Lowassa anaweweseka tu

Lowassa anaweweseka tu

LIKUYU SEKA

Member
Joined
Nov 15, 2013
Posts
53
Reaction score
24
Na Saed Kubenea

WAZIRI Mkuu “aliyeng’olewa na Bunge,” Edward Lowassa, ameanza kujitetea akisema hakupokea rushwa yoyote kutoka kampuni ya Richmond Development Company. Lowassa anasema kilichotokea ni kwamba aliponzwa na watendaji walio chini yake; na kwamba binafsi hakuhusika na mchakato mzima ulioipa ushindi wa zabuni Richmond.

Anasema, “Sikuhusika katika mchakato wa zabuni ulioipa ushindi Richmond. Mimi niliponzwa na wasaidizi wangu. Hawa ndiyo walioniangusha. Nimewajibika kwa niaba yao,” Lowassa amewaambia wafuasi wake na wananchi kwa ujumla. Lowassa anasema kazi ya kufanya uchambuzi wa kuchagua mzabuni, haikufanywa na yeye, bali ilifanywa na Kamati Maalum ya Serikali (GNT).

Hakuna ubishi kwamba utetezi huu mpya wa Lowassa unahitaji kuhojiwa. Je, Lowassa kwa nini hakueleza haya ndani ya Bunge; Na alipewa nafasi bungeni, alishindwa kulieleza Bunge kile ambacho kwenye mkutano wa hadhara, kijijini kwake, katika jimbo la Monduli? Inawezekana kabisa, Lowassa hakusema bungeni yale aliyosema Monduli kwa kuwa alijua wabunge wangeyapinga kwa kuwa wanajua ukweli mzima wa suala hili.

Ndiyo maana wala hakujihangaisha kujibu hoja za Kamati teule iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, iliyoonyesha mazingira ya kuhusika kwake. Vilevile, Lowassa alijua kuwa Bunge lingekataa utetezi wake. Matokeo yake, angebanwa na kanuni zinazotaka mbunge kutosema uwongo bungeni.

Inawezekana pia kwamba Lowassa alishindwa kusema hayo bungeni, kwa hofu kwamba Nazir Karamgi na Dk. Msabaha walikuwamo ndani ya Bunge, na hivyo wangeweza kusema ukweli wa yote yaliyotokea. Lakini ukiacha hilo, hata utetezi wenyewe wa Lowassa bado una mashaka.

Kwanza, Lowassa anakubali kuwa Kamati ya Maalum ya serikali iliyoshughulikia zabuni ya Richmond iliundwa kwa maelekezo na maagizo yake. Lowassa ambaye leo anakana kuhusika na Richmond, ndiye anasadikiwa kutoa amri na hata kutisha wasaidizi wake, akitaka Kamati “Ibebe Richmond” na kuipa kazi iliyoomba.

Vilevile, ni Lowassa ambaye anatajwa kushinikiza upokonywaji Bodi ya Tenda ya Tanesco kazi ya kutafuta mzabuni, baada ya Bodi hiyo kukataa kuipa kazi ya kufua umeme wa dharula kampuni ya Richmond.

Ni Lowassa yuleyule anayetajwa kushinikiza kupunguzwa kwa vigezo ili kufanikisha azima ya kuipa kazi kampuni hiyo ya kitapeli. Lowassa na wenzake walijua, pasipo na shaka kuwa Richmond ni kampuni isiyokuwa na hadhi, sifa, wala uwezo wa kufanya kazi iliyotaka kupewa.

Hili linathibitishwa na barua ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha kwenda kwa Lowassa, ambayo watetezi na wafuasi wa Lowassa wanaitumia kutaka kumsafisha. Barua hiyo yenye Kumb. Na. CDB 286/397/01 ya 17 Juni, 2006 inasema, “…Nakubaliana na mapendekezo ya Kamati ya Majadiliano ya Serikali (GNT) ya kuteua Richmond na naomba kuwasilisha kwako, kwa uamuzi na maelekezo.”

Hii inathibitisha madai ya siku nyingi kwamba aliyeiteua Richmond kuingia mkataba na Tanesco, hakuwa Dk. Msabaha, alikuwa Lowassa. Ni wazi kwamba Lowassa alitumia ustadi mkubwa kuiteua Richmond, kwani alitumia kichaka cha Kamati yake ya Majadiliano.

