Lowassa, Chenge were lined up for Speaker's job

Its very painful kuona watu tunashabikia hii spinning ya ndugu yetu Mzee Mengi, waandishi wa habari waliojaa urambo walikuwa ni wa IPP MEDIA, bahati mbaya maandamano yakawa a BIG BIG FLOP, ikabidi aite waandishi wa habari nyumbani kwake nidyo aongee na kesho yake akaenda kwenye mkutano wa injili tabora mjini ili anagalau Mengi apate picha zenye umati wa watu.
Kwanini tukuamini wewe? tutajua vipi kama wewe siyo spinning doctor?

Kwenye gazeti lao la kiswahili KULIKONI walisema vikao vingne vilifanyika Zanzibar, kwahiyo hapa unaongelea kona zote za nchi, yaani Dodoma, Dsm, Mbeya na Znz, kwa maana hii upinzani wa Spika kwenye chama chake ni mkubwa sana.. tujiulize kwanini? Tusishabikie wamenunuliwa, maana yake ndiyo easy way out siku hizi, huwezi kununua wenzako wenye akili timamu ili waseme ambayo hawayaamini, hata kama ungekuwa Bill Gates.
sababu zilizotolewa ni kuwa spika anaiachia mijadala ya ufisadi ijadiliwe bungeni. This is the saddest milestone point we are! Sasa kwanini tusiamini kuwa wamenunuliwa na mafisadi? Kumbuka point kubwa ya NEC ilikuwa ni kuzuia mijadala ya ufisadi au inayodhoofisha chama ndani ya bunge ila ijadiliwe ndani ya kamati ya wabunge wa CCM iliyo chini ya Waziri Mkuu. Sasa wewe unataka twende wapi wakati mambo yote yamewekwa hadharani hata kwenye maazimio ya NEC?

Halafu hii spinning kusema a reliable source bila kumtaja nidyo yale yale ya kuaminishwa mambo ili wafikishe ujumbe wao, lakini bado hiyo source inasema hana uhakika kama Lowassa na chenge walikuwa na taarifa.. maana yake nini sasa??
wewe ndo unaita spinning, lakini mwandishi na editor wake wamesema reliable source? unahoja gani ya kupinga? mwandishi analindwa na maadili na sheria juu ya kuiweka wazi source yake/wake.

Yale yale niliyosema ya kununuliwa, kwahiyo mnataka kuniambia Mzee Kingunge alipewa Tsh ngapi?? Alisema Sitta hatufai na arudishe kadi yetu.
wewe ndo unaona Kinguge hanunuliwi, au bei ya Kigunge ipo juu sana? At least we know that Kigunge used to be socialist but these days has turned to capitalism. Jamaa ni mpebari sasa, hana imani za ki-socialist tena, hivyo ku-support bigshots ndani ya chama ndo sera yake.

What a shame?? Tunasema leo wajumbe walipewa 3M na 5M, mimi ningekuwa mwenyekiti wa CCM ningewa-summon hili gazeti ili wathibitishe, yaani hizo pesa ndiyo za kununua wajumbe wa NEC? Embu haraka haraka jitajie mwenyewe majina ya wajumbe wa NEC wenye shida na 3M - 5M, mpaka wajidhalilishe kuongea jambo ambalo hawaliamini mbele ya umati wote huo
anao wanasheria wa chama, wanaweza kufungua mashtaka kama wapo tayari kushinda au kuumbuka. Haya ndo yaliyomkuta Londa na Makamba bungeni. Kipindi cha kufanya uhalifu na kusingiza ushahidi kimepitwa na wakati. Sasa hivi technologia imekuwa, werevu umeongezeka na kujiamini kumeongezeka. Nami nitafurahi kama CCM italishtaki gazeti husika ili haki itendeke, either kwa kumkama mwongo au kuiumbua na kuiua CCM kabisa mafisadi kabisa.

