Mohamedi Mtoi
R I P
- Dec 11, 2010
- 3,321
- 6,331
Na ili kulifanikisha hili lazma turudi kwenye nationalization of schools, kusiwepo na private schools ili usawa uwepo...baada ya hapo wahamie kwenye afya, nayo iwe bure!!
Mwanangu Mtoi umeleta hoja nzuri ingawa nasita kukubaliana na Lowassa. Nani atawaruhusu tegemezi na ombaomba kutoa elimu ya bure wakati bajeti yao inategemea wafadhili. Laiti angesema kuwa kama tutasimamia raslimali zetu na kodi vilivyo hili la kutoa elimu bure lingewezekana ningemwelewa. Lowassa anaongea kama mgombea wa urais wa Marekani Mitt Romney. Ni pendekezo zuri ingawa sijui kama alionyesha jinsi ya kulifanikisha.
Na ili kulifanikisha hili lazma turudi kwenye nationalization of schools, kusiwepo na private schools ili usawa uwepo...baada ya hapo wahamie kwenye afya, nayo iwe bure!!
Naona Lowassa ameanza kampeni mapema
OKANilifikiri wamesham write off by now? kumbe bado yupo kwenye mbio?
Mtoi,Mkuu wangu Father of All
Naamini Lowasa ni sawa na kata inayoingia kwenye mtungi, si unakumbuka ule msemo "siri ya mtungi aijuaye kata", anajua kuwa serikali ni tegemezi sana hasa kwenye bajeti lakini nachelea kusema huenda ana kifuniko cha siri moyoni na anajua kuwa waliyo kuwa wanapinga yanawezekana.
Nakubaliana na wewe kuwa hajaonyesha njia kuwa itawezekana vipi (Romnesia) lakini naamini anajua kuwa kama wenzake wa ccm wakiwa naka uzalendo kidogo na huruma kwa taifa hili, wanauwezo wa kutoa elimu bure kuanzia msingi hadi sekondari na hata kuwapatia wastaafu wa nchi kiasi cha shilingi elfu 30 kwa mwezi kwa kuanzia ili angalau kuwapunguzia machungu ya kulipa bili za umeme za na maji au kununua mafuta ya taa kwa ajili ya vibatari vyao na kandili zao.
Inawezekana! Waliyopinga miaka 3 iliyopita leo wanakiri hadharani kuwa inawezekana. Hizi ni alama za wanafiki kwenye imani yangu.