Lowassa fanya mbwembwe na Mameya wako wa Ilala na Kinondoni lakini usituibie tena

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Katika Kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikaeli Mbowe aliibuka na kusema na hapa nanukuu:

"WAPO WAFANYABIASHARA WAKUBWA WATANO AMBAO WANGEWEZA KUGHARAMIA KAMPENI ZA CHADEMA, LAKINI WANAOGOPA MAJINA YAO KUTAJWA KWA KUHOFIA KUFUATILIWA NA VYOMBO VYA DOLA.

Mara tu baada ya Uchaguzi kumalizika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli(TINGATINGA) kuanza KUTUMBUA MAJIPU kama alivyoahidi Bungeni Dodoma, aliyekuwa Mgombea Urais kwa Tiketi ya CHADEMA na Waziri Mkuu aliyeshinikizwa kujiuzulu kwa Kashfa mkataba tata wa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya RICHMOND, Edward Lowassa alijitokeza bila aibu wala kupepesa macho wala kumung'unya maneno na kusema UTUMBUAJI MAJIPU UNAWAONEA WAFANYABIASHARA waliokifadhili chama chake cha CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka jana.

Siku chache tu kabla ya uchaguzi wa MAMEYA wa Manispaa za Kinondoni na Ilala kufanyika, LOWASSA alikutana na wafanyabiashara wa Kariakoo waiojipa jina la Wana-MABADILIKO na miongoni mwa mambo makubwa ambayo LOWASSA aliwahakikishia wafanyabishara hao ni pamoja na:

1. Wasikate tamaa kwani 2020 atagombea tena urais na hivyo kuwataka kuendeleza harakati za mabadiliko.

2. Aliwahakikishia kuwa watapewa kipaumbele katika ZABUNI mbalimbali katika manispaa za Ilala na Kinondoni(alijuaje manispaa hizo zingeongozwa na CHADEMA?)

Yote haya yanalenda kufanikisha mambo makubwa matatu kwa mujibu wa wachunguzi wa mambo ya siasa:

1. Kutaka kuwasahaulisha Watanzania na UFISADI wa Lowassa na washirika wake(Rostam Aziz, Mazir Karamagi n.k), Ufisadi ambao umeligharimu Taifa hasara kubwa na bado unaendelea kuligharimu.

Watanzania tusijisahau, tukumbuke maneno ya mmoja wa Mahasimu wake wakubwa kwenye UFISADI wakati akiwa CCM, SAID KUBENEA aliwahi kuandika MAKALA kupitia Gazeti lake la za Zamani la MWANAHALISI, makala ilikuwa na kichwa kilichosomeka "LOWASSA HASAFISHIKI". Leo KUBENEA ni mfuta viatu vya LOWASSA. Pesa za kifisadi zimefanya kazi.

2. Mwenye asili haachi asili. Manispaa za ILALA na KINONDONI ni manispaa mama kwa Uchumi wa Taifa letu. Zinatoa Zabuni nyingi sana zenye kuliingizia taifa mapato mengi sana. Tusidanganye kwa LOWASSA hawezi kuzitumia Kampuni zake kuingia mikataba feki kupitia manispaa hizi.

Jambo moja tumshukuru Mungu kuwa sasa TAMISEMI iko chini ya OFISI YA TINGATINGA, lakini hiyo haitoshi, Nguvu ya MAFISADI haina tofauti na nguvu ya MAUZA UNGA. wanaweza kutumia kila mbinu kupenya. Naamini kama siyo Tingatinga basi washauri wake wanaingia kwenye hizi social networks. Mkisoma hii mumfikishie Mkuu.

3. Kujipatia fedha kupitia Manispaa hizo na kutoka kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2020

Ujumbe wangu kwa Lowassa ni huu: Afanye mbwembwe zote na MAMEYA wa Ilala na Kinondoni, lakini mosi, atambue kuwa mbwembwe zake haziwezi kutusahaulisha UFISADI wake , pili awe makini hii serikali ya TINGATINGA inaweza kumzoa akitumia MANISPAA hizo kuhujumu uchumi wa wanyonge.
 
