VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Mwanasiasa Edward N. Lowassa anapigiwa upatu wa kutosha kupeperusha bendera ya Urais wa CCM yetu. Akisaidiwa na ukwasi wake,Lowassa amewekeza kwenye media na kwingineko kutimiza lengo lake hilo. Amegusa hata makanisani na misikitini.Lowassa anasifiwa na wapigadebe wake kama mbunifu wa Shule za Sekondari za Kata na Mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Viktoria.
Kwa hali ya shule za Sekondari za kata, Lowassa ataangushwa na jambo hili. Shule hazina walimu wa kutosha, maabara, vifaa vya kufundishia na kadhalika. Ziko hohehahe. Taabani kwelikweli. Si jambo la kujivunia na kulitumia kama jambo jema la kubuniwa naye. Jambo hili la shule za kata linamwonesha Lowassa kama mkurupukaji anayejali wingi badala ya ubora;ukubwa badala ya uzuri.
Kama yeye ndiye hasa mbunifu,ubunfu wake umeshindwa vibaya. Kuhusu mradi wa maji Ziwa Viktoria, kuna mvutano juuya nani hasa ni muasisi kati ya Lowassa na Diallo na wenzake. Vyovyote iwavyo,mradi huo nao umeshinwa vibaya na kuonesha ukurupukaji pamoja na kutokuwa na malengo na mipango kwa mwanzilishi. Hapa pia ataanguka na kuangushwa kwa hoj hii.
Karata yake ya maamuzi magumu ndiyo haina mashiko kabisa. Upi uamuzi mgumu aliowahi kuufanya Lowassa? Hivi kujiuzulu kwa kashfa aliyohusishwa nayo ni uamuzi mgumu? Si kweli hata kidogo.
Nchi inamhitaji Rais mwenye hekima,busara,uwezo,msafi,mwenye mipangodira, mkweli na muamuzi. Lowassa hatoshi. Tanzania haitaji tu wa aina ya Lowassa. Atasubiri sana!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam