Lowassa azungumzia hatma yake CHADEMA

Lowassa azungumzia hatma yake CHADEMA

“Tumepigana pamoja,tunangojea kupangana kupiganapamoja kwenye uchaguzi ujao, anayesema ninataka kuondoka Chadema anajifurahisha, nataka kuwahakikisha wanachama wa Chadema na wananchi nipo Chadema na nitaendelea kuwa Chadema


Lakini unakumbuka ukiwa bustanini ulisema hivihivi na kuwaaminisha watu kuwa wewe ni vegetarian utakufa ukila ugali wa yanga na mboga za majani hadi ukamilifu wa dahari? Ghafla ukabadilika na kuanza kula ugali mweupe wa kukobolewa na nyama nyekundu kwenye sahani ya blue!? Tukuaminije Lowasa
 
Tatizo hapa siyo yeye kusifiwa bali KUSIFIA ......... Pale anapodai kuwa JPM anafanya kazi nzuri bila kueleza pale anapokosea inamaanisha kuwa anamkubali. Kama ameridhika na kazi nzuri ya Rais kuna haja gani ya yeye kugombea 2020!!
 
Huyu naye kesha buma kilichobaki akasomee ushemasi kwa waluteri lakini auleze umma namna alivyojipatia Mali na auleze ni kwa nini Chadema walimuweka katika orodha ya juu ya waporaji wa mali za umma !
 
Bavicha wameshawatosa Lowasa ,Lisu ,Mbowe ,Sumaye mahaba yao yote yapo kwa Membe.

Lisu amenuna sana
Mfikishieni ujumbe bashiru asithubutu kumwekea zengwe lolote Membe, sisi wanaccm tumeamua mgombea urais bendera apeperushe Membe.
 
Dar es Salaam. Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amefunguka kuhusu hatima yakendani ya Chadema na kusisitiza kuwa hana mpango, hajafikiria wala hajapanga kuondoka katikachama hicho kikuu cha upinzani nchini.“Sina mpango wa kuondoka Chadema, sijapanga wala sijafikiria kuondoka Chadema,” alisema Lowassa alipofanya mahojiano maalumu na Mwananchi ofsini kwake jijini Dar es Salaam jana.Lowassa alizungumza na Mwananchi kwa mara ya kwanzabaada ya viongozi wa chama hicho kumtaka ajitokeze na kuweka wazi msimamo wake.Mwanzoni mwa wiki hii, naibu katibu mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu alimtaka Lowassa kujitokeza kuweka msimamo wake hadharani baada ya kusifiwa mara kwa mara na viongozi wa juu wa CCM na Serikali.“Siasa maneno mengi siku hizi, kila mahali maneno.. maneno,” ndivyo alivyoanza kujibu Lowassa alipoulizwa kuhusu madai kuwa ana mpango wa kurejea CCM.“Ningetaka kuweka wazi kwa Watanzania na wanachama wa Chadema kwamba sina mpango wa kuondoka Chadema hata kidogo, sina mpango wa kuondoka Chadema, sijapanga wala sijafikiria kuondoka Chadema,” alisema Lowassa aliyezaliwa miaka 65 iliyopita wilayani Monduli.Waziri huyo mkuu wa kwanza waSerikali ya Awamu ya Nne alisema, “Ninazo sababu nyingi, katika uchaguzi uliopita walionibeba ni Chadema na walinibeba tukazunguka na tukapeperusha bendera zetu nchi nzima vizuri na kwa umakinina tukapata watu waliotuamini.”Lowassa ambaye ni Waziri Mkuuwa kwanza kuhamia upinzani katika historia ya Tanzania, alisema anakosa sababu ya kuwaambia watu milioni sita waliompigia kura katika uchaguzi mkuu uliopita.Katika uchaguzi huo aligombea nafasi ya urais kupitia muunganowa vyama vinavyounda Ukawa (Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD) na kupata kura 6,072,848 (sawa na asilimia 39.97) akiwa nyuma ya Rais John Magufuli aliyeshinda kwa kupata kura 8,882,935 (asilimia 58.46).“Watu wale zaidi ya milioni sita ndizo kura wanazokubali Tume ya Uchaguzi, watu wale zaidi ya milioni sita nawaambia nini? Nawaambia naondoka Chademakwa sababu gani? Kwa hoja gani?” alihoji.Lowassa ambaye ameshika nafasi mbalimbali katika serikali za awamu nne za mwanzo, alitoa matumaini zaidi kwa viongozi na wanachama wa Chadema. “Tumepigana pamoja,tunangojea kupangana kupiganapamoja kwenye uchaguzi ujao, anayesema ninataka kuondoka Chadema anajifurahisha, nataka kuwahakikisha wanachama wa Chadema na wananchi nipo Chadema na nitaendelea kuwa Chadema, naomba waendelee kuniunga mkono nikiwa Chadema,” alisema huku akirudia mara kwa mara kutaja jina la chama chake.Kusifiwa na viongozi CCMAlipoulizwa kuhusu viongozi wa CCM na Serikali kumsifu mara kwa mara, alisema, “Naacha wananchi wahukumu na wenyewe wahukumu, mimi naamini ni nia njema na nia njema itaendelea kuwepo.”Alipoulizwa haoni kama kusifiwahuko na viongozi wa CCM na Serikali kunaweza kutafsiriwa tofauti, alisema: “Anayetaka kufikiria hivyo ni hiyari yake, huwezi kumnyima binadamu kufikiria, ila ninachosema mimi sina mpango wa kuondoka Chadema.”Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amekuwa akimmwagiasifa Lowassa akimuelezea kuwa kiongozi mzalendo wa kweli, mstaarabu aliye tofauti na viongozi wengine wa upinzani.Hivi karibuni wakati akizindua maktaba ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais Magufuli alirudia tena sifa hizo, akisema Lowassani mwanasisasa mstaarabu ambaye baada ya kushindwa mbio za urais 2015 alikubali matokeo. Alimtaka awashauri watu anaowaongoza watulie, akisema la sivyo wataishia gerezani. Siku hiyo, Lowassa alimpongeza pia Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya.Julai mwaka huu, Rais Magufuli alikutana na viongozi wakuu wastaafu Ikulu Dar es Salaam, pia alitoa sifa kama hizo kwa Lowassa akimuita kuwa ni “mtu mwema sana” ambaye hakuwahikumtukana.Mwanzoni mwa wiki hii, sifa hizozilidakwa na katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally aliyesema Lowassa hana unafiki kwa sababu aliondoka ndani ya chama hicho baada ya kukosa ridhaa ya kugombea na kwenda chama kingine (Chadema) badala ya kubaki ndani kinafiki na kuwagawa wanachama.Sifa anazomwagiwa Lowassa naviongozi wakuu wa CCM zimekuwa zikiibua mijadala na wakati mwingine maswali, baadhi wakihisi kuwa chama hicho kinamhofia na wengine wakidhani jina lake linatumika kuwagawa wapinzani.Jambo hilo lilimfanya naibu katibu mkuu wa Chadema - Zanzibar, Mwalimu kumtaka Lowassa kujitokeza na kuweka msimamo wake hadharani.Lakini katibu mkuu wa Chadema,Dk Vincent Mashinji alisema anaamini CCM wanamtumia Lowassa kuwafarakanisha. Alisema (CCM) wanajua Lowassa ana nguvu kubwa akiwa upinzani kama ilivyoonekana kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita na ndiyo maana wanajaribu kumdhoofisha.Dk Mashinji alisema bado wanaendelea kumuamini Lowassa na yumo kwenye mipango yao.


Chanzo : Mwananchi
Mimi huwa nawashangaa sana watanzania,sijui ccm ilituroga kwa uchawi wa wapi? Watu badala ya kuhangaika na kuihoji ccm na Magufuli wao kwa namna walivyomtukana lowassa ile 2015 na leo watu wale wale wanakula U-turn ya nguvu,wao wanahangaika na Lowasa
Sometime nafeel bad kuchangia nchi moja na watu wa aina hii
 
Mtahangaika sana kuhamisha magoli lakini Membe kawashika makalio kisawasawa hadi mnaomba msaada kwa Team Lowasa. Membe ndiye mgombea wa CCM 2020 mtake msitake habari ndiyo hiyo.
Labda kama kuna CCM mbili
 
Lowassa amewapa makavu live, wana-CHADEMA wanaomchokonoa ili atoe neno. "Anayetaka kufikiria hivyo ni hiari yake..."
Bro c.musiba hvi kule jeshi ulikimbia au ulifukuzwa na nn au mafunzo yalikuwa magumu?na je unajua mzee lowassa jeshini alikuwa afande wako?Pia mh mbowe unajua amekulia jeshini au hujui sasa hao ndio wazalendo wa taifa la Tzania na wewe nimesahau uliamua kuacha na cheo gani vile? Wajanja wa mjini wanasema karibu majura musiba na viva cdm!!
 
Hakika sasa nimeamini kuwa Mh.Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa ni kiongozi anakumbuka Fadhira.Mh.Lowassa amekuwa anawakumbuka na kujisikia kukosa cha kuwambia wapiga kura wake za Urais kuwa kwanini anaondoka Chadema.Mh.Lowassa ana kiri kuwa wapiga kura walimwamini akiwa Chadema hivyo atabaki Chadema licha ya CCM kumtaka ahamie CCM.
 
Back
Top Bottom