VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Ukweli mchungu. Binafsi namchukia Edward Lowassa. Nilifarijika alipohamia upinzani-CHADEMA. Kwangu mimi,nilidhani kuhama kwa Lowassa kungekipa nafasi chama chetu cha CCM kujisafisha na kusonga mbele. Mimi,kwakuwa hakuna uwazi wa ukwasi wake,namchukulia Lowassa kama asiye msafi.
Lakini,Lowassa hakwepeki. Bado anairun CCM. Ni kupitia marafiki na wafuasi wake chamani ambao sasa ni mihimili. Kwasasa,nitatoa mifano miwili. Wa kwanza ni Andrew Chenge. Chenge ni moja wa mapacha watatu waliosemwa kuwa wangetimuliwa CCM. Wengine ni Lowassa na Rostam Aziz. Zoezi ĺa kuvua gamba likakwama.
Chenge na Lowassa ni marafiki wa ngazi ya ndugu wa damu kisiasa. Chenge amepitishwa na kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Mwenyekiti wa Bunge. CCM inamwamini Chenge. Kumwamini Chenge ni kumwamini Lowassa. Chenge na Lowassa ni chanda na pete. Ndiyo kusema,Lowassa analiongoza Bunge kama Mwenyekiti kupitia kwa Chenge.
Kwa Wabunge,yupo Hussein Bashe wa Nzega Mjini. Wabunge wote wa CCM wanamwamini Bashe kama jembe ndani ya chama kwasasa. Anapozungumza hushangiliwa na kusikilizwa kwa makini. Bashe na Lowassa ni baba na mwana. Ndiyo kusema,Lowassa ametutengenezea jembe CCM. Bashe hajawahi wala hatawahi kumuacha mkono Lowassa.
Lowassa is unavoidable politician,he still runs the ruling party from outside. Mwenye masikio na asikie,mwenye macho na aone!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Pemba)