Barua ya Dk. Msabaha inaonyesha na kuthibitisha ukweli kwamba Lowassa alikuwa mstari wa mbele katika kusimamia, kupitisha, kuagiza na hata kuamuru Kamati kuipa zabuni Richmond. Si barua ya Dk. Msabaha pekee, ambayo inathibitisha ukweli huo, bali hata barua iliyotoka ndani ya ofisi ya Lowassa mwenyewe inaliweka wazi jambo hili.

Msaidizi Mkuu wa Lowassa, Ole Kuyan, katika barua yake kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anasema, “…Endelea kusaini mkataba kati ya Richmond na serikali, maana Waziri Mkuu, Edward Lowassa tayari ameridhika kwamba Richmond ipewe mkataba.

Kauli kwamba Waziri Mkuu Lowassa “ameridhika” inafunga mjadala na inadhirisha kwamba Lowassa alijua kila hatua katika kufanikisha mkataba huu. Aidha, kauli ya Kuyan, kwamba Waziri Mkuu ameridhika na hivyo mkataba kati ya serikali na Richmond usainiwe, inaonyesha wazi kuwa Lowassa ndiye aliyekuwa anasimamia jambo hili.

Kwa upande mwingine, hoja ya Lowassa kwamba aliwahi kumuonya Dk. Msabaha kuhusu “Ubabaishaji wa Richmond,” na “kutaka kuvunja mkataba huo mara mbili, lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na kuzuiwa na wanasheria,” haina uzito wala mantiki.

Sababu ni mbili: Kwanza, hakuna hata mwanasheria mmoja nchini na nje ya nchi, ambaye angeshauri serikali kubaki katika mkataba wa Richmond, kama Lowassa angesema ukweli kwamba Richmond haipo kwa mujibu wa sheria.

Hii ina maana haipo katika orodha ya kampuni za Marekani, wala katika orodha ya Wakala wa Msajili wa Kampuni (BRELA) nchini Tanzania. Lilikuwa ni jukumu la Lowassa kuwaeleza kinaga ubaga wanasheria kwamba, si hapa Tanzania wala Marekani, ambako Richmond imesajiliwa.

Halikuwa jukumu la wanasheria kujua kama Richmond ni kampuni hewa. Hilo lilikuwa jukumu la Lowassa na serikali yake. Kwani wanasheria ni kama madaktari; jukumu la kueleza maradhi linabaki kwa mgonjwa mwenyewe. Na mficha maradhi, umauti humfichua. Lowassa hakuchukua jukumu hilo.

Hakusema ukweli kwa wanasheria kuwa Richmond haipo kisheria. Kwamba Richmond ni kampuni ya mfukoni. Kwamba haina uwezo wala heshima ya kufanya kazi na serikali. Kwa hakika, kama yote haya yangejulikana wazi kwa wanasheria, lazima wangeshauri serikali kuvunja mkataba, tena mara moja.

Kwa kuwa Richmond haikuwa imesajiliwa, wanasheria wanajua kuwa hakuna mtu ambaye angekwenda mahakamani na kudai yeye ni mmiliki wa Richmond. Je, angeanzia wapi? Angetumia nyaraka gani kuthibitisha madai yake? Angesema nini mbele ya sheria? Wapi hasa angeshika?

Kutokana na hali hiyo, Lowassa asitake kukwepa jukumu lake la kikatiba la kutumia vyombo vya serikali kufanya uchunguzi na kujua uhalali wa kuwapo kwa Richmond. Serikalai ilipaswa kujua nani mmiliki wa Richmond. Yuko wapi? Uwezo wake kifedha ni upi?

Je, si tapeli lililokubuhu ambalo lilitaka kuingiza taifa mkengeni kama ilivyotokea? Lilikuwa ni moja ya majukumu ya ofisi ya Lowassa kwenda BRELA, na kupekua mafaili ili kubaini ukweli wa madai ya wananchi na vyombo vya habari vilivyokuwa vinapaza sauti vikisema, Richmond haikuwa kampuni, bali kilikuwa kikundi cha watu waliojikusanya ili kuchota hazina ya taifa.

