Lowassa awakaanga vigogo Serikali ya JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa awakaanga vigogo Serikali ya JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 20, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 19 March 2012 21:40[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [​IMG]
  Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa​

  ASEMA WAMEKWAMA KUMALIZA TATIZO LA AJIRA, AWATAKA MAASKOFU WAINUSURU, RUWAICHI AIPONDA KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI

  Juma Mtanda, Ifakara

  WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa amesema anashangazwa na Serikali kuendelea kulifumbia macho tatizo la ajira kwa vijana na kuwaomba maaskofu wasaidie kulimaliza akisema hilo ni bomu linalosubiri kulipuka.

  Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akitoa salamu zake kwenye sherehe za uzinduzi wa jimbo jipya la Kanisa Katoliki la Ifakara zilizofanyika katika Viwanja vya Kanisa Kuu la Mtakatifu Edward, Ifakara.

  Alisema viongozi wa juu serikalini wameshindwa kulitatua na kulifumbia macho tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana hivyo kuwaomba maaskofu waliangalie kundi hilo ambalo linakabiliwa na changamoto nyingi.

  "Suala la ajira kwa vijana hakuna kiongozi anayelishughulikia ipasavyo ndani ya Serikali, hivyo niwaombe maaskofu nchini walione hili. Nawaomba katika miradi yenu mlipe kipaumbele suala la tatizo la ajira kwa vijana," alisema Lowassa na kuongeza:

  "Kanisa Katoliki limekuwa likisaidia sana katika sekta ya elimu na afya kwa hiyo sasa waelekeze nguvu hizo katika kusaidia ajira kwa vijana. Wengi wanaomaliza elimu ya sekondari na vyuo wanakabiliwa na tatizo kubwa la ajira. Hili kama tunavyosema ni bomu linalosubiri kulipuka, sasa naliomba Kanisa lisaidie juhudi za Serikali kutatua tatizo hili," alisema Lowassa huku akishangiliwa.

  Ruwaichi na mgomo
  Akizungumza katika sherehe hizo, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Yuda Dadeus Ruwaichi alisema mgomo wa madaktari nchini umedhihirisha udhaifu wa Serikali katika kushughulikia migogoro na kusema ni aibu kwa Tanzania.

  "Watu wengi wamekufa katika mgomo ule na hii imeonyesha Tanzania ni taifa lisilo na dira," alisema Askofu Ruwaichi huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda ambaye ni Mbunge wa Ulanga Mashariki akimsikiliza.

  "Hakuna hata uharaka uliochukuliwa kushughulikia mgomo ule na hii ni kwamba nchi yetu sasa imefikia pabaya kwani inaonekana imeshindwa kushughulikia matatizo," alisisitiza.

  Katika salamu hizo kwa Askofu mpya wa jimbo jipya la Ifakara, Salutaris Libena, Askofu Ruwaichi alisema kanisa litaendelea kupiga vita umasikini.

  Alimtaka askofu huyo kutoogopa kukemea maovu yanayofanywa na viongozi wa Serikali na kusababisha pengo kati ya wenye nacho na wasionacho.

  Mwinyi asisitiza upendo
  Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi alimtaka Askofu Libena kutumia nafasi yake kuleta amani na upendo miongoni mwa waumini wa dini mbalimbali.

  Mwinyi alisema uaskofu ni daraja kubwa linalofanana na nafasi ya uwaziri katika Serikali hivyo waumini wa dini ya Kikristo katika jimbo jipya la Ifakara wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kiongozi huyo aliyesimikwa kutumikia dini hiyo na Watanzania kwa ujumla.

  "Nafasi ya uaskofu haifungamani na dini wala kabila kwani daraja hilo limejaa roho ya huruma na upendo hivyo jamii ya jimbo la Ifakara ni wakati wa kutoa ushirikiano ili kumpa nafasi mhashamu Askofu Salutari Libena ya kuwahudumia katika nyanja mbalimbali za elimu, afya na tabia njema," alisema Mwinyi.

