Lowassa asema ili kuwaendeleza wafugaji tanzania itakuwa na viwanda 10 vya kusindika

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
681
126
Lowassa asema ili kuwaendeleza wafugaji tanzania itakuwa na viwanda 10 vya kusindika nyama

Lowassa asema ili kuwaendeleza wafugaji tanzania itakuwa na viwanda 10 vya kusindika nyama
By Irene K. Bwire | Published 10/4/2007 | Habari Mpya | Unrated


WAZIRI Mkuu Edward Lowassa amesema Tanzania inatarajia kuwa na viwanda kumi vya kusindika nyama nchini katika miaka mitatu ijayo ili kuinua kipato cha wafugaji.

Akifungua mkutano wa viongozi wa kimila wa kabila la Wamasai mjini Arusha leo (Alhamisi Okt. 4, 2007) Lowassa alisema viwanda hivyo pia vitaendeleza ufugaji nchini.

Wafugaji wengi nchini hivi sasa wanachunga tu mifugo na hawafugi kisasa na hivyo wanashindwa kupata maendeleo kutokana na mifugo yao kama ilivyo kwa mazao ya wakulima, alisema.

"Kama wakulima wanavuna kahawa kwa nini wafugaji wasivune mifugo? Kama wakulima wanavuna pamba, kwa nini wafugaje wasivune mifugo," alisema.

Tangu kufungwa kwa kiwanda cha Tanganyika Packers cha Dar es Salaam miaka kadhaa iliyopita, Tanzani haina kiwanda kikubwa cha kusindika nyama. Kuna viwanda kadhaa vinakamilishwa hivi sasa katika mikoa ya Shinyanga, Rukwa na Arusha.

Kutokana na kutokuwa na viwanda vya kutosha vya usindikaji nyama, baadhi ya wafugaji na wafanyabiashara wengine wanasafirisha nje wanyama wazima hasa nchi za Komoro na Arabuni.

Tanzania ni ya tatu katika Afrika, baada ya Sudan na Ethiopia, kwa kuwa na mifugo ya ng'ombe, mbuzi na kondoo.

Waziri Mkuu alisema kuwa kutokana na mifugo kushindwa kuhimili mahitaji ya kiuchumi ya wafugaji, ndiyo maana vijana wa wafugaji wa kabila la Kimasai wanakimbilia mijini kufanya kazi za ulinzi wa usiku.

"Wamasai sasa wametapakaa Dar es Salaam na Zanzibar; Nairobi, Kenya; Kampala, Uganda na katika miji mingine kufanya kazi za ulinzi wa usiku…tuwasaidie hawa waachane na kazi hii isiyo na tija," alisema.

Lowassa alisema njia nzuri ya kuondokana na hali hiyo ni kuendeleza elimu ili wafugaji hao wawe bora zaidi na waingie katika mfumo wa uchumi wa kawaida.

Alisema wale waliopewa "rungu" kuongoza wawaongoze watu wao kwa kuhakikisha wanapata elimu. Katika mila za Kimasai, kiongozi hukabidhiwa rungu.

Waziri Mkuu aliwataka wafugaji kote nchini wawe wafugaji wa kweli kwa kunenepesha mifugo yao na kuiuza ndani na nje na siyo kuwa wachungaji kwa kuzunguka nchi nzima kutafuta malisho.

"Hamuwezi kuzunguka na kusambaa nchi nzima kutafuta malisho. Hamtakiwi kuigeuza Tanzania yote kuwa ni eneo la malisho," alisema.

Mkutano huo wa viongozi wa kimila ulikuwa ni sehemu ya shughuli za Waziri Mkuu katika ziara yake ya siku mbili ya mkoa wa Arusha. Jana (Jumatano Okt. 3) alitembelea wilaya ya Monduli ambako alikagua shule, bwawa la maji na na kuzungumza na vijana waliokuwa katika Kambikazi ya kimataifa kabla ya kufuturu na waumini wa Kiislamu wanaofunga mfungo wa Ramadhani katika futari aliyowandalia katika mji mdogo wa Mto wa Mbu.

http://www.jakayakikwete.com/tanzan...-na-viwanda-10-vya-kusindika-nyama/Page1.html
 
Kisa tu nimemsema Lowassa? Sina chuki wala ugomvi nae, ila kwa madhambi aliyoyatenda akiwa CCM wacha tu akutane na dola.
Ukipanda mahindi huwezi kuvuna chips
Lakini yeye alikuwa anapata ujumbe toka juu kwa Rias think like great thinker


Swissme
 
Back
Top Bottom