amani vita ya ufisadi ni muhimu kwa taifa lolote, lakini ni muhimu ifnaywe bila kuonea watu fulani. Mengi anataka kutuaminisha mafisadi ni hao aliowataja yeye, bahati nzuri tukapewa facts za ufisadi wake na akabatizwa FISADI NYAGUMI, lakini zote hizo ni allegations tu ambazo zimeruhusiwa kwenye vyombo vya habari, lakini hamna mtu mwenye haki ya kumnyooshea mwenzake kidole kumuita fisadi, tusimamie sheria zetu vizuri na haya mambo hayatasumbua, UFISADI sasa hivi unatumika kama kete ya kisiasa kuwashughulikia watu wote waliokuwa karibu na JK tu. Kwa mwendo huu hatutafika popote.
Sawa lakini nani wa kuiongoza hiyo vita? kama Serikali (yenye taarifa zote tena kamili) haichukui hatua, individuals au vikundi vya watu vitachukua hatua kulingana na taarifa chache walizonazo ambazo pia zinaweza zikawa na makosa. Sasa hapa ilaumu Serikali inayokumbatia mafisadi wa Richmond/Dowans, Kagoda, CIS, Meremeta, Tangold etc. Tambua kwamba wananchi hawawezi kuacha kuchukua hatua kwa kiwango wanachoona inafaa ili angalau kuziba pengo lililoachwa wazi na wahusika yaani serikali. Umesoma kusadikika mzee? kama bado kitafute uungane na Shaban Roberts...
 
Its very painful kuona watu tunashabikia hii spinning ya ndugu yetu Mzee Mengi, waandishi wa habari waliojaa urambo walikuwa ni wa IPP MEDIA, bahati mbaya maandamano yakawa a BIG BIG FLOP, ikabidi aite waandishi wa habari nyumbani kwake nidyo aongee na kesho yake akaenda kwenye mkutano wa injili tabora mjini ili anagalau Mengi apate picha zenye umati wa watu. Gazeti la serikali Habari Leo na menigne mawili yalisema masafara ulikuwa na magari mawili urambo.. Inasikitisha na inauma, nilifikiri Sitta ni kipenzi cha wananchi.

Mbona hayo magazeti mengine 2 hujayataja? Magazeti yaliyo report safari hiyo hayakusema kuhusu msafara wa magari mangapi. Wao wali ripoti kwamba alihutubia vijiji 3 njiani akiwa anaelekea Jimboni kwake Urambo. Na alipofika Ndorobo ndipo alipokuta watu wengi wenye pikipiki na wengine wakitembea kwa miguu, na ikiwa imebaki kilomita moja alishuka kwenye gari na kutembea kwa miguu. Sasa utata uko wapi and where is the BIG BIG FLOP? Kwani wapiga kura wa Sitta wako Tabora Mjini ama wako Urambo Mashariki? Na wewe naona unatuletea spin zako kwa malengo yako.

Kwenye gazeti lao la kiswahili KULIKONI walisema vikao vingne vilifanyika Zanzibar, kwahiyo hapa unaongelea kona zote za nchi, yaani Dodoma, Dsm, Mbeya na Znz, kwa maana hii upinzani wa Spika kwenye chama chake ni mkubwa sana.. tujiulize kwanini? Tusishabikie wamenunuliwa, maana yake ndiyo easy way out siku hizi, huwezi kununua wenzako wenye akili timamu ili waseme ambayo hawayaamini, hata kama ungekuwa Bill Gates.

Kinachoongelewa ni mikutano ya mafisadi katika harakati za kutafuta wajumbe wawaunge mkono kwenye hoja waliyokuwa nayo mafisadi. Unapochanganya wananchi na mikutano ya mafisadi unachanganya mambo na analysis yako inaonekana ni ya kitoto. Kufanyia mikutano kwenye hayo maeneo haimaanishi kwamba watu wa mikoa hiyo ndiyo wanampinga Sitta, bali ni juhudi za kusaka wajumbe wa kuunga mkono hoja!

Halafu hii spinning kusema a reliable source bila kumtaja nidyo yale yale ya kuaminishwa mambo ili wafikishe ujumbe wao, lakini bado hiyo source inasema hana uhakika kama Lowassa na chenge walikuwa na taarifa.. maana yake nini sasa??