Lakini pamoja na kwamba Lowassa alijua ukweli huo, aliamua kukaa kimya. Hili alilifanya ili kupata mahali pakutokea, pale ukweli utakapodhihiri. Maana hata pale ilipodhihirika kuwa Richmond haikuwa na uwezo wa kifedha, na kwamba mabenki ya Marekani yamekataa kutoa barua ya dhamana (LC), bado serikali iliamrisha au ilishauri au ilishawishi benki ya CRDB kubeba jukumu hilo.

Je, mbona Lowassa hataki kulisema hili, badala yake anaendelea kung’ang’ania wanasheria akidai wamemshauri vibaya? Ni Lowassa ambaye alijiapiza na kusema, “Richmond ni watu makini,” na kwamba umeme utaingia katika Gridi ya Taifa ndani ya mwezi mmoja. Ni uwongo huo uliomuambukiza Rais Jakaya Kikwete, hadi kufikia kuchukua hatua ya kuwadanganya wananchi na jumuiya ya kimataifa juu ya ujio wa umeme wa Richmond.

Wanaokumbuka vema wanajua kuwa alikuwa ni Lowassa ambaye alihubiri wananchi kutojadili Richmond kwa madai kwamba, “mabwawa ya kuzalisha umeme tayari yamejaa maji,” na hivyo hakuna tena tatizo la umeme nchini.

Ukiondoa hilo, kuna hili analolieneza kuwa yeye ni bingwa wa kuvunja mikataba nchini. Mfano anaotoa ni mkataba kati ya serikali na kampuni ya City Water. Sasa swali tunajiuliza: Kama kauli ya Lowassa ina ukweli, kwa nini alishindwa kuvunja mkataba huu wa Richmond?

Mbona huu ndiyo ulikuwa wazi zaidi, ambapo hata ‘juha’ alifahamu kuwa Richmond ilikuwa kampuni ya kitapeli? Kudai kuwa serikali na Lowassa hawakujua kuwa Richmond lilikuwa genge la walaghai, na hivyo kuwaachia matapeli wa kila rangi kufanya watakavyo, ni kuidharaulisha serikali kwa viwango vya juu mno.

Katika taarifa yake kwa Shirika la Habari la Associated Press (AP) la Marekani, anayetajwa kuwa mmiliki wa Richmond Mahammed Gire anasema, “Si sisi, wala yeyote kati ya watumishi wetu, hakuna aliyepokea sarafu nyekundu au kulipwa chochote, kutoka serikali ya Tanzania au kwa ofisa yeyote wa kampuni yetu.”

Anasema, “Badala yake tumekuwa tukishuhudia kauli za uongo na madai potofu juu yetu,” inasema taarifa ya kampuni hiyo. Je, Waziri Mkuu Lowassa hana wasaidizi? Kwa nini alishindwa kuwasiliana na Mohammed Gire, aliyetajwa kuwa mmiliki wa Richmond na kujua ukweli wa jambo hili? Je, kama yote haya aliyajua, lakini alishindwa kuyasimamia kwa dhati, kwa nini watu wanajihangaisha kutaka kumsafisha? Mkurugenzi wa Mawasiliano wa ikulu, Salva Rwenyemamu amethibitisha kuwa anamfahamu aliyekuwa anadaiwa kuwa “mwenye” Richmond, mtu mmoja aitwaye Gire.

Salva anakiri kuwa alitambulishwa kwa mtu huyo na Rostam Aziz ambaye alikiri pia kuwa ni rafiki yake. Vipi Lowassa alishindwa kuwasiliana na rafiki yake sana, Rostam Aziz kuhusu suala hili? Kutokana na maelezo hayo ya Salva ambayo hayawezi kutiliwa mashaka, ni wazi kuwa Rostam anaijua vema kampuni ya Richmond.

Na kwa kuwa Lowassa na Rostam ni chanda na pete, hakuna mwenye ubavu wa kumficha mwenzake jambo. Hivyo haiingii akilini kwamba Rostam angeweza kumdanganya Lowassa juu ya Richmond, hadi Lowassa aharibikiwe kwa kiwango hiki.

