johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,968
- 141,976
Kuna vijana wadogo hapa Jf wanadhani tuhuma za Lowassa kwamba ni fisadi zilianzishwa na Dr Slaa kwa msaada wa Tundu Lisu pale mwembeyanga, Hapana.
Tuhuma za ufisadi kwa Lowassa zilianza mwaka 1995 wakati yeye na rafiki yake Kikwete walipochukua form za kuomba kuteuliwa na CCM kuwa wagombea wa urais. Wakati huo wakijulikana huku mtaani kama Boys II Men.
Ni pale marafiki walipotumia ndege ya kukodi wakiwa na rafiki zao Temu MD wa Bima na Mattaka MD wa PPF ndipo wazalendo wakaanza kuhoji ukwasi wa Lowassa.
Walichokifanya Chadema wakati ule ilikuwa ni kudandia treni na kutafuta umaarufu wa kisiasa, wakamfanya Lowassa kuwa ajenda yao kwenye mikutano yao ya kisiasa.
Waswahili husema " mwiba hutokea ulipoingilia" na ndicho alichokifanya Lowassa 2015 kwa kuitumia Chadema kama bafu la stendi....na baada ya kuoga amerudi nyumbani.
Kwa wale wasiojua, Lowassa alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya ulinzi na mambo ya nje. Edward anaijua kanuni ya urais na alienda Chadema akijua kwa hawezi kuwa Rais, hivyo alienda pale " kutakaswa" na kwa bahati mbaya sana katika kundi lile lililojiita UKAWA aliyeshtukia janja ya Lowassa ni Dr Slaa na Prof Lipumba basi.
Sasa Lowassa ametakasika kajirudia nyumbani kulikonoga
Maendeleo hayana vyama!