Unaandika ukiwa umatokea nchi za nje au upo hapa hapa Tanzania.Inamaana wewe hujui Slaa kajiondoa Chadema na aliombwa a kuabudiwa ili arudi akakataa.Hivi unafikiri ccm ndiyo imeumba Tanzania.Lazima tujue Tanzania ni yetu wote.Kila msaliti wa haki na ukweli ataadhibiwa na natural law kikamilifu.Ach kujitoa ufahamu.Wote waliojiinua kinyume cha haki na ukweli na kutumia kodi zetu kwa lengo la kumchafua mtu na kujisahau hata wao ni wachafua yatawakuta mambo makuu wataanguka siku moja na wasijue kilichowaangusha.Namna alivyondolewa Dr Slaa chadema naifananisha kama namna alivyoondolewa Samwel Etoo Barcelona. Tokea kipindi hicho sijawahi kuifurahia Barcelona tena.
Hoja siku hizi imekuwa kwanini amkumpeleka mahakamani hawa majamaa ata kesho wanaweza kuibuka na kutuambia Rostam Aziz amekuwa anasingiziwa tu kwa muda mrefu, wakati ni wao wenyewe ndio waliotumia nguvu nyingi kutuaminisha huyo mtu afai kama walivyofanya kwa Lowassa wanaemtetea leo.
It begs ze kwesheni kama kweli ni waumini wa kile wanachosema kama wanaweza jikana wao wenyewe pia hadharani. Maswali ni mengi kuliko majibu kwa wale wanaoamini uongozi wa CDM chini ya Mbowe niwakutukuka.
Wewe ufisadi hauwezi kuwa mwisho wakati mtarajiwa wenu ndo fisadi nyangumi, na kukishakuwa na ufisadi UJINGA,UMASIKINI,MARADHI,UJANGILI, NA MIKATABA MIBOVU lazima viongezeke kwa kasi ya ajabu kisemo chake.
Acha kukariri wewe, toka ameondoka serikalini mwaka 2008 ufisadi umeisha? ESCROW, meremeta, EPA, nyumba za serikali, net group solution, mikataba mibovu, kivuko cha zamani kwa bei mpya, vyote kavifanya Lowassa? Twiga kupanda ndege, kuuliwa kwa ndovu, hivi ni Lowassa aliyechukua hela kwenye viroba pale Stan Bic bank? Usitumie masaburi kufikiria
Kalugendo ni vigumu sana kubadili kaniki kuwa nyeupe. Kwa wale wasojua kaniki ni vazi jeusi huvaliwa ns wamama kama kitengeTupo tayari kuitwa majina yoyote mpendayo lakini shida yetu ni huyo jini mnayemkumbatia kwa miaka mingi bila kuona kinachofanyika nyie endeleeni na hoja za dr.Slaa wacha sisi tusonge mbele tunaamini tutakutana mbele ya safari.
Karugendo,Nawe kama sikosei ni kasisi wa calibre ya Slaa.Ni ukweli usiopingika kwamba Dr alikuwa na lengo la kutufumbua macho juu ya kiongozi anayewania kuongoza taifa hili.Watu wangemuelewa vizuri kama angegusia upande wa pili wa shilingi kwa kueeza pia Ccm imefanya mabaya mangapi dhidi ya watanzania na kuwafahamisha ni vipi huyo mgombea anavyoweza kudhibiti fisi waliomzunguka ili hali yeye ni mwanakondoo. Kitendo cha kutogusia Escrow.Kiwira,epa nk ndicho kinapelekea jamii ya kitanzania imchukulie kama ametumwa vile.Huko alikoelekeza kisogo chake ndo kiwanda cha kupika maovvu kwani hata anayemzungumzia ametengenezwa huko huko nao wakafumba macho.
Pia kitendo cha Slaa kukiri kwamba
a alikutana na Mwakyembe muda mfupi kabla ya kutable alichokusudia nalo ni ombwe lingine.Nami naungana na lile kundi linalomwona Dr alikuwa pia msaka madaraka.
Mfikishieni salaam hizi huyu Karugendo na asalimie parokia yake huko Bushangaro Krg.
Tunakuhabarisha Lowasa anaenda kuongoza Tanzania kwa kibali cha Mungu huyu huyu unayemtumaini wewe nami pia.
Kwa sababu ni wao ndio waliokuwa vinara wakutuambia Lowassa ni wakufungwa ina maana pia wanatakiwa kuwa na ushaidi pia.Sasa na wewe mtu mhalifu anatakiwa apelekwe wapi? Mhalifu yeyote sheria inatakiwa ichukue mkondo wake mbona mramba na yona wapo jela wengine kwa nn hawajapalekwa toka 2008 walipojiuzulu?
Sasa na wewe mtu mhalifu anatakiwa apelekwe wapi? Mhalifu yeyote sheria inatakiwa ichukue mkondo wake mbona mramba na yona wapo jela wengine kwa nn hawajapalekwa toka 2008 walipojiuzulu?
Ndugu yangu Karugendo ....Taifa limepigwa ganzi ....Leo kuna watu wanataka hata kumpiga mawe Dr Slaa ....huu usaliti tuliomfanyia baada ya kuweka roho yake rehani kwa muda mrefu kujenga Chama na kutetea wanyonge unasikitisha sana ..... Kwa tabia hii itazaa watu waoga kutetea taifa wakijua ni rahisi Kuwa twist Watanzania .....Leo hakuna hata anayetaka kufikiri ...