Lowassa atinga Muhimbili kumjulia hali Ester Bulaya

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,699
Reaction score
2,260
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mh. Edward Lowassa amefika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar kumjulia hali Mbunge Ester Amos Bulaya.

Lowassa.jpg

========

Dar es Salaam. Hali ya Mbunge wa Bunda Ester Bulaya aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH ) inaendelea vizuri baada ya kuanza kupatiwa matibabu jana.

Bulaya ambaye alipata tatizo la kupumua baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya Kituo cha Kati cha Polisi mjini Tarime, alifikishwa hospitalini hapo juzi usiku na kulazwa katika wodi namba 18 Sewahaji.

Akizungumza Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, John Stephen alisema leo Bulaya amepata ahueni kiafya na anaendelea vizuri na matibabu.

"Sasa ameanza kujihudumia mwenyewe, anakula vizuri na bado anaendelea na matibabu," amesema Stephen huku akisisitiza kuwa mgonjwa bado anahitaji utulivu kwa kipindi hiki.

Bulaya amesota rumande tangu akamatwe Ijumaa ya Agosti 18 kwa madai ya kuingia jimbo la Tarime na kufanya shughuli za kisiasa kwa kutoa msaada wa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi jimboni humo baada ya kualikwa na mbunge mwenzake Ester Matiko

Chanzo: Mwananchi
 
Sitaki kusikia ujinga ujinga wa kinafiki wa viongozi wa dini kuwa eti bwana yule aombewe sana, Mimi nasema acheni ajiombee mwenyewe shetani mkubwa! Watu wanateseka kwa kutimiza wajibu wao kama raia wa nchi hii halafu jitu lililolewa madaraka linatesa raia wema pasipokuwa na kosa lolote
 
Bila shaka fahamu zitawajia kuwa kule ndani sio kuzuri, wala sio sifa kupelekwa kule.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Mh. Edward Lowassa amefika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar kumjulia hali Mbunge Ester Amos Bulaya.

View attachment 573279

========

Dar es Salaam. Hali ya Mbunge wa Bunda Ester Bulaya aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH ) inaendelea vizuri baada ya kuanza kupatiwa matibabu jana.

Bulaya ambaye alipata tatizo la kupumua baada ya kuzidiwa akiwa mahabusu ya Kituo cha Kati cha Polisi mjini Tarime, alifikishwa hospitalini hapo juzi usiku na kulazwa katika wodi namba 18 Sewahaji.

Akizungumza Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, John Stephen alisema leo Bulaya amepata ahueni kiafya na anaendelea vizuri na matibabu.

"Sasa ameanza kujihudumia mwenyewe, anakula vizuri na bado anaendelea na matibabu," amesema Stephen huku akisisitiza kuwa mgonjwa bado anahitaji utulivu kwa kipindi hiki.

Bulaya amesota rumande tangu akamatwe Ijumaa ya Agosti 18 kwa madai ya kuingia jimbo la Tarime na kufanya shughuli za kisiasa kwa kutoa msaada wa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi jimboni humo baada ya kualikwa na mbunge mwenzake Ester Matiko

Chanzo: Mwananchi
Hiyo mifuko hamsini ya simenti itatumika kama ushahidi wa kesi ya uchochezi.
 
Hizi janjajanja, sero sikumbili ndo anakonda hivo?
 
Huyu mzee wa ajabu sana, wagonjwa woote hao kamwona ester tu?
 
Back
Top Bottom