Lowassa hawezi kuwa mpinzani mzuri

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,981
45,903
Kichwa cha uzi huu kinatokana na msemo maarufu ambao jamaa zetu wa kiingereza hupenda kuutumia pale wanapotaka kueleza jambo linaloshahabiana na hili ninalotaka kulileta kwenu, msemu huo ni kama ufuatavyo " You can not teach an old dog new tricks" kwamba " Huwezi mfundisha mnyama mzee mbinu mpya za kuishi" ( Tafsiri nimeidarizi ilikupunguza ukali wa maneno).

Nimevutiwa kuzungumza haya kufuatia kauli ya mwanasiasa huyu alipokua Monduli wakati akieleza mikakati yake ya kufanya ziara ya kuwashukuru wananchi pamoja na kukijenga chama.

Kauli hiyo inatoa picha ya kutaka kuonesha mabadiliko ya kifikra ya Mheshimiwa huyu, jambo ambalo kwa wafuatiliaji wa siasa za dunia na nchini kwa ujumla wataona kama ni hadaa tu.

Ikumbukwe kwamba Bw. Lowassa amekua na kupanda katika ranks mbali mbali za kiuongozi katika chama na serikali, maisha yake yote amekua katika upande wa utawala, mind set na hata malengo yake yamekaa kiutawala zaidi kuliko kiuanaharakati.

Kila mtu ni shahidi kua, kutoka kwake CCM kulifuatia baada ya yeye kudai kutotendewa haki na kamati kuu ya CCM wakati akigombea nafasi ya kuwa mwakilishi wa CCM. Hivyo inamaana kama angepata nafasi hiyo asingelihama CCM. Na ipo wazi kua alihamia Chama cha CHADEMA ili kutimiza malengo yake ambayo aliyapa jina la "Safari",Ukitazama kwa ukaribu sana utaona kwamba hiyo safari sio yetu bali ni yake binafsi.

Kwahiyo utaona kwamba kila analolifanya mheshimiwa lipo katika lengo lake kuu la kushika madaraka, na sio kutukomboa sisi maana hakuwahi kuishi maisha ya uanaharakati katika kipindi chote alichowahi kua kiongozi.

Lowassa hakuwahi kushiriki harakati zozote za ukombozi ambazo zilikwenda kinyume na watawala, hakuwahi kuibua hoja wala kuonesha mfano wa kupinga watawala isipokua kua sehemu ya watawala.

Zaidi sana malengo ya safari yake ni kujikuza kisiasa, kwa kua ameshasahaulika kutokana na yale mema ambayo serikali ya CCM aliyokua sehemu yake inayafanya sasa kupitia Magufuli.

Lowassa hawezi kufikiri wala kutenda kinyume na CCM. Lowasa ni CCM na atabaki maisha yote kua CCM maana amekua ccm na hana matendo wala mawazo tofauti na CCM.

Ukitaka kupata ukweli wa hili, jiulize ni jambo gani jipya sana ambalo amelifanya kuonesha kua yeye ni mtu mpya? Jiulize na hili pia je ni rahisi kwa mvuvi mzee kujifunza mbinu mpya za kuvua? Au kwa mwindaji mzee kujifunza mbinu mpya za kuwinda? Sidhani ndio maana nasema lowasa kachelewa sana katika safari yake ya kuwa mpinzani mzuri, ndio maana hata sisi waswahili tukaja na neno letu kua " Samaki mkunje angali mbichi".
 
Siku zote Lowasa ni mtu wa kupoteza tu. hata huko upinzani soon watamtema
 
Angekuwa siyo mpinzani mzuri mngetumia majeshi yoooote ya ulinzi na usalama na NEC kumkabili?Nyie mko hapo kwa mabavu ya dola tu.
 
Lowassa alisababisha watu kuagiza magari 777 ya kuwasha na kama aitoshi watu wakaamua kupiga pushapu na hata juzi kwenye kikao cha "ulevini" mzee wa msoga kamtaja edo! sasa kwa mtindo huu edo atawasumbua sana hapo "ulevini" lumumba
 
Back
Top Bottom