Kwa kiongozi kama Lowassa kukubali kuidhinisha mamilioni yote hayo ya shilingi kwa kampuni hewa, ni lazima kuna jambo limejificha.

Ndugu zangu majizi kama lowassa,ni ya kuogopa kama ulama
 
Mkuu wa kaya yeye anacheka tu, anacheka tu, anacheka tu.

Majimbo ya uchaguzi yanagezwa ili kila mhusika wa karibu apate la kwake yeye anacheka tu.
 
Tulitarajia ujio wake huyu ni kawaida sana. Huyu anatamani aandike haya makala magazeti yote hapa Tanzania, bahati mbaya ni kwamba haiwezekani. Ataandika sana tena sana, lakini safari ya matumaini ndio imeanza tayari!

Alhamisi ijayo ataandika tena! Tar 30.05.15 asisahau kwenda Arusha ili apate cha kuandika tena!
 
habari ya mjini
makongoro cv
1.alikuwaga mlevi kama Mkapa na KENYATTA junior na BUSH
2.MAHAKAMA ilitengua ubunge wake kwa kosa la kuanza kampeni mapema na SI KOSA LA TAKRIMA
3.hakupigiwa kampeni za ubunge na baba yake
4.hakugombea ubunge kupitia chama cha baba yake
5.Alishinda ubunge njee ya mkoa wake asilia yaan Mara na au DAR
6.HATA KIKWETE RAIS hana uwezo wa kushinda ubunge ARUSHA mjini ila Makongoro alishinda

Nipe CV ZA MGOMBEA WAKO
nakutabiria:
1.atakuwa fisadi wa richmond
2.Atakuwa fisadi wa escrow
3.atakuwa fisadi wa pesa za Libya na mara kusilimisha taifa
4.Atakuwa Muuza nyumba za serikali na mzee wa bil 262
5.atakuwa mzee wa kuiba mitihan kule Galanos
6.

hapo niambie kati ya Makongoro na mgomea wako nani anafaa urais????
 
Mwaka huu Mungu atawaumbua waizi nyie.
 
hayo tuwaachie wanasiasa.
 
Ni kweli TeamLowassa boss wako kumsafisha inataka moyo,ukichaa,wehu fulani vile.Hakika huyu kijana Lowassa ni jasiri sana anataka nikamsafishe jimboni kwake Monduli by "J K Nyerere"

Tulitarajia ujio wake huyu ni kawaida sana. Huyu anatamani aandike haya makala magazeti yote hapa Tanzania, bahati mbaya ni kwamba haiwezekani. Ataandika sana tena sana, lakini safari ya matumaini ndio imeanza tayari!

Alhamisi ijayo ataandika tena! Tar 30.05.15 asisahau kwenda Arusha ili apate cha kuandika tena!
 
Last edited by a moderator:

safari hiyo itaishia palepale Chimwaga.
 
Tulitarajia ujio wake huyu ni kawaida sana. Huyu anatamani aandike haya makala magazeti yote hapa Tanzania, bahati mbaya ni kwamba haiwezekani. Ataandika sana tena sana, lakini safari ya matumaini ndio imeanza tayari!

Alhamisi ijayo ataandika tena! Tar 30.05.15 asisahau kwenda Arusha ili apate cha kuandika tena!

Hii ni ya SIKU NYINGI sanaa...!!! tokea 2008.....wakati huo Kubenea hakujua ukweli halisi, kuwa Richmond ni ya Mkulu...!!!

Hivi sasa, Kubenea ni team Lowassa 100%, hii ni baada ya KUJUA WAZI PASIPO SHAKA, kuwa Lowassa hakula hata senti tano ya Richmond...!!!

Mpigieni Said Kubenea, sasa hivi ni Team Lowassa 100%, sbb kajua ukweli halisi, Lowassa alibeba tu majukumu kuiokoa Chama na Serikali yake...

Na hakuna sasa wa kuzuia mafuriko...mvua kubwa ya mawe itaanza rasmi Arusha 30 May 2015, ikiandamana na upepo mkali na lightining ya hatari, kwa wale walio Arusha mahoteli yote yamejaa, Ni safari mpya ya matumaini...!!!
 