  Kadinali Pengo
  Katika mahubiri yake, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo alisema uamuzi wa kugawanya Jimbo la Mahenge ni mchakato wa muda mrefu uliotokana na ukubwa wa Jimbo la Mahenge.

  "Mchakato huo uliridhiwa na Papa Benedict wa 16 Januari 14, 2012 kwa kukubali Ifakara kuwa jimbo jipya na makao makuu katika Kanisa la St Andrew lililopo mji mdogo wa Ifakara.

  Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini na taasisi wakiwemo maaskofu wa majimbo 34.

  Wengine waliohudhuria sherehe hizo ni Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga na Kilombero, Francis Miti.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkiwa kwenye chungu kimoja huwezi kuwakaanga wenzako maana wote mtaungua!
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Nilidhani Lowassa hakualikwa kwenye hizo sherehe za kidini Ifakara; Rais Mwinyi alikuwepo lakini Lowassa alishambulia Vigogo wa CCM, sasa hapo ndipo anapotuchanganya

  Vigogo wa CCM ndio kina nani?
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Well, since politicians are people, and people have beliefs, it's pretty hard to separate politics and religion, people's attitudes and decisions will be affected by those beliefs. And I wouldn't want to, conscience is presumably a guide to ethical behaviour. That isn't really much of a danger. The real danger is vesting political and religious authority in the same people and institutions. A common feature of religious belief is a claim to be absolutely correct about certain things based on divine authority. It's a short and easy step from there to thinking you have both a right and a duty to interfere in the lives of people who disagree with you. That's a prescription for tyranny.


  Be careful of your kipima joto; be realistic make sure you do have facts and not a tool to create isolation and tyranny.
   
 5. w

  wikolo JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hili suala la ajira kwa vijana limekuwa linaongelewa sana na huyu mheshimiwa EL. Kuna mtu anayejua kama yeye alipokuwa kwenye nafasi yake ya PM aliwahi kufanya lolote juu ya tatizo hili? Sikumbuki kama alishawahi kuwasilisha japo hoja binafsi bungeni juu ya hili kwa kutumia nafasi yake ya ubunge. Yeye ni mbunge wa CCM na serikali ni ya CCM na kwa maana hiyo anatakiwa awe sehemu ya ufumbuzi wa tatizo hilo. Kama CCM imeshindwa kama anavyosema yeye (na kwa kweli ndo ukweli wenyewe), basi ina maana na yeye ameshindwa.Haiwezekani akakaa pembeni na kuanza kuwanyooshea wengine vidole kwani na yeye ni sehemu ya hao!!
   
 6. Z

  ZABANGA Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu analilia urais kwa udi na uvumba.ameamua kumwangukia YUDA.Mbona hata hawa wakatoliki wanatushangaza kuzidi kumpokea huyu mwizi?Anasema ajira mwanae FRED ana mamilioni kwanini asiseme ameyatoa wapi kwa umri mdogo kama huo?
   
 7. z

  zee la weza Senior Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Swala la ajira tumeshalichoka, hebu tunaomba azungumzie swala la ufisadi wa richmond, dowans na sasa simpion power
   
 8. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Wewe Lowasa unataka kumkasirisha mamba kabla hujavuka MTO? Hujui kwamba mkweo anakabiriwa uchaguzi wa ubunge. Na majaliwa yake yako kwa wateule wa Kikwete tume ya uchaguzi. Hivi JK akikasairika akanawa MIKONO mithili ya Pilato unafikiri SIOI atashinda bila msaada wa NEC?!

  Yale yale ya Wassira kutukanwa na Sendeke kwamba watu wa Mara wasiingilie mambo ya wana Arusha, na Wassira kwa pembeni anacheka kama ZUZU!
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  matukio-michuzi angalia EL anavyopunga mikono kila mara!
  Yaani ndoto za uraisi bado anazo!
   
 10. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Anajaribu kujitafutia mvuto kwa vijana kwa maneno ambayo yanapingana na vitendo vyake.
  Huyu mtu ni mnafki na hatari sana.
   
