Lowassa had his chance. CHADEMA itafute mgombea kijana mwenye mvuto 2020/25

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
32,998
60,486
..najua hii itakuwa ngumu kumeza, lakini kwenye ukweli lazima usemwe.

..OK, Lowassa amewezesha kuchaguliwa wabunge wengi wa CDM kupita wakati wowote.

..lakini hilo lisitufumbe macho kwani lengo letu lilikuwa kuingia IKULU na kukamata BUNGE.

..sasa hivi CDM haiko Ikulu na bungeni tuko wachache bado CCM wanaweza kufanya wanavyotaka.

..wakati umefika tuangalie mbele uchaguzi wa mwaka 2020 na 2025. bila shaka mtaona kwamba Lowassa ha-fit katika mahesabu hayo.

..wakati umefika kwa CDM kuwekeza ktk viongozi VIJANA ambao wataweza kushindana na Magufuli 2020, na ikishindikana watakuwepo 2025.

..lazima CDM ianze sasa hivi kuwekeza kwenye viongozi ambao wanakubalika KITAIFA. watafutwe watu wenye MVUTO, KIPAJI, ANAYEAMINIKA, na ANAYECHAGULIKA.

..Elimu yake isiwe ya mashaka-mashaka. Pia asiwe na mawaa ya kimaadili.

..watafutwe wagombea ambao CCM itashindwa kuwabomoa na kuwapaka matope wakati wa uchaguzi.

..pia CDM itakuwa inakosea kuwekeza kwenye mtu mmoja kama tulivyofanya kwa Dr.W.Slaa.

..Lowassa na Sumaye kwangu mimi hawa-fit description ya potential candidate atakayeweza kupambana na Magufuli in 2020, au kupambana na mrithi wake in 2025.

..Pia CDM lazima iwe na mkakati zaidi ya mmoja, na siyo kuwekeza karata zote kuingia ikulu. Iangalie uwezekana wa kuwa na majority bungeni, kama daraja la kuingia ikulu.

cc Nguruvi3, Pasco, The Boss, Ben Saanane, zumbemkuu, Chakaza
 
Kuna mbunge wa CHADEMA Joseph Silinde i guess
nilitamani apewe nafasi za kitaifa tuone uzoefu wake
labda akipata watu sahihi wa kum groom atafika mbali.....

..wanatakiwa wawape exposure wabunge vijana.

..CDM inatakiwa ijifunze kutokana na makosa iliyofanya uchaguzi uliopita.

..mgombea Uraisi lazima awe mtu anayeweza kulitawala jukwaa na kushawishi wapiga kura.
 
Lowassa keshawadhibiti
kitendo cha yeye kutangaza kugombea tena mwaka 2020
kinafanya zoezi la kuwaandaa wengine liwe gumu..
ni kama hiyo nafasi ina mwenyewe
 
Lowassa keshawadhibiti
kitendo cha yeye kutangaza kugombea tena mwaka 2020
kinafanya zoezi la kuwaandaa wengine liwe gumu..
ni kama hiyo nafasi ina mwenyewe

..but Lowassa has too much baggage.

..pia uwezo wake wa kupiga kampeni ni mdogo.

..Lowassa labda angekuwa mgombea mzuri kwa ccm, lakini cdm inahitaji mgombea tofauti.

NB:

..kum-circumvent Lowassa, CDM waseme wanaandaa wagombea wengine incase he[lowassa] can not run.
 
Mie naona majina aya 3 yanafaa yapewe nafasi ya kuwekeza kupitia kwao

Heche
Mnyika
Wenje
 
l
Lowassa keshawadhibiti
kitendo cha yeye kutangaza kugombea tena mwaka 2020
kinafanya zoezi la kuwaandaa wengine liwe gumu..
ni kama hiyo nafasi ina mwenyewe
labda wamrudishie hela yake na riba. hata hivyo kama akikubali maana inadaiwa mbowe alishamuuzia chama.
 
CHADEMA na wapinzani wengine wakikubali kushiriki uchaguzi mkuu ujao chini ya tume ya uchaguzi iliyo na muundo kama hii iliyopo sasa nitawaona majuha wa kutupwa.
usianze kuleta visingizio kuhusu tume kana kwamba uchaguzi uliopita wapinzani walishindwa kwa sababu ya tume. kudhani hivyo ni ujuha tena uliokithiri. lazima wapinzani wakubali kuwa kosa kubwa walilofanya ni kubali gia angani. na wapinzani wakirudia kosa hilo tena 2020, kipigo kiko palepale. na dalili zote zinaonyesha kosa lile lile kurudiwa.
 
Mkuu hata wakibadilisha katiba sidhani kama ccm wanaweza shindwa kwa kura za makaratasi kwan husikiagi matamshi ya viongozi wao...????
 
..but Lowassa has too much baggage.

..pia uwezo wake wa kupiga kampeni ni mdogo.

..Lowassa labda angekuwa mgombea mzuri kwa ccm, lakini cdm inahitaji mgombea tofauti.

