Lowassa, jiwe litakaloitesa CCM 2020

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Hutaki acha,huu ndio ukweli wenyewe!!!!

Ukweli ni kwamba mpaka sasa Lowassa sio fisadi na wala hana ubadhirifu wowote.Aliitwa fisadi lakini mpaka leo pamoja na uwepo wa mahakama ya mafisadi hajawahi kuitwa,kukamatwa na kuhojiwa mahali popote, sio TAKUKURU wala POLISI na hana shitaka lolote mahakamani juu ya uhujumu uchumi,matumizi mabaya ya madaraka wala kujilimbikizia ukwasi.


Alitengenezewa Zengwe na mahasimu wake wa kisiasa,wakamuundia tume iliyokua imebeba maslahi ya watu wachache na wakafikia maamuzi ya kumbebesha mzigo usiomhusu wala siokua na uhalisia wowote! Aliundiwa ushadihi wenye mkanganyiko na ubabaishaji ambao hata leo ushahidi huo umetiwa kapuni na hukutumika mahali popote kumtia hatiani.


Zilikua ni propaganda chafu za kisiasa ambazo mpaka kufikia hivi sasa zimeshindwa vibaya sana, hakuna ukweli wowote kuonesha au hata kuhisia kua Lowassa ni "FISADI".


2020 atawaambia watanzania kua " Nilifadhaishwa sana,lilidhalilishwa sana,nilionewa sana kwakua tu tatizo lilikua ni uwaziri mkuu" Watanzania amueni wenyewe na kisha toeni hukumu wenyewe.Kwahiyo kwa mwenye uelewa atakua amenielewa.


Mahitaji ya Mh Lowassa ni makubwa sana hivi sasa kwa wananchi, wanamhitaji kuliko hata ilivyokua awali na kama haki itatendeka kwenye uchaguzi mkuu 2020 endapo akisimamishwa na chama chake sidhani kama kuna mtu wa kushindana nae. In short ni kwamba Lowassa hana mshindani kwenye sasa za nchi hii endapo vyombo vya dola pamoja na wa tawala wakaacha taratibu na sheria zikatumika badala ya maekekezo.


Angalizo

Ni lazima kuwe na tume huru ya uchaguzi, haijalishi chama tawala hakipendi kulisikia hili lakini kwa namna yeyote ile ni lazima kuwe na mabadiliko kwenye tume ya taifa ya Uchaguzi.
 
Kwani refa atakae simamia huo mtinange ameshateuliwa?? Na kama ameteuliwa, ameteuliwa na timu moja
au timu zote zimemkubali
 
Baadhi yetu tuepukane kushikiwa akili, unajua walosema ED ni fisadi wanajulikana tena walitangaza hadharani na walizunguka Tz nzima wakitangaza ufisadi wa huyo bwana, na walisema ushahidi wanao wa kutosha kuhusu ufisadi wake, na wakamtaka ED aende mahakamani na ED pia hakwenda, baada ya ED kuhamia palipokuwa na ushahidi wa kutosha, palepale ushahidi ukayeyuka-ulitakiwa uwabane kwa nguvu walotangazia uma kuwa ushahidi upo tena wa kutosha. Au kwa kuwa2 tumezea kulalamika?
 
Wasiojua ni kuwa Lowassa kama PM mstaafu alikula kiapo cha utii ... Wengi wamemsingizia mambo chungu nzima, lakini hakuna hata mmoja aliethubutu kum-face au kumpeleka mahakamani... Kutokana na Ukimya wake, wengi wamejenga hofu nyingi juu yake kuwa atakuja kuwachinja ... watafanya kila aina ya vitimbwi kuhakikisha kuwa hapewi nafasi ... Wanasahau kuwa yeye pia ana mtandao wenye nguvu zaidi ndani na nje ya nchi ... Only time will tell ...
 
Wewe na Lowasa wako unakera sasa, kila siku, au ndiyo kazi aliyokutuma? Mgombea mwenyewe wa Chadema bado hajapatikana kupitia mchakato wa kidemokrasia.
 
Sijui kwann Mungu ametupitisha kwenye hili balaa.lowassa ataendelea kuwa masikioni mwa watanzania milele.namimi niwape tu angalizo tukipata tume huru ya uchaguzi kabla ya ibada ya kwanza kutoka sikuhiyo tumeshaitenganisha ccm na jeshi la polisi
 
Siasa, siasa, siasa, siasa. Ni miezi kadhaa tu tangu Lowasa ameshindwa kwenye urais, lakini andiko lako linaonesha kana kwamba watanzania ambao kwa wingi wao hawakumpa kura miezi kadhaa iliyopita eti leo tunaaminishwa wanamhitaji. Ndugu yangu inawezekana Lowasa hajawahi kufisadi chochote kwa yeyote, lakini hicho pekee hakiwezi kuwa ndiyo free ticket ya Lowasa kuchaguliwa. Lakini pia kwani Lowasa hata akiwa msafi, mwenye busara na hekima, pia mchapa kazi kuliko wa Tz wote ndiyo iweje? Kwani yeye kazi pekee hapa Tz inayomfaa ni kuwa rais tu basi.
 
Lazima awahenyeshe, mlimchafua wenyewe sasa mumsafishe wenyewe!!
 
Ndio ni Lowassa tu, amini usiamini.
 
Wewe na Lowasa wako unakera sasa, kila siku, au ndiyo kazi aliyokutuma? Mgombea mwenyewe wa Chadema bado hajapatikana kupitia mchakato wa kidemokrasia.
Tulia dawa ikuingie mkuu, utampenda tu.
 
Hata huelewi ni kwanini unaandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…