singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,538
Lowassa hasafishiki
Na Mwandishi wetu - Imechapwa 06 April 2011
JUHUDI za waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kujisafisha mbele ya jamii, zimegonga mwamba baada ya kubainika kuwa ni serikali iliyoingiza kampuni ya Richmond katika mkataba wa kufua umeme.
Wakati huo, maelekezo yote kuhusiana na utoaji mkataba kwa Richmond yalikuwa yakifanyika chini ya Lowassa, kwa mujibu wa waziri wa nishati wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha.
Ilibainika katika kikao baina ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali na makatibu wakuu wa Fedha na Nishati, kwamba TANESCO ililazimishwa na serikali kuingia mkataba na kampuni ya kitapeli ya Richmond.
Taarifa zimeeleza kuwa serikali ilitupilia mbali sheria zote za manunuzi na mikataba ili "kulazimisha na kulinda Richmond kupewa zabuni."
Kamati teule ya bunge, katika uchunguzi wake wa kashfa hii, pamoja na kutaja wahusika wote na kutaka wawajibishwe, ilimwacha waziri mkuu "kuchukua uamuzi" anaoona unafaa. Lowassa alijiuluzu.
Taarifa zinaonyesha serikali iliingia mchakato wa kupata mzabuni, hata baada ya TANESCO kuona kuwa hakukuwepo mshindi kwa mujibu wa zabuni.
Kinyume na maoni ya TANESCO, wizara ya nishati, baada ya kupitia maombi ya zabuni, iliamuru bodi kukubali kuwa Richmond ndiye mshindi na Juni 19, 2009 wizara ikaagiza TANESCO kusaini mkataba na Richmond.
Katika uchunguzi wa bunge, ilibainika kuwa Richmond haikuwa na fedha, uwezo wa kiufundi, vitendea kazi wala uzoefu katika miradi kama hii.
Mkataba wa Richmond ulirithiwa na kampuni ya Dowans Holdings SA ya Costa Rica na Dowans Tanzania Limited (DTL).
Kwa mujibu wa Ibara ya 68 ya sheria ya manunuzi ya mwaka 2004, jukumu la kuamua mshindi wa zabuni ni la bodi ya zabuni ya shirika (TANESCO).
Kwa msingi huo, kamati iliyoteuliwa na serikali kushughulikia mkataba na zabuni, haikuwa na mamlaka ya kisheria ya kufanya uamuzi kuhusu zabuni.
Hiki ndicho chanzo cha kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma kufikia hitimisho wiki iliyopita kwamba ni serikali inayopaswa kubeba mzigo kwa vile TANESCO ilikuwa ikiamriwa tu.
Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara (ICC) iliamua katika kesi ya madai, Novemba mwaka jama, kuwa TANESCO ilipe Dowans na Richmond dola 62.4 milioni (sawa na Sh. 94 bilioni) kwa kuvunja mkataba wake.
Tayari Dowans wamesajili uamuzi wa ICC mahakama kuu kama utaraibu wa kulipwa unayotakiwa.
Hata hivyo, TANESCO inapinga tozo hiyo. Katika utetezi wake, shirika hilo la umeme, pamoja na hoja nyingine, inawasilisha pia kuwa ililazimishwa na serikali kuingia katika mkataba.
Wachunguzi wa mambo ya utawala bora wanasema Lowassa, ambaye aliwahi kukiri kuwa alikuwa karibu sana na mchakato wa kupata mfua umeme, hawezi kujinasua katika kashfa hii.
"Hilo siyo swali, hata wewe unaona na Lowassa mwenye aliliona ndiyo maana aliamua kujiuzulu kabla hajafukuzwa au kabla bunge halijataka achukuliwe hatua," ameeleza kiongozi mmoja wa asasi ya kijamii inayofundisha masual ya utawala bora.
chanzo Mwanahalisi