NB:

..kum-circumvent Lowassa, CDM waseme wanaandaa wagombea wengine incase he[lowassa] can not run.
CDM wanaweza kutumia lowasa ku divert attention ya CCM hivyo kuwapa nafasi kujenga mtu
 
..najua hii itakuwa ngumu kumeza, lakini kwenye ukweli lazima usemwe.

..OK, Lowassa amewezesha kuchaguliwa wabunge wengi wa CDM kupita wakati wowote.

..lakini hilo lisitufumbe macho kwani lengo letu lilikuwa kuingia IKULU na kukamata BUNGE.

..sasa hivi CDM haiko Ikulu na bungeni tuko wachache bado CCM wanaweza kufanya wanavyotaka.

..wakati umefika tuangalie mbele uchaguzi wa mwaka 2020 na 2025. bila shaka mtaona kwamba Lowassa ha-fit katika mahesabu hayo.

..wakati umefika kwa CDM kuwekeza ktk viongozi VIJANA ambao wataweza kushindana na Magufuli 2020, na ikishindikana watakuwepo 2025.

..lazima CDM ianze sasa hivi kuwekeza kwenye viongozi ambao wanakubalika KITAIFA. watafutwe watu wenye MVUTO, KIPAJI, ANAYEAMINIKA, na ANAYECHAGULIKA.

..Elimu yake isiwe ya mashaka-mashaka. Pia asiwe na mawaa ya kimaadili.

..watafutwe wagombea ambao CCM itashindwa kuwabomoa na kuwapaka matope wakati wa uchaguzi.

..pia CDM itakuwa inakosea kuwekeza kwenye mtu mmoja kama tulivyofanya kwa Dr.W.Slaa.

..Lowassa na Sumaye kwangu mimi hawa-fit description ya potential candidate atakayeweza kupambana na Magufuli in 2020, au kupambana na mrithi wake in 2025.

..Pia CDM lazima iwe na mkakati zaidi ya mmoja, na siyo kuwekeza karata zote kuingia ikulu. Iangalie uwezekana wa kuwa na majority bungeni, kama daraja la kuingia ikulu.

cc Nguruvi3, Pasco, The Boss, Ben Saanane, zumbemkuu, Chakaza
Jokakuu. Hata kama Chadema wataweza kumshawishi Magufuli ahamie kwao kushinda uchaguzi kwa mazingira ya huu mfumo na tume ni HAKUNA. Suala la Zanzibar lifumbue macho wale waliokuwa wana-doubt na mfumo wetu wa uchaguzi kuibeba CCM. Kwa maana nyingine ni kuwa hata huu uchaguzi uliopita Lowassa angegombea kwa tiketi ya CCM na Magufuli kwa Chadema... Lowassa angeshinda kwa kishindo kuliko Magufuli alivyoshinda!
 
sijajua why Vincent Nyerere amekataliwa

Acha utani mkuu
Vincent Nyerere kila alichoahidi hakukitekeleza
mbaya zaidi hadi open spaces yeye na madiwani wenzie wa CHADEMA walituhumiwa kujiuzia
wananchi walimrudisha Mnyinyi kwa hasira na kuona wametapeliwa....
 
Sidhani kama Lowassa alimaanisha alichokisema kuhusu kugombea urais 2020. Maana uchaguzi uliopita wote tumeona afya mbovu ya mzee, siasa za majukwaani haziwezi, kunadi Ilani ya chama ilikuwa shida, ni mtu ambaye si myenyekevu kwa wapiga kura (rejea majibu yake na sakata la Richmomd) wakati wa kuomba kura anajiamini sana mpaka mtu haoni umuhimu wa kumpa kura maana anafahamu hata hasipompa kura atashinda tu.
Uzuri wake ni mzee wa mikakati..

Nafikiri kisa cha Chadema kumchukua Lowassa kuwa mgombea wao ilikuwa ni kama wangekataa basi Lowassa alikuwa anakwenda ACt wazalendo na kama angefanya hivyo basi uwezekano wa ACt kuwa chama kikuu cha upinzani ulikuwa mkubwa..Maana Dar ingekwenda kwa Act na CCM, kanda ya kaskazin kura za wabunge wangegawanywa na mfaidika angeksuwa CCM, kanda ya ziwa Magufuli alikuwa ameisha iteka.. hivyo basi utaona kuwa Chadema/Ukawa walikuwa hawana namna zaidi ya kukubali japo kwa shingo upande kumchukua LOWASSA, kitu ambacho mwaka 2020 huu msukumo hautakuwepo hivyo Lowassa hana nafasi kabisa ya kugombea kiti chas urais..

Nyani Ngabu umeongea jambo ambalo miaka yote tumekuwa tukilipigia kelele lakini cha ajabu wadhirika wa jambo ili wamekuwa kimya kwa miaka 20 as if hawaoni au kuelewa kinachoendelea wakati mwingine huwa nafikiri kuna siri kubwa katika jambo ili na wanufaika ni wagombea urais/ubunge
e
 
Back
Top Bottom