OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 437
Katika maisha ni rahisi sana kumrubuni mtu masikini kwa sababu utatumia njaa na shida zake kumrubuni na kumfanya afanye lolote unalotaka. Saikolojia inasema; uwezo wa mtu kufikiri na kufanya maamuzi sahihi unapunguwa pale mtu anapokuwa na matatizo. Kwa mfano; mtu mwenye njaa anaweza akarubunika kufanya kitu chochote ili apate chakula.
Ni rahisi sana kumrubuni mtu asiye na elimu kwa sababu utatumia upeo wake mdogo kumrubuni na kumfanya afanye chochote unachotaka. Upeo wa binadamu kufanya maamuzi sahihi unaongezeka kadiri binadamu anavyopata elimu.
Ni vigumu sana (mara nyingi haiwezekani) kumrubuni mtu tajiri mwenye elimu. Hii ni kwa sababu mtu aliyeshiba na mwenye elimu siku zote anatumia akili yake na siyo tumbo au akili ya mtu kwenye kufanya maamuzi.
Toka atangaze nia, tumeshuhudia Lowassa akiungwa mkono na makundi ya wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee, wasomi na wasio wasomi, masikini kwa matajiri.
Najiuliza maswali yafuatayo;-
1. Maelfu ya Watanzania wanaomuunga mkono Lowassa wana njaa kiasi cha kurubuniwa? Kama ni njaa, Lowassa kawapa nini kuwarubuni?
2. Maelfu ya Watanzania wanaomuunga mkono Lowassa hawana upeo (elimu) mpaka wafikie kurubuniwa kumuunga mkono Lowassa pasipo utashi wao?
3. Maelfu ya wasomi (wakiwemo Maprofesa) wanao muunga mkono Lowassa wamepewa nini kurubuniwa kumuunga mkono Lowassa?
4. Maelfu ya Matajiri wanao muunga mkono Lowassa wamepewa nini?
5. Maelfu ya wasomi-matajiri wanao muunga mkono Lowassa wamepewa nini kurubuniwa kumuunga mkono Lowassa?
Ukijiuliza kwa makini maswali hayo hapo juu utagunduwa kuwa huwezi kuwarubuni maelfu ya watu wakati wote. Hivyo kwa kuungwa mkono na makundi ya wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee, wasomi na wasio wasomi, masikini kwa matajiri, Lowassa ndiye mtia nia pekee mwenye wafuasi wengi ndani na nje ya CCM.
Binafsi ni muumini wa demokrasia ya kweli. Na msingi mkubwa wa demokrasia ni kuheshimu maoni ya wengi. Kwa mapenzi yangu kwa CCM na taifa la Tanzania, naandika haya kuwaasa wajumbe wa vikao vya maamuzi (Baraza la Wazee, CC, NEC mpaka Mkutano Mkuu) wapitishe jina la Lowassa kuipeperusha bendera ya CCM uchaguzi mkuu 2015.