Kulikoni au ThisDay siyo gazeti la kwanza kutoa habari ambazo zimetoka kwenye chanzo cha kuaminika ambacho hakisemwi. Vyanzo vya habari hizo vingekuwa vinatajwa iwapo Tanzania tusingekuwa na sheria mbaya ya Magazeti. Pamoja na hayo, mbona RA alipotoa habari kwenye gazeti la Tanzania Daima hakuna aliye-question chanzo cha habari cha Tanzania Daima? Au ni kwa vile Kulikoni na ThisDay ni magazeti ya Mengi ambaye ana ugomvi na RA & Co.?


Yale yale niliyosema ya kununuliwa, kwahiyo mnataka kuniambia Mzee Kingunge alipewa Tsh ngapi?? Alisema Sitta hatufai na arudishe kadi yetu.

Kwani Kingunge ana tofauti gani na RA? Wote ni mafisadi. Kingune is another fisadi na ufisadi wake ni wa moja kwa moja kwa kuwa unahusu familia yake moja kwa moja, biashara za kifisadi za Kingunge zinafanywa na mkewe na wanae. Mkataba wa kwanza unaomgusa Kingunge ni wa pale Ubungo, Stendi ya Mabasi ya kwenda mikoani. Kwa hiyo Kingunge anaweka uzio ili kesho na keshokutwa asije akaguswa kwenye anga zake za ufisadi. Kwa taarifa yako ni kwamba wanaompinga Sitta wako makundi 2, wako wananunuliwa na wako wenye maslahi ya moja kwa moja. Niliwahi kuhoji hapa kwamba ikipelekwa hoja ya ufisadi kwenye Kamati ya Maadili ya CCM, je, Chenge anaweza kuchangia bila kuwa biased? Tayari ana tuhuma nzito na bado miaka yake 10 ya uanasheria mkuu wa serikali ameiingiza nchi kwenye mikataba ya ajabu ajabu sana, hakuna hata mkataba mmoja ambao una nafuu kwa serikali, yote ukiingalia unaweza kujiuliza hivi huyu mwanasheria mkuu ana certificate in law ama ana degree ya sheria kabisa?

What a shame?? Tunasema leo wajumbe walipewa 3M na 5M, mimi ningekuwa mwenyekiti wa CCM ningewa-summon hili gazeti ili wathibitishe, yaani hizo pesa ndiyo za kununua wajumbe wa NEC? Embu haraka haraka jitajie mwenyewe majina ya wajumbe wa NEC wenye shida na 3M - 5M, mpaka wajidhalilishe kuongea jambo ambalo hawaliamini mbele ya umati wote huo.

Kuna wajumbe wa NEC ambao kwao hela yoyote ile inamtosha anachoangalia ni hela tu, wewe ndiyo unaona kwamba milioni 3 au 5 ni kidogo sana, lakini wako walio hongwa hizo na wakaona zinawatosha. Labda nikuulize wewe, wajumbe wengi waliokuwa wakali walikuwa ni kutoka Zanzibar, je, ni kwanini? Ukishatoa jibu la swali kwanini Wazanzibari watetee ufisadi wakati kule kwao kuko safi, ndiyo utaelewa kwamba kuna watu walihongwa hizo milioni 3 au 5.

Wengi wa waliokuwa wanadai kwamba Spika hafai ukiwachunguza kwa ndani wamezungukwa na tuhuma za ufisadi, kwa hiyo wanachohofia wao ni kwamba kama mambo yakiachwa kama yalivyo, basi iko siku na wao wataguswa na kuwekwa kikaangoni. Kama Lowassa alikaangwa na juhudi za kumsafisha zinagonga mwamba, hao wengine watapona? Ukiangalia watu kama Komba wa TOT Plus ana tuhuma za matumizi mabaya na ziko kwa Makamba, Mgeja ana tuhuma za kuifilisi SHIRECU na CCM inajua lakini inafumbia macho.

Jamani vita ya ufisadi ni muhimu kwa taifa lolote, lakini ni muhimu ifanywe bila kuonea watu fulani. Mengi anataka kutuaminisha mafisadi ni hao aliowataja yeye, bahati nzuri tukapewa facts za ufisadi wake na akabatizwa FISADI NYAGUMI, lakini zote hizo ni allegations tu ambazo zimeruhusiwa kwenye vyombo vya habari, lakini hamna mtu mwenye haki ya kumnyooshea mwenzake kidole kumuita fisadi, tusimamie sheria zetu vizuri na haya mambo hayatasumbua, UFISADI sasa hivi unatumika kama kete ya kisiasa kuwashughulikia watu wote waliokuwa karibu na JK tu. Kwa mwendo huu hatutafika popote.

Sentensi ya kwanza ninakuunga mkono, lakini maelezo yanayofuata umechemka na hasa ulivyokuja kumalizia sentensi zako za mwisho. Nina uhakika kwamba kama Mengi angekuwa na tuhuma za ufisadi ambazo zina evidence, siku nyingi sana angeishatinga Kisutu ama Mahakama Kuu, kwani siyo Mengi waliyesema wanatafuta njia ya kummaliza ili kumnyamazisha na hayo mambo yakaishia kimya kimya na waziri aliyehusika na tuhuma hiyo aliingia mitini mpaka leo hii.

Madai kwamba vita ya ufisadi imeelekezwa kwa watu waliokaribu na JK hapo umeenda nje ya mstari kabisa. Kwa hiyo unataka kutumia hiyo kama excuse kwa EL na RA ili wasishambuliwe na ilhali wao ni mafisadi? Serikali ya JK inawaogopa kwa kuwa na JK nae ni mhusika wa some of the deals na ndiyo maana Luhanjo na Rweyemamu walipoona maji yameanza kuzidi unga wakaanza kumtetea boss kwamba hahusiki na Richmond. Pia kitendo cha kutowashughulikia wale wote ambao walihusika na Richmond inaonyesha wazi kwamba kiongozi mkuu wa serikali (JK) ana mkono ama alikuwa na maslahi kwenye hilo deal na sasa mnataka kuanza kutudanganya kwamba vita ya ufisadi inapigwa kwa kuangalia walio karibu na JK.

Wahusika wa Kiwira wako karibu na JK? Wahusika wa TICTS nao wako karibu na JK? Yule aliyekuwa Mh. Balozi wa Italy (Prof Mahalu) nae ni rafiki wa JK? Mzee wa Twin Tower za Benki Bwana Liyumba nae ni best wa JK? Jamani tunapojenga hoja tuje na facts na siyo kutumia mfano mmoja tu ambao unamgusa RA na EL. Yaani hawa mabwana wawili wakiguswa tu serikali nzima na CCM yote matumbo moto na wanakuja juu kama moto wa kifuu kuwatetea kwa nguvu zote mpaka mapovu yanawatoka midomoni. Halafu baada ya hapo utawasikia kwamba kila mtu abebe mzigo wake wa ufisadi individually lakini asihushwe na chama. Ila Sitta akiruhusu mijadala ya ufisadi unaofanywa na hao vigogo kwa kushirikiana na serikali linakuwa ni kosa, what a double standard!
 
Nimependezwa na majibu ya ndugu zangu hawa wawili, kwasababu wamejaribu kujibu kwa hoja, na ndivyo JF inavyotakiwa kuwa, tushindane kwa hoja na facts na siyo matusi na jazba. Ahsanteni kwa michango yenu, inapendeza.

Nduguzanguni, fanyeni utafiti wenu wa influence ya media kwenye jamii, especially nchi kama ya kwetu ya dunia ya tatu, the influence of the MEDIA is very very powerful, you cannot ignore it kabisa, leo Mengi kwenye matukio anaitwa Mheshimiwa na anazo guts za kubishana na Mawaziri wa serikali ya jamhuri anavyotaka, na mara nyingi ameshinda. Hao Mawaziri kwanza wamechaguliwa na wananchi majimboni na baadaye wameteuliwa na RAIS wa nchi na amiri jeshi Mkuu, lakini bado Mengi ana kifua cha kulumbana nao, why??/ POWER OF THE MEDIA.

