Lowassa atoa neno kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,411
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amewatakia mfungo mwema wa Ramadhani Waislamu wote akiwaomba kutumia ibada zao kuwaombea viongozi wa nchi hekima na busara na kuombea nchi amani na utulivu.

Waumini hao wanatarajiwa kuanza mfungo mtukufu wa Ramadhani Jumamosi baada ya mwezi kuandama.

Lowassa amesema kuanza kwa mfungo huo ni kutekeleza moja ya ibada zao muhimu kwa waumini hao.

“Ni kipindi ambacho Waislamu wanatakiwa kutenda mema zaidi na kuwa karibu zaidi na mwenyezi Mungu kwani malipo katika mwezi huu ni mara dufu zaidi ya miezi mingine.”

“Nachukua nafasi hii kuwatakia ndugu zangu Waislamu mfungo mwema katika mwezi huo mtukufu wa Ramadhani, na kuwaomba wafanyabiashara kutopandisha bei za vyakula katika mwezi. Pia nawaomba ndugu zetu akristo na wa dini nyingine kuwa na ushirikiano na wenzao kama ilivyo desturi yetu, ili watimize ibada hii muhimu kwao.”

“Kwa wale wenye uwezo tuwasaidie wenzetu wasiyokuwa nao na pia katika ibada zetu tuiombee nchi yetu amani na utulivu na pia kuomba hekim
 
Tunashukuru, asante mzee!

image.png
 
Aliahidi angepeleka chakula kule Kagera kwa wahanga vipi alienda kuwasaidia..?
Halafu unaposema "Mstaafu" alistaafu lini huo uwazir mkuu..?
 
Kwa kila Mtz ni muhimu kuonyesha upendo kwa mwenzie na bila shaka Lowasa ameona hivyo.
 
Lakini ingekuwa vema aje atolee ufafanuzi au kauli japo kwa ufupi juu ya hili sakata la mchanga wa dhahabu ambao muheshimiwa Rais ameweza kuwatumbua hawa jamaa wa Acacia mining waliokuwa wanatuibia mali zetu kila uchao kwa kutuzuga kuwa wanatekeleza mkataba ambao tuliingia nao.
 
Back
Top Bottom