 11. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mimi namuheshimu jamaa huyu kama binadamu, hila njia yake ya kutuma ujumbe ndiyo inanitia wasi wasi sana. Yeye aliwahi kuwa Kiongozi mkuu msaidizi wa Raisi, aliwahi kusema JK ni mtu wake wa karibu walisoma wote na hawakuokotana BARABARANI. Sasa kama ndiyo hivyo kwa nini kama anataka kutoa ushauri aendi nyumbani kwa Mheshimiwa Jakaya wakashauliana in CAMERA bila kutafuta publicity STUNT, unaweza kukosoaje chama chako mbele ya kadamunasi na kibaya zaidi unazungumzia : A TIME BOMB yaani ajila kwa Vijana!!! wakati unajuwa majority wa Raia Tanzania ni Vijana, sasa hii inaleta taswila gani? Vijana wa-act au wa-react na kwa maslihi ya nani?

  Mtu ukiangalia kijuu juu unaweza kufikili hili nijambo la kawaida tu, si kweli tanapashwa kuwa makini sana katika matamshi yetu na timing - mtu ambaye alijuwana naye toka enzi za ujana wenu siyo vizuri ku-critise administration yake in Public, urafiki wenu uendelee na mmalize tafauti zenu kama zipo - kimya kimya.

  Unajulikana katika utendaji wako mahili kikazi "unquestionably non-nonsense human; lakini tukumbuke aliyowahi kusema the late J.Kambarage kwamba unapokuwa kiongozi, wakati mwingine husikilize watu wanao kwambia "mzee we endesha gari kilometa mia mbili kwa saa husipunguze mwendo kwenye mashimo wala kona husijali litakalo tokea" akasema kama kiongozi kwenye mashimo na kona hunatapunguza mwendo utaharibikiwa, katika maoni yangu naona JK alizingatia sana wosia wa mwalimu la sivyo saa hizi ingekuwa vurugu tupu kama angekuwa anatumia jazba au kutunishiana misuri - tuwe wangalifu jamani, amani NZURI.
   
 12. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani ni wakati mwafaka wa yeye kuwashughulikia walioko serikalini na ndani ya CCM maana wao walipata nafasi ya kumshughulikia wakashidwa! acha awakaange! Isipokuwa wananchi wa Tanzania hatuwezi kusahau ujio wa RICHMOND na DOWANS!
   
 13. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna watu humu janvini mlisrma lowasa hakualikwa haya sasa oneni aibu
   
 14. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umenena yaliyo mema, yeye kila siku ajenda hiyo hiyo hana nyingine?
   
 15. B

  Baba advent Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 70
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Hivi ninyi mnae mwalika E.Lowasa mnamwalika kama nani? Maana siyo waziri, siyo mbunge wenu,kanisa acha ufitini,simamieni amani nchini.Hamna hata aibu kuripoti habari za Lowasa kilombero.
   
 16. m

  mzizi dawa Senior Member

  #16
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aache unafiki uyo,vijana wa Monduli wame chaka,awana lolo ye anagawa pesa makanisani,akati kuna jirani zake pale ngarashi awapati mlo mmoja,Alafu tunaambiwa ametubu,Je ame waambia watanzia amewaibia na je amerejesha pesa zawavuja jasho?
   
 17. m

  mharakati JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ajira bomu kwa vijana kwa nini asitumie baadhi ya utajiri wake kuwekeza kwenye mambo ya msingi hapa na kuwapa hao vijana ajira..kiongozi unaongoza kwa mifano na kwa mstari wa mbele..aongee na wenzake akina chenge waanzishe tuviwanda tuwili tutatu huku wakijairi vijana ndiyo aanze kupiga hizi singo za ajira na bomu la taifa...
   
 18. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hujajianda wewe na hujui unataka kusema nini..suala la Richmond si lilishahitimishwa na Pinda kuwa limekwisha sasa unataka kujadili nini?
   
 19. K

  Kuchayaa Senior Member

  #19
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  As longer as this generation exists Lowesa will never live to see himself the pricident of this country & that will always be the truth!
   
 20. K

  Kuchayaa Senior Member

  #20
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  As longer as this generation exist Lowasa will never live to see himself the precident of this country, & tht will always be the truth!
   
Loading...