Leo hii tunataka kuongea huyu ni Fisadi sana, lakini Sitta na wateule wake kumi na moja, nasikia wanaitwa 'first eleven' siku hizi, wao ndiyo wasafi sana na ndiyo mashujaa wa nchi hii, kabla ya 2005 hatukumbuki walishiriki wapi kwenye maendeleo ya nchi, historia ya nchi hii ikiandikwa, tutakumbuka hili kundi kwa lipi?? Hii miaka miwili wao ndiyo wamekuwa heroes na majemadari wakubwa. Watu wapo walioleta mapinduzi ya uchumi nchi hii.. ndiyo Mafisadi wakubwa.... Wapo waliosimamia mikakati ya elimu nchi nzima.. ndiyo mafisadi... Why?? Why?? Why?? hivi nchi yetu tumelogwa wote? Tunafanya uchambuzi wetu kwa kutumia nini??

Wengi wa wapenzi wa JF ni watu wenye access na computer, kwahiyo wameajiriwa, wasomi vyuoni vya ndani na nje ya nchi etc., kwahiyo ni watu wenye exposure kidogo. Tuitendeeni nchi yetu haki yake, tutoe michango ya kujenga, ili kweli hata Rais wetu mpendwa aweze kuingia huku kwa kupata maoni ya kujenga, tusichoke, na tuache jazba.

Tanzania Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote... Wote tunaipenda nchi yetu tena sana sana, lisitudanganye kundi la watu kwa influence ya media.

Nimechagua ku-avoid kujibu mambo ya Mzee Kingunge na wajumbe wa NEC, kwasababu nilijaribu kuelewa imekuwaje mpaka tutukane watu wote hivi, tujiulize vizuri. Haiwezi kuwa watu wote hao ndiyo baya, halafu kundi dogo la Sitta na 'first eleven'na mengi ndiyo mashujaa nchi hii, there must be a problem somewhere. Tuiombee nchi yetu, tunapitia kipindi kigumu.
 
Mimi naona sasa tumekuwa tunatumika tu na waandishi wa habari wanaogeuza hata siasa na utawala wa nchi yetu kama novel na riwaya fupifupi ili wauze magazeti ambayo kwa sasa hayana tofauti kubwa na vitabu vya "someni kwa furaha" n.k.

Mkuu umenikumbusha mbali sna. Kitabu kilikuwa kinaitwa "someni bila shida" Makali hodari. Bulicheka. Lizabeta na wengine wengi. Wale jamaa walikuwa makini sana na hadithi zile ndio maana hadi leo tunazikumbuka. Kuna magazeti mengine unaweza kusoma asubuhi jioni unasahau ulisoma nini. Kuna porojo nyingi na uchwara mwingi ambao unaonesha kuwa hawafanyi research kabla ya kuandika. Hawa ndio wanachangia sana kulea mafisadi. Japokuwa siku hizi kuna magazeti mawili matatu yameonesha mwelekeo wa kuwa makini!
 
Siku hizi magazeti ya IPPMEDIA yanatengeneza habari badala ya kutupa yaliyotokea au kutupa maoni yao.Hivi CCM watakuwa wapumbavu kiasi gani kutaka Lowassa au Mzee wa vijisenti wawe Spika?Hata wakitaka kumtoa Sitta watampendekeza mtu atakaye weza kupata kura za wabunge na kukubalika na wananchi.Sitta badala ya kuwa na kundi dogo la maswahiba wake bungeni ajaribu kuwa karibu na wabunge wengi zaidi na hii itampa kinga ya chama kutoweza kumpoteza.Sasa hivi chama kinafahamu kundi la Sitta halizidi wabunge 20 na nirahisi kumyumbisha.
 
Hawa watu wanatuhumiwa kwa ufisadi. Ni ajabu kwamba wanataka kuwa Speaker. CCM,tunatumaini itachukua muda kidogo kujadili swala la ufisadi,katika NEC Butiama,kabla
 
Back
Top Bottom