Lowassa: CCM ilimtuhumu ufisadi akiomba kugombea urais 1995. CHADEMA imemsafisha akigombea urais 2015

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,087
2,000
Kuna vijana wadogo hapa Jf wanadhani tuhuma za Lowassa kwamba ni fisadi zilianzishwa na Dr Slaa kwa msaada wa Tundu Lisu pale mwembeyanga, Hapana.

Tuhuma za ufisadi kwa Lowassa zilianza mwaka 1995 wakati yeye na rafiki yake Kikwete walipochukua form za kuomba kuteuliwa na CCM kuwa wagombea wa urais. Wakati huo wakijulikana huku mtaani kama Boys II Men.

Ni pale marafiki walipotumia ndege ya kukodi wakiwa na rafiki zao Temu MD wa Bima na Mattaka MD wa PPF ndipo wazalendo wakaanza kuhoji ukwasi wa Lowassa.

Walichokifanya Chadema wakati ule ilikuwa ni kudandia treni na kutafuta umaarufu wa kisiasa, wakamfanya Lowassa kuwa ajenda yao kwenye mikutano yao ya kisiasa.
Waswahili husema " mwiba hutokea ulipoingilia" na ndicho alichokifanya Lowassa 2015 kwa kuitumia Chadema kama bafu la stendi....na baada ya kuoga amerudi nyumbani.

Kwa wale wasiojua, Lowassa alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya ulinzi na mambo ya nje. Edward anaijua kanuni ya urais na alienda Chadema akijua kwa hawezi kuwa Rais, hivyo alienda pale " kutakaswa" na kwa bahati mbaya sana katika kundi lile lililojiita UKAWA aliyeshtukia janja ya Lowassa ni Dr Slaa na Prof Lipumba basi.

Sasa Lowassa ametakasika kajirudia nyumbani kulikonoga

Maendeleo hayana vyama!
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,087
2,000
Lengo la ccm mpya mlikua mnajinadi Eti mnamwaga oil chafu!
Mbona sasa hivi Mnatia tena hiyo oil chafu?

Lowasa, Rostam.....

Mnameza matapishi safari hii
Tundu Antipas Lisu anasema Lowassa haijawahi kushtakiwa mahali popote hapa duniani na hata kule mbinguni hivyo ni msafi!
 

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,082
2,000
Tundu Antipas Lisu anasema Lowassa haijawahi kushtakiwa mahali popote hapa duniani na hata kule mbinguni hivyo ni msafi!
Kama ni mchafu sasa amerudi kwenu!
Haya mpelekeni mahakama ya mafisadi!

Swali la nyongeza!
Hivi chenge Si alitajwa kwenye ripoti za makinikia zaidi ya Mara mbili?
Mbona bado mmemkumbatia na hamumshtaki?

Aiseee awamu inaendeshwa kihuni hii sijawahi ona
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,087
2,000
Kama ni mchafu sasa amerudi kwenu!
Haya mpelekeni mahakama ya mafisadi!

Swali la nyongeza!
Hivi chenge Si alitajwa kwenye ripoti za makinikia zaidi ya Mara mbili?
Mbona bado mmemkumbatia na hamumshtaki?

Aiseee awamu inaendeshwa kihuni hii sijawahi ona
Lowassa ameshaoga kwenye bafu la kulipia hapo Ufipa sasa yu msafi kisiasa!
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,652
2,000
Eti ccm mpya!
Vijana mna vituko sana aisee!

ccm ina wenyewe bhana na wenyewe ni hao akina lowasa, rostam, chenge etc
Unataka kurudisha ule ubishi wa anakatwa hakatwi?CCM ni ya wananchi wazalendo hakuna mwenye nguvu zaidi ya Chama...ukizingua unakatwa unafunzwa adabu na unarejeshwa kundini.
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,087
2,000
Wewe kweli pang'ang'a na Wa juzi tu. Unapoandika jambo humu jua kuwa kuna werevu na wakongwe. Hivi 1995 CHADEMA ilikuwa hata maarufu uchaguzini?
Mbwiga 1995 huko upinzani maarufu ilikuwa Nccr mageuzi ya Mrema na Marando.

Chadema haijawahi kuwa maarufu hadi mwaka 2015 Lowassa alipokuja kuoga ndio ikapata umaarufu wa muda.

Nccr na Cuf ndio vyama vya upinzani vilivyoandika historia usisahau hilo!
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,116
2,000
Wewe kweli pang'ang'a na Wa juzi tu. Unapoandika jambo humu jua kuwa kuna werevu na wakongwe. Hivi 1995 CHADEMA ilikuwa hata maarufu uchaguzini?
1995 Mwl Julius Nyerere (RIP) alikuwa akipambana na Mrema jukwaa kwa jukwaa kuhakikisha Mkapa anaingia Ikulu. CHADEMA ilikuwa haipo kabisa kwenye rada. Watu walilala nje kulinda kura za Mrema ila bado bao la kiwiko likapigwa
 

Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,668
2,000
Tundu Antipas Lisu anasema Lowassa haijawahi kushtakiwa mahali popote hapa duniani na hata kule mbinguni hivyo ni msafi!
Yah right ....... Innocent until proven guilty!!

Sasa huyu aliyekuja na Mahakama ya Mafisadi kwa nini asimshughulikie na huyu Bwana ili kila mtu alizike kuwa yuko kwenye group gani!!?
 

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,861
2,000
CCM waliwatuhumu kwa ufisadi wote 2 Kikwete na Lowassa, na wakawatakasa wenyewe,baadae kilichofuata Kikwete alikuwa Rais na Lowassa akawa waziri mkuu na tangu hapo CCM hawajawahi kusema kuwa viongozi wa nchi wanaotokana na chama chao ni mafisadi, kwa hiyo Lowassa alikwenda CHADEMA akiwa ametakaswa na CCM wenyewe.
 

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,554
2,000
Mbwiga 1995 huko upinzani maarufu ilikuwa Nccr mageuzi ya Mrema na Marando.

Chadema haijawahi kuwa maarufu hadi mwaka 2015 Lowassa alipokuja kuoga ndio ikapata umaarufu wa muda.

Nccr na Cuf ndio vyama vya upinzani vilivyoandika historia usisahau hilo!
Sasa isome mada yako tena. Pang'ang'a we!:D:D
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom