Lowassa apotezwa

Lowassa apotezwa

salimkabora

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2012
Posts
2,441
Reaction score
653
SIKU KADHAA NYUMA NILISEMA HIVI:
Kwa maoni yangu midahalo ya wagombea haionyeshi kama itaisaida sana UKAWA kwa kuzingatia kwamba mazingira sio rafiki sana. Kwa tathmini yangu, Lowassa hatajiongezea idadi yoyote ya kura kwa njia ya midahalo; midahalo inaendeshwa na walionacho ambao tayari wameshajipambanua kuulinda mfumo uliopo ili waendelee kufaidi keki ya taifa kwa upendeleo.
Yaliyofanywa na twaweza ndio yatakayofanywa katika midahalo ku discredit upinzani na wala hakuna lofa atakayenufaika na midahalo hiyo inayoandaliwa kuwaumiza. Lowassa akitaka midahalo akaongee kwenye vyombo vya habari vya nje ya nchi sio hivi vinavyojulikana wazi vinampromote nani. Bali ni muhimu sana UKAWA kuanza kutumia vyombo vya habari kwa nguvu zote kwa kuwa dunia inasikiliza vyombo vya habari na sio yanayosemwa kwenye majukwaa ya kampeni. Kimahesabu nikichukulia majukwaa ya kampeni kuchangia asilimia 50 na vyombo vya habari asilimia 50 napata taswira hii: Kukubalika majukwaani UKAWA 25% CCM 20% WENGINEO 5 (% ) Kampeni vyombo vya habari: UKAWA 4% CCM 45% WENGINEO 1 (%) JUMLA : UKAWA 29% CCM 65% WENGINEO 6%
Nikichukulia kwamba Lowassa anakubalika na wapiga kura kwa asilimia 60 na magufuli aslimia 40 na pia kwamba ccm imechokwa kwa asilimia 70 napata wastani wa kukubalika upinzani sawa na asilimia 65 yaani wastani wa 60% na 70%; Nikikokotoa hapo napata ushindi kwa Lowassa 54% (sawa na 29x65/35) na Magufuli 40%. Ushindi huu ni kiduchu sana na unaweza kupinduliwa. Lakini iwapo UKAWA wangeshambulia kwenye vyombo vya habari na angalau kusogeza asilimia toka 4 hadi 15 matokeo yangekuwa ya uhakika zaidi kama ifuatavyo: Lowassa 74% (sawa na 40x65/35) na Magufuli 20%. Ushindi huu kuupora ni kazi.

LEO NASEMA HIVI:
Kwa sasa kampeni za majukwaan za ccmi zimeipiku Ukawa na kufikia 23% toka asilimia 20 ya awali na pia kampeni zao kwenye vyombo vya habari zimepaa hadi asilimia 48; kwa maana hii Ukawa wamepoteza alama muhimu 11 (yaani 6x65/35) na hivyo kuangukia pua toka 54% hadi 43% leo hii. Tukichukulia kwamba nyomi za ccm hazina uhalisia kwa asilimia 5 (kutokana na wahudhuriaji kupewa vishawishi na wengine kuhofia kupoteza ajira zao) Ukawa wanapata ahueni kidogo na kulalia asilimia 52.5 (yaani 43x55/45). Hapo nimechukulia kwamba bado Lowassa ana asilimia 20 za kukubalika zaidi ya Magufuli. Asilimia hii ni rahisi kushuka chini zaidi hata ya asilimia 5 ambapo tutaikuta Ukawa ikiendelea kugaagaa kwenye 43%. Kwa muktadha huu muujiza pekee wa kuifanya Ukawa ishinde ni kubadili muelekeo wa kampeni zake kwa kiwango kikubwa hasa kujihakikishia haikosi dominance ya vyombo vya habari kwa angalau 15% toka asilimia moja ya sasa.

SURA YA MATOKEO:
CCM imejipanga kwa asilimia 80; hii inapungua hadi asilimia 65.5 (yaani 80x45/55) kutokana na nyomi za kuchonga na hii nayo inapungua zaidi hadi 53.6% (yaani 65.5x45/55) kutokana na mgombea wake kuzidiwa umaarufu kwa alama 10 na Lowassa. Kwa vyovyote, haya ndio yatakuwa matokea ya mwisho wa siku iwapo Ukawa hawatajipanga upya na kupunguza ile asilimia 80 ya ccm inayotokana na harakati za usiku na mchana, kuvuruga wapinzani, kutumia turufu ya uwepo madarakani, kutamalaki kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii , n.k : Wafanye hivyo kwa kujipatia angalau alama 10 au zaidi kwenye vyombo vya habari, INGAWA TUNAWAJUA NI WATU WENYE SHINGO NGUMU KUPOKEA USHAURI LAKINI NI WAZI WASIPOFANYA HIVYO USHINDI KWAO NI NDOTO YA MCHANA. Mtaambulia hiyo 40.4% pekee.
 
Pumba tupu, CCM ushindi upo palepale kwa zaidi ya 70%

Toa hoja acha mapovu; linganisha kwanza tathmini yangu hapo juu ambayo ndiyo hiyohiyo waliyokuja nayo watafiti wa TADIP. Tunaongea namba sio porojo kama namba zinakupiga chenga nyamaza.
 
Peleka porojo zako ufipa.

Ikiwa wameshindwa vyombo vya habari vya ndani wataweza vya nje?

Mdahalo Lowassa hawezi kwa kuwa ni mgonjwa hawezi kuongea zaidi ya dakika kumi, hawezi kusimama muda mrefu na kwenye mdahalo tuaka wagombea wasimame na kujibu hoja kwa masaa matatu.

Si umeona midahalo ya USA?

Bado ninawashangaa sana Watanzania wanaotaka mgonjwa walikuwa wanamnadi kama fisadi aende Ikulu.
 
Tatizo moja ulilolifanya ni kusahau kwamba wakàti Ukawa wanapanga hayo eti CCM wao hawatakuwa wanafanya chochpte cha kureverse hizo anticipations zako ..umeliwa na hata iende irudi coma la Ukawa halitavuka hata 30% kwasababu kadiri Sikh zinavyokwenda lkuna ukweli ambao haupingiki kwamba 1. kambi ya Lowassa inahamwa kwasababu ya kambi kugundua haiwezi kupenya na 2. wale waliokuwa neutral wengi wao wanaopt kwa JJP Magufuri, hivyo basi tuchukulie Ukawa wanatumia media na hizi sabau mbili zinaenda simultaneously, bado kura za Ukawa zinacheza kwenye 20-25% na za JJP Magufuri zinapanda hadi 70% ..na 5% ni share ya ACT na zitakazopotea ..haya ndo matokeo ya mwisho.
 
Mbona hamsemi wanaohama kwenu hala mwenye clip yoyote watu wakisomba ukawa watume ila zipo nyingi za mafusiemu halamnasenma eti………… toeni ushuzi wenu hapaaa
 
Mimi nimetoa namba na wasomi TADIP wameibuka na namba hizohizo wewe unakuja na porojo sijui hapo nani aonekane hazimtoshi. Toa namba sio majungu uchaguzi ni sayansi; onyesha figures jinsi ugonjwa unavyoathiri umaarufu wa Lowassa au jinsi mdahalo unavyochangia ushindi na kwa asilimia ngapi halafu uje na hitimisho; hapa sio gest
 
Tatizo moja ulilolifanya ni kusahau kwamba wakàti Ukawa wanapanga hayo eti CCM wao hawatakuwa wanafanya chochpte cha kureverse hizo anticipations zako ..umeliwa na hata iende irudi coma la Ukawa halitavuka hata 30% kwasababu kadiri Sikh zinavyokwenda lkuna ukweli ambao haupingiki kwamba 1. kambi ya Lowassa inahamwa kwasababu ya kambi kugundua haiwezi kupenya na 2. wale waliokuwa neutral wengi wao wanaopt kwa JJP Magufuri, hivyo basi tuchukulie Ukawa wanatumia media na hizi sabau mbili zinaenda simultaneously, bado kura za Ukawa zinacheza kwenye 20-25% na za JJP Magufuri zinapanda hadi 70% ..na 5% ni share ya ACT na zitakazopotea ..haya ndo matokeo ya mwisho.

Unaongea udhaifu wa fikra zako; hakuna namba zinazoelea hewani kihivyo. Fikiria kwanza ni kwa vipi nilichokiandika kabla kikathibitika na utafiti wa TADIP kama kilivyo? suala hapa ni vyombo vya habari: kuna zaidi ya watu milioni kumi wanafatilia uchaguzi kwenye vyombo vya habari tofauti na hizo nyomi za watu elfu mbili au tatu kwenye mikutano ya kampeni. CCM inanufaika sana na hiyo nyomi ya mamilioni ya vyombo vya habari ndio mana nimeonyesha umaarufu wa Magufuli tayari umeshaanza kuimega ile asilimia 20 ya Lowassa na kuifanya 10 na bado mambo ni mwendo mdundo kiasi kwamba kama jamaa hawasituki hata hiyo kumi itapotea na kuishia huko kwenye 30 au chini zaidi. Tatizo hamtaki kuelewa hoja mnakurupuka kama mgombea wenu na mna mihemko
 
Mbona hamsemi wanaohama kwenu hala mwenye clip yoyote watu wakisomba ukawa watume ila zipo nyingi za mafusiemu halamnasenma eti………… toeni ushuzi wenu hapaaa

Endelea hivyo hivyo.
Wala hakuna haja ya kukushtua mpaka Oct 26.
Unadhani yaliyofanyika kwenye uzinduzi wa kampeni jangwani ni siri.
Na unadhani yaliyofanyika mwanza wakati wa kuwapokea lembeli na bulaya ni siri pia.
Tulia hivyo hivyo huku ukicheka cheka
 
SIKU KADHAA NYUMA NILISEMA HIVI:

SURA YA MATOKEO:
CCM imejipanga kwa asilimia 80; hii inapungua hadi asilimia 65.5 (yaani 80x45/55) kutokana na nyomi za kuchonga na hii nayo inapungua zaidi hadi 53.6% (yaani 65.5x45/55) kutokana na mgombea wake kuzidiwa umaarufu kwa alama 10 na Lowassa. Kwa vyovyote, haya ndio yatakuwa matokea ya mwisho wa siku iwapo Ukawa hawatajipanga upya na kupunguza ile asilimia 80 ya ccm inayotokana na harakati za usiku na mchana, kuvuruga wapinzani, kutumia turufu ya uwepo madarakani, kutamalaki kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii , n.k : Wafanye hivyo kwa kujipatia angalau alama 10 au zaidi kwenye vyombo vya habari, INGAWA TUNAWAJUA NI WATU WENYE SHINGO NGUMU KUPOKEA USHAURI LAKINI NI WAZI WASIPOFANYA HIVYO USHINDI KWAO NI NDOTO YA MCHANA. Mtaambulia hiyo 40.4% pekee.

View attachment 291324

View attachment 291339

CCM Kadi 02.jpg

CCM Kadi 03.jpg

Mwaka wao huu wataisoma namba na FIESTA YAO

Leo ukimuuliza NAPE NNAUYE kuwa ana jumla ya wanachama wangapi atakuambia kuwa ni zaidi ya Milion 6!!!!!!

Mmekwisha mwaka huu
 
Unaongea udhaifu wa fikra zako; hakuna namba zinazoelea hewani kihivyo. Fikiria kwanza ni kwa vipi nilichokiandika kabla kikathibitika na utafiti wa TADIP kama kilivyo? suala hapa ni vyombo vya habari: kuna zaidi ya watu milioni kumi wanafatilia uchaguzi kwenye vyombo vya habari tofauti na hizo nyomi za watu elfu mbili au tatu kwenye mikutano ya kampeni. CCM inanufaika sana na hiyo nyomi ya mamilioni ya vyombo vya habari ndio mana nimeonyesha umaarufu wa Magufuli tayari umeshaanza kuimega ile asilimia 20 ya Lowassa na kuifanya 10 na bado mambo ni mwendo mdundo kiasi kwamba kama jamaa hawasituki hata hiyo kumi itapotea na kuishia huko kwenye 30 au chini zaidi. Tatizo hamtaki kuelewa hoja mnakurupuka kama mgombea wenu na mna mihemko

Sidhani kama mie na wewe tunapingana kwasababu mie pie nimeweka data katika kuonesha mambo yanavyomnyookea Magufuri, kama ni waingereza basi ningesema nimekuwa pro-Magufuri na nimeeleza vivyo hivyo kwamba yawezekana kabisa na ndo uharisia kwamba mwisho matokeo ya Ukawa yatakuwa yanacheza kwenye 20-25% ..ova.
 
