengenezamazingira yasiyokuwa na usawa dhidi ya wagombea wenzie wasio na uwezo wakiuchumi, hivyo kulinyima taifa kupata kiongozi mwenye sifa stahiki. Wananchiwenzangu nawaomba msidanganyike na hizi sanaa za ndg lowassa kwamba anakubalikasio kweli, nchi hii ni kubwa sana na bado watanzania wengi tokea enzi zamwalimu nyerere mpaka sasa wanamjua kuwa ni kiongozi mbadhirifu na fisadi.
Lakini natoa wito kwa watanzania wampuuze ndglowassa kwakuwa hana mapenzi mema na taifa lake kwakuwa anajua fika swala latatizo la afya yake linalomkabiri lkn amekuwa akiwaadaa wananchi kwakutengeneza vipande vya picha kwa bandia ambavyo vinaonyesha akiwa anakimbiakwa kujivutavuta, kwa hali yake hatoweza kulitumika taifa hili lenye changamotonyingi na nzito, tunatakiwa kujifunza kwa mataifa mbalimbali yaliyopata kuwekaviongozi wenye matatizo ya kiafya jinsi walivyokabiriana na matatizo baadaezilivyowagharimu kisiasa na kiuchumi, kwa mfano Zambia rais Levy Mwanawasa naMichael Sata, Malawi rais Bingu wa Mutharika, na mataifa mengineyo pia, afya nijambo la msingi kwa kiongozi na si la kubezwa au kuangaliwa katika jicho kengeza.
Ndugu wanahabari mnalo jukumu la kuwakumbushawatanzania Lowasa ni Mwanasiasa na mfanya biashara Moja kati ya kosa kubwaambalo watanzania watalifanya na watalijutia maisha yao yote Ni kumpelekamfanya biashara huyu aliyepelekea kupangwa mpangwa wa ardhi Peninsula yaMsasani kwa faida yake, ikulu katika taifa ambalo linalasimali nyingi zinaitajikutengenezewa mpango mzuri na endelevu kwa manufaa ya Watanzania na siowachache wanaotamani ona zinawaneemesha wao tu .kumpa nchi mfanyabiashara mlafikama lowasa ni KUCHEZEA SHILINGI KATIKA TUNDU LA CHOO...
kuna kila sababu ya kumuita lowasa mwanasiasaasiyetosheka maana kwa muda aliotumikia taifa hili kwa zaidi ya miaka 30. Yapomaswali ya kujiuliza kwa nini hatosheki? Kuna kipya kipi ambacho hajakifanya miaka30 atakifanya ndani ya miaka mitano ya uraisi? Jibu linabaki moja tuu ni tamaaya madaraka na mali, ndio tafsiri yake. Mwalimu Julius Kambarage Nyererealiwahi hoji pale Ndg. Lowass alipojitokeza kugombea uraisi wa Nchi mwaka 1995.
Hata kufikia sehemu ya kupelekea Chamakuhengua jina lake katika Ugombea. Ni lini Ndg. Lowassa amejirekebisha katikatabia yake ya urafi na kujilimbikizia mali ? Ushauri wangu , BwanaLowasausigombee uongozi huu wa nchi hii iliyo na watu wema, wapenda maendeleo nawanaotamani kuona maendeleo iwe salama. Fedha ukizopeleka Uingereza na kuanzakufuatiliwa na Intelligensia ya Uingereza kazitolelee majibu. Nyumba zakifahari unazonunua hadi vyombo vya nje vinajiuliza unapata wapi fedha zotehizi unapswa kuvitolea majibu.
Baada ya kutoa wito huo kwa wananchi wakumpuuza ndg edward lowassa na kumchukulia kama ni mtu asiyejua analolifanya,napenda kuchukua fursa hii kumshauri ama kumuonya ndg Hussein Bashe mjumbewa,mkutano mkuu wa ccm na mtendaji mkuu wa kampuni ya habari corporation ambayeamejipa mamlaka ya kuwa msemaji wa ndg edward lowassa, kwa kutoa matamko dhidiya viongozi ambao wanatambulika kikatiba, ya kuwapinga na kutumia manenoyasiyofaa, hii inaonyesha utovu wa nidhamu alionao dhidi ya viongozi wake nachama kwa ujumla, kitendo cha ndg bashe kumshambulia katibu mwenezi wa ccm kwakutoa agizo ambalo muhusika amelitii, kimemdhalilisha sana, ameonyeshakukurupuka na kukosa adabu.
Mh. Nape ni Mwenezi wa Chama na kwambaanapozungumza juu ya masuala ya Chama lazima ajue kuwa huyu ni mtu mwenyemamlaka ya kusema katika Chama. Kama amekosea sio yeye wa kusema hayo.Utaratibu upo wa kwenda kupeleka malalamiko na kwamba Chama kitashughulikiakama kilivyoshughulikia malalamiko mengine.kitendo hiki kimenitia shaka juu yauwezo wa mtu mwenye nafasi aliyojitaja kuwa msemaji wa ndg Lowassa.
Shaka kubwa ni pale kauli zao zinapopishana naNdg. Lowassa juu ya kuwakusanya watu. Wakati Bwana Lowassa anadai hawaandaiwatu lakini ukweli nikwamba anajiongopea mwenyewe maana yule aliyejitambulishakama msemaje wake amethibitisha kuwa wanaandaa watu. Ushahidi wa wazi ni juu yakauli ya Nndg. Bashe kuwa wamekusanya saini za wajumbe zaidi ya 1700 wa MkutanoMkuu wa Ccm na kwamba wanajipanga kwenda kumshindikiza Bwana Lowassa juu yakuchukua fomu. Maswali mengi nimekosa majibu yake, yule mjumbe aliyepo kulemwambani Tanga alipataje hiyo karatasi na kusaini fomu ya kumuunga mkono kamasi kweli kwamba alipewa sababu za kusaini fomu hiyo?
Swali hata huyo aliyekwenda kumsainisha huyomjumbe, alifanyaje kama si kwamba kuna kikao kilitangulia ambacho kilipangamikakati ya kwenda kuwatafuta. Hapa nazungumzia wajumbe wote waliosemwa kusainikaratsi hiyo ambao wanatokea vijiji vya wilaya za Nchi nzima maana wajumne niwengi sana na kwa bahati mbaya hawaishi mtaa mmoja au nyumba moja. Na hata kamawangekuwa wanaishi pamoja basi wangelazimika kuitwa sehemu na kuambiwamadhumuni ya zoezi hilo. Ndg Waandishi hata ninyi niliwaita hamkujikuta mpondani ya eneo hili pasi kujua agenda mliyokuja ifuata.
Natambua pia ni uhuru wake kumuunga mkonoampendaye lkn asubiri muda sahihi wa kikatiba kuhusu maswala hayo, na baada yavikao kufanya uteuzi wa viongozi wasafi wanaofaa, watanzania wanapaswakuwapuuza watu kama hawa kwa maana mara nyingi wanakuwa wanakurupuka bila yakujijua, anastahili kuwa mtulivu aendelee kukua akijifunza siasa na asitumiwekwa manufaa ya wachache wasiothamini Watanzania tulio wengi.
Mwisho mshaurini Bwana Lowassa kuwa Usafi waKiongozi si kupiga picha na MheshimiwaRaisi, viongozi wa dini, maaskofu namasheikh au viongozi wakimila. Usafi wa kiongozi unaenda sanjari na historia yamaisha aliyoishi kiongozi huyo. Kama uliishi katika uongozi wako Ukiiba nakushindikiza maovu yafanyike kwa faida yake, basi jua wazi watanzaniasisitunayokumbuku nzuriya uovu ulioutenda. Hivyo usitamani kujifanya unapendasana na viongozi kwa kuwaandaa wapiga picha . Waombe radhi watanzania kwa yaleuliyowakosea.
Pia naipongeza kamati kuu ya ccm kwa kutoaadhabu za kikanuni na kuendelea kama siku zote kusimamia sheria, taratibu namiongozo yake katika kipindi hiki kigumu cha kuelekea uchaguzi mkuu, napendakumtia moyo mkt wa chama na wajumbe wote pamoja na wanaccm wote kwamba sisisote tupo pamoja nao, wafanye maamuzi ya haki kama sikuzote pasipo kumuhofiamtu yeyote, chama kisimamie kanuni, taratibu na miongozo yake ili kuwezakuwasaidia watanzania kama chama tawala kuweza kupata kiongozi bora.
Mwisho upo msemo usemo MAMBO HAYAENDI VIBAYAKWA SABABU WATU WABAYA WANAYAFANYA LA HASHA ILA NI KWA SABABU WATU WAZURI WAMEKAAKIMYA...Kwa niaba ya watu wazuri wote wanaoitakia mema nchii hii Nimeamuakuvunja ukimya dhiidi ya watu wabaya wanaotaka kulipeleka taifa hili sehemumbaya
Asanteni kwa,kunisikiliza
Nawatakia kazi njema.
Comrade kamati ya utekelezaji ya balazala UVCCM Na Mwenyekiti mstaafu washirikisho la ELimu ya juu la wanachama wa CCM Taifa
Last editedby Mwaka Mpya 2015; Today at 10:53.