Jina la muvi ni CCM kumekucha

Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,200
5,553
JINA LA MOVIE NI CCM KUMEKUCHA!

WAHUSIKA wakuu wa movie hii ni Lowassa na Kikwete. Marafiki walioingia madarakani kisha wakagombana. Kikwete Rais, Lowassa waziri mkuu. Lowassa akataka Urais baada ya Kikwete, ooh, Kikwete akambana mbavu.

Katikati ya mapambano ya Kikwete na Lowassa, akaibuka Magufuli. Kikwete akasema bora Magufuli kuliko Lowassa. Naam, Magufuli akawa Rais na Mwenyekiti CCM.

Magufuli baada ya kushinda Urais na uenyekiti CCM, anaunda mfumo wake. Wa Lowassa wanalia, wa Kikwete wananung'unika. Sophia Simba, Kimbisa, Nchimbi waliomuunga mkono Lowassa, mapema walikula vitofa vya kichwa! Bashe, mtoto pendwa wa Lowassa akalia bungeni kuwa alitekwa na Usalama wa Taifa.

Nape, yule mtoto pendwa wa Kikwete akatimuliwa uwaziri baada ya mwaka mmoja na nusu! Usajili wa kihistoria ukafanyika, wanabebwa wapinzani kuwa wabunge na madiwani CCM, wanaCCM asilia wanaambiwa vyeo hivyo haviwahusu!

Ukaibuka mzinga wa nyuki, unaitwa Musiba! Unang'ata watu wa Lowassa na wapinzani. Mzinga wa nyuki ukageukia watu wa Kikwete. Wakaambiwa wanamhujumu Magufuli. Wakatulia, wakajua Magufuli atawatetea! Eeh, wanashangaa kimya. Membe, swahiba wa Kikwete, anamwaga 'mchozi' eti wamemkata mkia!

Makatibu wakuu wastaafu CCM, Kinana na Makamba ambao walifanya kazi na Kikwete, wanalalamika hadharani kuwa wanashambuliwa lakini hawatetewi. Wanasema mzinga wa nyuki (Musiba), unafugwa na wenye mamlaka makubwa. Otea ni nani!

Bashe, yule Kijana wa Lowassa, aliyelia bungeni kuwa alitekwa, baada ya Lowassa kujiunga na timu ya Magu, anawashambulia Kinana na Makamba. Anasema wanataka kumkwamisha Magufuli asiwe Rais 2020. Wakati huohuo, ni giza tupu kuhusu uhusika wa Rostam!

Nape na Kinana wanamteta Magu kwa simu kishkaji, wanarekodiwa, sauti zao zinavujishwa. Hii inaonesha CCM hakuna kuaminiana. Kumbe kuna wanaofuatiliwa kila mawasiliano wanayofanya. Hofu imetanda! Ni kasilibano, alisema Lufufu! Ndani ya CCM ni political violence! Jina la movie ni CCM Kumekucha.

Nakuacha na wimbo huu mtamu. Tuimbe wote; Tunatoana roho Yarabi, kwa chama alichoacha Nyerere. Tunatoana roho Yarabi, kwa chama alichoacha Nyerere!

Ndimi Luqman MALOTO
 
“War can only be abolished through war, and in order to get rid of the gun it is necessary to take up the gun.”
― Mao Zedong
 
Week ijayo tutaanza kubatiza baadhi ya watu kwa moto😁😁
download.jpeg
 
Ujue ikifikia stage baba na mama wanapigana, mpaka watoto wanajua, hapo kuna mvunjiko wa ndoa unakuja.

Baba na mama zamani walikuwa wanapeana mapigo ya wakubwa chumbani kwao. Wakitoka chumbani wanacheka na watoto tu.

Watoto hawajui mama kapigwa kibao, baba kararuriwa kucha.

Siku hizi zinapigwa ukumbini mpaka watoto wanaona hapa hatuna wazazi wenye akili.
 
Back
Top Bottom