Lowassa anapendelewa na Vyombo vya Habari?

Lowassa anapendelewa na Vyombo vya Habari?

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,266
Wakati huu mchakato wa wanachama wa CCM waliochukua fomu kuwania kuteuliwa kukiwakilisha chama katika kinyang'anyiro cha urais kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu 2015 wakizunguka mikoa mbali mbali kutafuta wadhamini, waziri mkuu aliyejiuzulu ambaye naye anawania kuteuliwa anaonekana kupewa upendeleo wa wazi kwenye vyombo vya habari kama televisheni, redio na magazeti.

Mimi binafsi sijaelewa kama upendeleo huu ni kutokana na mhusika mwenyewe kuwagharimia waandishi wa habari au ni vyombo vyenyewe ndio vinaonesha upendeleo huo au kuna asali imepitishwa ili jamaa apewe promo kubwa. Ukweli ukifuatilia taarifa za mizunguko ya watia nia wakitafuta wadhamini, Lowassa anapambwa sana na vyombo vya habari hasa TV kuliko wenzake.

Yaani wengine hata hawasikiki utadhani wamechukua fomu na kwenda nazo nyumbani. Mimi nashauri vyombo vya habari kutupa habari kwa haki na usawa kwa watia nia wote hasa kama taarifa zao zinagharimiwa na vyombo husika.

Lakini Kama ni watia nia wenyewe ndio wanaogharimia waandishi hapo sina neno kwani jamaa yule mpunga kwake sio tatizo na kila mwandishi angependa kuambatana naye maana wahenga walisema "Fuata asali ule nyuki"
 
Huo ni mtazamo wako tu kwamba anapendelewa
Badala useme nyota yake inang'aa kila kona anaonekana yeye tu ina maana hata tukishinda pamoja utasema wapigakura wamempendelea badala ya kusema ameshinda
 
Habari ya mujini ni Lowassa. Kigoma kapata wadhamini zaidi ya 11000.Jaribu kuzuia mafuriko na vidole. Utabebwa na maji bure.Kubalini yaishe.

Mtakapo rudi mjini, mkakuta biashara hakuna ndio mtasaga meno
 
Fisadi Lowassa AKA mgawa rushwa mashuhuri katika nyumba za ibada kupitia "mchango wa marafiki zake" wa mabilioni si ajabu kishagawa rushwa ya nguvu mpaka kwenye vyombo vya habari ili wampigie debe la nguvu.
 
Ni vinavyonunulika Tbc, daily news, idara ya hbr maelezo hana mashiko.....
Kweli hivi vya binafsi ndio vimezidi utafikiri vyote anavimiliki yeye.
 
Ile style inaitwa huwezi zuia mafuriko kwa mikono bado inawapa homa wachanga wa siasa za Tx
Hapa ndio kwanza safari imeanza
 
Napata tabu sana kama kweli watz tumeamua kumwingiza ikulu fisadi. Hivi kweli urais unauzwa kwamba una bei?
 
nimewafatilia sana ITV,wamekuwa wakimrusha sana lowassa au ndio mambo ya ukanda?mbona watia nia wako wengi sana ccm lakini chombo hicho kimekuwa kikirusha sana lowasa kuliko wagombea wengine.....tumesha jua ajenda yenu ninyi watu wa lowassa na ukaskizini.
 
nimewafatilia sana ITV,wamekuwa wakimrusha sana lowassa au ndio mambo ya ukanda?mbona watia nia wako wengi sana ccm lakini chombo hicho kimekuwa kikirusha sana lowasa kuliko wagombea wengine.....tumesha jua ajenda yenu ninyi watu wa lowassa na ukaskizini.

Duh! ni lazima uangalie ITV? chepuka
 
Mbona huwa wanamrusha hata kwa mabaya ambayo mhusika (Lowassa) sidhani kama angependa yarushwe.
Nazungumzia tukio la kuzomewa siku mbili zilizopita.
 
Duuuh kama na wewe una fikra ya ukanda nakuwa na mashaka na kichwa chako.....
 
Back
Top Bottom