Sema anakufaa ww, we don't get tempted, he is not even a Leader, we know him, just a hooligan and drunkard...!!! Nothing he did so special to Tanzanians, even kuwa Waziri hakuwahi, sbb hana UWEZO HUO...!!!

Najua unajua nani ana nguvu CCM kwa sasa... so mnajihangaisha tu.. keep ur eyes open, muone the King of Tz politics how he moves the GAME... hii issue ndogo sana kwa Lowassa... hili ni jabali la CCM na Wananchi wanampenda... ukijidanganya ananunua watu, ur lost, subiria few days ahead, ndio uje useme hapa kanunua watu... We are moving ahead, and CCM will dominate, na sio mwingine kwa sasa thru Lowassa...!!! easy..easy...easy..!!!

habari ya mjini
makongoro cv
1.alikuwaga mlevi kama Mkapa na KENYATTA junior na BUSH
2.MAHAKAMA ilitengua ubunge wake kwa kosa la kuanza kampeni mapema na SI KOSA LA TAKRIMA
3.hakupigiwa kampeni za ubunge na baba yake
4.hakugombea ubunge kupitia chama cha baba yake
5.Alishinda ubunge njee ya mkoa wake asilia yaan Mara na au DAR
6.HATA KIKWETE RAIS hana uwezo wa kushinda ubunge ARUSHA mjini ila Makongoro alishinda

Nipe CV ZA MGOMBEA WAKO
nakutabiria:
1.atakuwa fisadi wa richmond
2.Atakuwa fisadi wa escrow
3.atakuwa fisadi wa pesa za Libya na mara kusilimisha taifa
4.Atakuwa Muuza nyumba za serikali na mzee wa bil 262
5.atakuwa mzee wa kuiba mitihan kule Galanos
6.

hapo niambie kati ya Makongoro na mgomea wako nani anafaa urais????
 
mfa maji haachi kutapatapa, LOWASSA anatapatapa.

Jipe moyo, Ujidanganya, ni wananchi kwa wingi wao ndio wateuzi, CCM itampitisha ukiona....

U talk, anti-Lowassians they talk, but Lowassa is WALKING THE TALK....hv u noticed big difference there...!!? haven't you..!? if not, ur puzzled...!!!
 
ukisikia maajabu duniani ni pamoja na hilila mijitu kumng'ang'ania mhujumu mkuu kuwa kiongozi mkuu wa nchi!

Pamoja na kwamba binadamu tunatofautiana kwa
hekima na uelewa, yapo mambo amabayo mtu unatakiwa uone aibu mbele ya watu.

Wallahi sijui wamelishwa nini hawa?
 
Tulitarajia ujio wake huyu ni kawaida sana. Huyu anatamani aandike haya makala magazeti yote hapa Tanzania, bahati mbaya ni kwamba haiwezekani. Ataandika sana tena sana, lakini safari ya matumaini ndio imeanza tayari!

Alhamisi ijayo ataandika tena! Tar 30.05.15 asisahau kwenda Arusha ili apate cha kuandika tena!

Pole kwa muweweseko.Lowasa ni jizi na tapeli LA kimataifa.Wachumia tumbo kama wewe lazima mulitetee mkitarajia kushibisha njaa zenu
 
Tulitarajia ujio wake huyu ni kawaida sana. Huyu anatamani aandike haya makala magazeti yote hapa Tanzania, bahati mbaya ni kwamba haiwezekani. Ataandika sana tena sana, lakini safari ya matumaini ndio imeanza tayari!

Alhamisi ijayo ataandika tena! Tar 30.05.15 asisahau kwenda Arusha ili apate cha kuandika tena!

Wakati mnachumia matumbo yenu mnatakiwa pia na kufikiri kama huyu EL mnaempigia debe wakati anajitahidi kurudiaha gharama zake hicho mlichochuma kitakuwa kinawatosha ninyi na familia zenu na jamaa zenu wote kukabiliana na hali itakavyokuwa ngumu wakati huo

Je matumaini haya mnayoyatangaza kwasababu munayapewa sasa hayatakuwa kilio wakati huo?
Kweli ni njaa zinawasumbua ila kuweni na akili mujiulize shibe munayoipata oktober ikishaisha mutaweza kuvumilia njaa ya miaka kumi?
TAFAKARINI
 
Back
Top Bottom