Wananchi bado wanakumbuka ahadi za CCM kupitia kwa Kikwete!!Mnatumia nguvu ku "Magufulika" wakati wananchi wanahitaji majibu ya "ahadi" hizi za CCM tokea 2010..Ndugu zangu,Tafiti za Twawezwa na Ipsos zisitutoe katika "Mstari" wa kutafakari "AHADI" za CCM za mwaka 2010 na Zile mpya za John Magufuli kama zisizotekelezeka.Ukitaka kujua kama Magufuli atatekeleza ahadi zake ANGALIA kama CCM ya Kikwete ilitekeleza walichowaahidi WATANZANIA wanaowaita "Wapumbavu,Malofa,Mbumbumbu na Kunguni kwa kuwa tu wepesi KUSAHAU!!!Kwa kuwa ninyi mpo sehemu mbalimbali TANZANIA thibitisha kama ahadi hiyo imetekelezwa ama kuna ahadi aliahidi sijaiweka hapa na HAIJATEKELEZWA!!!!
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora (HAJATEKELEZA)
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini (HAJATEKELEZA)
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria- Igunga (HAJATEKELEZA)
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga (HAJATEKELEZA)
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma (HAJATEKELEZA)
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini (HAJATEKELEZA)
7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma (HAJATEKELEZA)
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera (HAJATEKELEZA)
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi- Kagera (HAJATEKELEZA)
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba- Bukoba Mjini (HAJATEKELEZA)
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini (HAJATEKELEZA)
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera (HAJATEKELEZA)
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera (HAJATEKELEZA)
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu- Kagera (HAINA MENO KABISA NA IMEJAA RUSHWA)
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya (MAUAJI YANAENDELEA)
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba- Kagera (HAJATEKELEZA NA ZILIZOPO MBOVU HAZIFAI)
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali (HAJATEKELEZA)
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika- Mwanza (HAJATEKELEZA NAVYAMA VILIVYOPO VINA HALI MBAYA NA VINGI VIMEKUFA KABISA)
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza (HAJATEKELEZA)
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita (
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote- Pemba (KERO HAZIJATATULIWA)
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro (HAJATEKELEZA)
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa- Mbeya mjini (HAJATEKELEZA)
24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa (HAJATEKELEZA)
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea (HAJATEKELEZA NA WALIMU WAMEPUUZWA WANAULIZA -SHEMEJI UNATUACHAJE?)
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya (HAJATEKELEZA)
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga (HAJATEKELEZA)
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa (HAJATEKELEZA)
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro (HAJATEKELEZA)
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini (HAJATEKELEZA)
31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora (HAJATEKELEZA)
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu (AMETEKELEZA)
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini (HAJATEKELEZA)
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)- Hydom Manyara (HAJATEKELEZA)
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa-Musoma (HAJATEKELEZA CCM NDIO CHANZO CHA CHOKOCHOKO)
36. Kulinda haki za walemavu- Makete (HAJATEKELEZA,WANATUMIKA KWENYE KAMPENI TU)
37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini (HAJATEKELEZA)
38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha (HAJATEKELEZA)
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini (HAJATEKELEZA)
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni- Kigoma– Kaliua,Tabora (HAJATEKELEZA)
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi- Arusha Mjini (ANGALAU JAPO KIWANGO HAKIRIDHISHI)
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma (HAJATEKELEZA)
43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido (HAJATEKELEZA)
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga (HAJATEKELEZA)
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu 2010 mkoani Arusha – Arusha mjini (HAJATEKELEZA NCHI IPO GIZANI KWA MGAO AMBAO HAUJATANGAZWA)
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo- Busekera, Wilaya ya Musoma, . (HAJATEKELEZA)
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido (HAJATEKELEZA)
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti – Ngorongoro (HAJATEKELEZA)
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara (HAJATEKELEZA)
50. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini (HAJATEKELEZA)
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa (HAJATEKELEZA NA HALI NI MBAYA SANA)
52. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
53. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania- Iringa (HAJATEKELEZA)
54. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda (HAJATEKELEZA - CHOKOCHOKO ZA CCM ZINAHATARISHA AMANI)
55. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara (HAJATEKELEZA)
56. Kuwapa wanawake nafasi zaidi- Kilolo ,Iringa (ANGALAU)
57. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar (HAJATEKELEZA)
58. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa- Kabandamaiti mjini Zanzibar (HAJATEKELEZA)
59. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti (HAJATEKELEZA)
60. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma (HAJATEKELEZA)
61. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma (HAJATEKELEZA)
62. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma (HAJATEKELEZA)
61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma (MISAADA YA VYANDARUA NA VYOO KWA MSAADA WA WATU WA MAREKANI)
62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam (HAJATEKELEZA)
63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara (HAJATEKELEZA)
64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha (HAJATEKELEZA)
65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa- Kibaha. (HAJATEKELEZA)
66.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha (HAJATEKELEZA) N.K
CCM HAIAMINIKI TENA,WAKATI UMEFIKA CCM INAPASWA ITOLEWE KWA NJIA YA KURA MADARAKANI?..KWA NINI WASITEKELEZE AHADI HIZI KABLA YA KUAHIDI ZINGINE?....CHAGUA LOWASSA..CHAGUA UKAWA (CHADEMA/CUF/NLD/NCCR MAGEUZI)
 
Back
Top Bottom