Asubutu aone. Chezea Bulldozer wewe. Kama alifikiri ndo anatokea huko kwenye Umeya basi ameula wa chuya.
 
Hakuna raha kama kumjua mtu. Kama siyo fisadi, mpenda vipesa pesa, mwenye harufu harufu ya rushwa, mwenye kujipendekeza na kutaka kutubu usamehewe katu huwezi kudanganyika kwa JIZI LOWASSA. Ataendelea kutukuzwa na watu kama akina Mbowe, Babu duni, Lissu, Kubenea na Wafanyabiashara. Hao wana sifa hizo, siyo watanzania wazalendo wenye uchungu na nchi yao.
 
Lowassa no zaidi ya Fedhuli, Fashisti, Katili na Muuaji. Pamoja na wizi wote kwa Taifa, bado haoni haya kujiona anafaa kuigwa, kutegemewa, kusaidia nchii? Hiki ndicho kipindi sasa cha kumwangamiza na matawi yake yote ili Tanzania izaliwe upya.
 
Kwa sasa Lowassa anatajwa Mara nyingi sana Ofisi ndogo ya CCM Lumumba kuliko mwenyekiti wa chama hicho JK au mwenyekiti mtarajiwa JPM na hata pia zaidi ya kinavyotajwa chama chenyewe.
Inanikumbusha zamani kidogo mama mmoja alivyozua timbwili kwenye ndoa. Jirani ya kwake kulikuwa genge la Mpemba, sasa yule mama kila akichukua bidhaa mpemba anampa na nyongeza. Basi mama roho yake ikamfia Mpemba na kila saa lazima ataje Mahmudu (jina la mpemba) kwa hili au lile.
Sasa kazi ilikuwa usiku yuko na mumewe Chacha Mwita kunako shughuli, mama kileleni kaanza kulialia " mahmudu, mahmudu mahmuduuu" !!
Kilichotokea hapo mpaka leo mtaani hatujasahau. Si unajua tena hasira za Mwita Chacha?
Hivyo Lumumba jina la Lowasa kuna siku litawaponza
 
Hakuna raha kama kumjua mtu. Kama siyo fisadi, mpenda vipesa pesa, mwenye harufu harufu ya rushwa, mwenye kujipendekeza na kutaka kutubu usamehewe katu huwezi kudanganyika kwa JIZI LOWASSA. Ataendelea kutukuzwa na watu kama akina Mbowe, Babu duni, Lissu, Kubenea na Wafanyabiashara. Hao wana sifa hizo, siyo watanzania wazalendo wenye uchungu na nchi yao.
Huyo mwizi kwa nini hakamatwii?
 
Wewe una
Kwa sasa Lowassa anatajwa Mara nyingi sana Ofisi ndogo ya CCM Lumumba kuliko mwenyekiti wa chama hicho JK au mwenyekiti mtarajiwa JPM na hata pia zaidi ya kinavyotajwa chama chenyewe.
Inanikumbusha zamani kidogo mama mmoja alivyozua timbwili kwenye ndoa. Jirani ya kwake kulikuwa genge la Mpemba, sasa yule mama kila akichukua bidhaa mpemba anampa na nyongeza. Basi mama roho yake ikamfia Mpemba na kila saa lazima ataje Mahmudu (jina la mpemba) kwa hili au lile.
Sasa kazi ilikuwa usiku yuko na mumewe Chacha Mwita kunako shughuli, mama kileleni kaanza kulialia " mahmudu, mahmudu mahmuduuu" !!
Kilichotokea hapo mpaka leo mtaani hatujasahau. Si unajua tena hasira za Mwita Chacha?
Hivyo Lumumba jina la Lowasa kuna siku litawaponza
Unaona sifa kutajwa mara nyingi kwa UJAMBAZI WAKO?
 
Katika Kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikaeli Mbowe aliibuka na kusema na hapa nanukuu: "WAPO WAFANYABIASHARA WAKUBWA WATANO AMBAO WANGEWEZA KUGHARAMIA KAMPENI ZA CHADEMA, LAKINI WANAOGOPA MAJINA YAO KUTAJWA KWA KUHOFIA KUFUATILIWA NA VYOMBO VYA DOLA.

Mara tu baada ya Uchaguzi kumalizika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli(TINGATINGA) kuanza KUTUMBUA MAJIPU kama alivyoahidi Bungeni Dodoma, aliyekuwa Mgombea Urais kwa Tiketi ya CHADEMA na Waziri Mkuu aliyeshinikizwa kujiuzulu kwa Kashfa mkataba tata wa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya RICHMOND, Edward Lowassa alijitokeza bila aibu wala kupepesa macho wala kumung'unya maneno na kusema UTUMBUAJI MAJIPU UNAWAONEA WAFANYABIASHARA waliokifadhili chama chake cha CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka jana.

Siku chache tu kabla ya uchaguzi wa MAMEYA wa Manispaa za Kinondoni na Ilala kufanyika, LOWASSA alikutana na wafanyabiashara wa Kariakoo waiojipa jina la Wana-MABADILIKO na miongoni mwa mambo makubwa ambayo LOWASSA aliwahakikishia wafanyabishara hao ni pamoja na:

1. Wasikate tamaa kwani 2020 atagombea tena urais na hivyo kuwataka kuendeleza harakati za mabadiliko.
2. Aliwahakikishia kuwa watapewa kipaumbele katika ZABUNI mbalimbali katika manispaa za Ilala na Kinondoni(alijuaje manispaa hizo zingeongozwa na CHADEMA?)

Yote haya yanalenda kufanikisha mambo makubwa matatu kwa mujibu wa wachunguzi wa mambo ya siasa:

1. Kutaka kuwasahaulisha Watanzania na UFISADI wa Lowassa na washirika wake(Rostam Aziz, Mazir Karamagi n.k), Ufisadi ambao umeligaharibu Taifa hasara kubwa na bado unaendelea kuligharimu. Watanzania tusijisahau, tukumbuke maneno ya mmoja wa Mahasimu wake wakubwa kwenye UFISADI wakati akiwa CCM, SAID KUBENEA aliwahi kuandika MAKALA kupitia Gazeti lake la za Zamani la MWANAHALISI, makala ilikuwa na kichwa kilichosomeka "LOWASSA HASAFISHIKI". Leo KUBENEA ni ni mfuta viatu vya LOWASSA. Pesa za kifisadi zimefanyakazi.

2. Mwenye asili haachi asili. Manispaa za ILALA na KINONDONI ni manispaa mama kwa Uchumi wa Taifa letu. Sinatoa Zabuni nyingi sana zenye kuliingizia taifa mapato mengi sana. Tusidanganye kwa LOWASSA hawezi kusitumia Kampuni zake kuingia mikataba feki kupitia manispaa hizi. Jambo moja tumshukuru Mungu kuwa sasa TAMISEMI iko chini ya OFISI YA TINGATINGA, lakini hiyo haitoshi, Nguvu ya MAFISADI haina tofauti na nguvu ya MAUZA UNGA. wanaweza kutumia kila mbinu kupenya. Naamini kama siyo Tingatinga basi washauri wake wanaingia kwenye hizi social networks. Mkisoma hii mumfikishie Mkuu.

3. Kujipatia fedha kupitia Manispaa hizo na kutoka kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo kwa ajili ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2020

Ujumbe wangu kwa Lowassa ni huu: Afanye mbwembwe zote na MAMEYA wa Ilala na Kinondoni, lakini mosi, atambue kuwa mbwembwe zake haziwezi kutusahaulisha UFISADI wake , pili awe makini hii serikali ya TINGATINGA inaweza kumzoa akitumia MANISPAA hizo kuhujumu uchumi wa wanyonge.
Suala la kuwekeza Ilala na Kino kwa ajili ya 2020 naona ni upuuzi, angekuja na mkakati wa kwenda kujiimarisha kanda ya ziwa, kati na kusini,
unatumiaje nguvu nyingi kujiimarisha sehemu ambayo tayari ni himaya yako? Wastage of resources!
 
Umesahau jambo moja ambalo Lowassa aliwahakikishia wafanya biashara walio mtembelea nalo ni: Hawatolipa kodi UKAWA ikishinda umeya Ilala. Hii ndio ahadi ya Lowassa kwa wale wafanya biashara.
 
Back
Top Bottom