Lowassa ataangushwa na haya mambo

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,065
2,000
Mwanasiasa Edward N. Lowassa anapigiwa upatu wa kutosha kupeperusha bendera ya Urais wa CCM yetu. Akisaidiwa na ukwasi wake,Lowassa amewekeza kwenye media na kwingineko kutimiza lengo lake hilo. Amegusa hata makanisani na misikitini.Lowassa anasifiwa na wapigadebe wake kama mbunifu wa Shule za Sekondari za Kata na Mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Viktoria.

Kwa hali ya shule za Sekondari za kata, Lowassa ataangushwa na jambo hili. Shule hazina walimu wa kutosha, maabara, vifaa vya kufundishia na kadhalika. Ziko hohehahe. Taabani kwelikweli. Si jambo la kujivunia na kulitumia kama jambo jema la kubuniwa naye. Jambo hili la shule za kata linamwonesha Lowassa kama mkurupukaji anayejali wingi badala ya ubora;ukubwa badala ya uzuri.

Kama yeye ndiye hasa mbunifu,ubunfu wake umeshindwa vibaya. Kuhusu mradi wa maji Ziwa Viktoria, kuna mvutano juuya nani hasa ni muasisi kati ya Lowassa na Diallo na wenzake. Vyovyote iwavyo,mradi huo nao umeshinwa vibaya na kuonesha ukurupukaji pamoja na kutokuwa na malengo na mipango kwa mwanzilishi. Hapa pia ataanguka na kuangushwa kwa hoj hii.

Karata yake ya maamuzi magumu ndiyo haina mashiko kabisa. Upi uamuzi mgumu aliowahi kuufanya Lowassa? Hivi kujiuzulu kwa kashfa aliyohusishwa nayo ni uamuzi mgumu? Si kweli hata kidogo.

Nchi inamhitaji Rais mwenye hekima,busara,uwezo,msafi,mwenye mipangodira, mkweli na muamuzi. Lowassa hatoshi. Tanzania haitaji tu wa aina ya Lowassa. Atasubiri sana!


Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Sep 8, 2014
3,311
2,000
Pamoja na kwamba mimi ni UKAWA damu damu ila lazima niseme neon hapa, Lengo la Lowassa kuanzisha shule za kata lilikuwa zuri sana na usimhukumu Lowassa kuwa shule hizo za kata zimeshindwa eti hazina walimu, vitabu, kumbuka kuwa Lowassa baada ya kutoka alikosa mamlaka ya kuamua chochote juu ya hili, kwa hiyo ilitegemewa Pinda ndiye asimamie, kamwe haitatokea eti pinda aje aseme kuwa "yeye hakuzianzisha hizo shule" utakuwa ni ujinga na upunguani mkubwa na atakuwa hana akili timamu.

hili la maji bado namtetea Lowassa, hivi jiulize, kwa katiba ya Tanzania, naibu waziri haingii ktk baraza la mawaziri ss ni lini Diallo akiwa Naibu waziri aliwasilisha mbele ya cabnet proposal hii?
 

Gracious

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
1,837
2,000
Point of correction;

Aliyeanzisha shule za kata sio serikali ya kikwete ni serikali ya Mkapa.

Lowassa alikuta hilo jambo liko tayari kabisa katika utekelezaji

Ni mkapa aliyetafuta pesa na kuleta hilo wazo na misingi ya utekelezaji wake.

Ni mkapa aliyeanza na program ya MMEM-Mpango wa maendeleo elimu ya Msingi...akaukamilisha

Ni mkapa aliyepanga program ya MMES-Mpango wa maendeleo elimu ya sekondari ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2005/2006.

Huu upotoshaji mkubwa unaofanywa kwamba MMES ni wazo la Lowassa unatakiwa ukemewe
 

samora10

JF-Expert Member
Jul 21, 2010
7,512
2,000
Kwa hiyo tumhukumu yeye kwa shule kukosa walimu na mazingira bora..? Je plan yake ilikua kuzijenga tu? leteni plan yote kwanza tuisome, inawezekana angekuwepo madarakani angaekua ameendelea na plan ya maboresho kuanzia walimu hadi vitendea kazi na tusingekua tunachangishwa hela za mabaara kama tunavyoanyiwa sasa..
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Kwa sasa ccm kuendelea kupigia debe itoe mgombea wa urais ni kuendelea kuinajisi ikulu yetu!
 

NDAGLA

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
2,486
1,500

We mwenyewe umekurupuka na hoja zenye makengeza.

Soma comment ya jenerali ambamba hapo juu.

Kama kuachia ngazi siyo maamuzi magumu muulize Werema na wenzake kwa nini hawataki kujiuzuru.

Katika siasa za Afrika kuwajibika ni maamuzi magumu.
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom