Lowassa, jiwe litakaloitesa CCM 2020

I see your point! 2020 is just around the corner. Let's just wait and see.
 
Ni nani? Na amefanya nini? Mpaka hakuna kama yeye!

Bora ata ungesema hakuna kama Mwl. Nyerere kwa sababu alipigania kuupata uhuru toka kwa wakoloni hapa angalau ambao shule ipo kichwani watakuelewa


Mkuu sikuwa namlinganisha lowassa na Nyerere hiyo itakuwa kufuru
Ila huyu Pogba wa sasa haezi mfikia Lowasa
 
Ukichange gia angani Nyeusi inakua nyeupe. Mlizunguka Tanzania nzima kwa gharama zaidi ya mamilion ya shilingi mkimtangaza kua Fisadi
 
Hakuna kama lowassa
Hakuna kama Lowassa kimuonekano ila kiutendaji hakuna kama Magufuri Africa nzima nadhani wewe mwenyewe huu mziki unauona. Pia hapo wameyaacha yale mambo ya nyuma ya ufisadi kuhofia usalama wa nchi maanake kila ukigusa ufisadi si chama hiki wala kile kote wametapakaa sasa ukigusa unategemea amani itakuwepo.
 



Hakuna kweli alievurunda kama ngosha
Nashindwa ajiri hata walimu
Dawa hamna Hospitali hata panadol
Maji hamna kanunue ndege tetere aka pangaboi
Uchumi wa nchi hoi taabani
Wazungu wammnyima misaada
Democracy iko rehani
Viwanda&hoteli zimefungwa
Bandarini kumekauka mizigo
Hapo Giza tuuu kama hujui unakoenda huwezi kupotea..
Direction ya Zimbabwe na North Korea tunaelekea mpaka2017hadi mishahara watashindwa kulipa
 
E

Toka lini kazi za tume ni kuhukumu mkuu?
Tume yoyote inayoundwa na bunge kuchunguza jambo kisheria ina hadhi ya mahakama na tume ya maadili ya bunge pia ina hadhi ya mahakama isipokuwa haina jela tu kumbuka wabunge hupewa adhabu mbali mbali na tume hii na zinatimizwa kwa mujibu wa sheria. Nikirudi kwenye issue ya lowassa tume ilimkuta na hatia ya ufisadi ikampa adhabu yenye nafasi mbili ajiuzulu ama bunge limjadili na hatimaye lipige kura akachagua kujiuzulu kumbuka inaitwa adhabu kwa sab hakuamua bali alilazimishwa.
 
Dua la kuku hilo mizigo imeanza kurudi baada ya op maalum dawa zimeshafika na zinaanza kusambazwa na ajira idadi imeshatajwa na nafasi zinahitajiwa mwezi wa pili wanaajiriwa na sab ya kusitishwa ajira inajulikana ni uhakiki.
 
Hivi nini maana ya neno uchumi ukinifafanulia nitakuelewesha huyu mtu anachokifanya.
 
 
Hapo akipandishwa kizimbani pia mtasema nikwakuwa alihama ccm na kutimkia ukawa
 

Siamini kama Mhe. Lowassa alishindwa kwa kuwa alitajwa na CCM kuwa ni fisadi. Hata huyu aliyeshinda hakushinda kwa kuwa sio fisadi. Niseme tena; aliyeshinda hakuwa mgombea bora, ila alikuwa bora kwa wagombea waliojitokeza. Wewe uliisha kusikia tuhuma za ufisadi dhidi Rungwe,Dovutwa, Mama Mgwira,Prof. Lipumba, Marehemu Dr. Mvungi? Unadhani ni kwanini walishindwa? Mapungufu mabli mbali yakiunganishwa yanakuwa sababu za kushindwa kwa mtu. Vile vile sifa nzuri mbali mabli zikiunganishwa zinaweza kuchangia ushindi.

Mhe. Lowassa akisaidie chama (CHADEMA) kijiandae kwa ajili ya ushindi na asimamie ujenzi wa demokrasia ya kweli ili wakati ukifika apatikane mtu makini na bora katika kundi la watu bora na sio mgombea nafuu katika watu dhaifu. Heshima aliyonayo Mhe. Lowasa kwa watanzania ni kubwa sana, na ameipata bila ya kuwa Rais. Wapo watu ambao wanheshimika sana ndani na nje ya nchi zao bila ya kuwa rais. Nani atasema Mchuingaji Desmond Tutu sio mashuhuri eti kwa sababu hakuwahi kuwa rais Africa ya Kusini? Nani atasema Mhe. Rashid Mfaume Kawawa sio mtu wa kupigiwa mfano mwema kwa sababu hakuwa rais wa Tanzania? Mzee Warioba( jaji) hajawahi kuwa na inavyoonyesha hatakuwa, lakini nani asiye mkubali pamoja na kwamba alisimama kwenye jukwaa la CCM kuwanadi wagombea ubunge na rais wa chama cha mapinduzi. Mzee Mtei, ataendelea kuwa mhimili muhimu wa upinzani nchini na baba wa demokrasia ya kweli, heshima ya watanzania kwake ni kubwa na hajawahi kuwa rais wa Tanzania

Heshima ya Mheshimiwa Lowasa etaendelea asipogombe tena ila akichangia katika maandalizi ya akamwandaa mtu bora na makini kugombea urais kwa tiket ya chama chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…