Jamani someni wenyewe jinsi team Lowassa Bungeni alivyomuua makongoro nyerere.
========
MTOTO wa Baba wa Taifa, Julius Nyerere, Makongoro, amekosa ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kwa sababu ya lugha isiyopendeza aliyoitumia dhidi ya vigogo wa upinzani kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, gazeti hili limeelezwa.
Makongoro Nyerere, ambaye mwaka 2015 alikuwa mmoja wa wapiga debe mashuhuri wa aliyekuwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli ambaye hatimaye aliibuka mshindi.
Hata hivyo, Makongoro ambaye aliwahi kuwa mwanachama wa chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi, mwaka 2015 alikuwa akifahamika kwa “vijembe’ vyake vikali dhidi ya aliyekuwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
“ Mwaka 2012, wakati Makongoro alipopata ubunge wa Afrika Mashariki, alibebwa na kura za wabunge wa vyama vya upinzani. Kule CCM hakuwa anapendwa sana lakini wapinzani walimpa kura kwa sababu walimwona kama mwenzao.
“ Lakini, kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, yeye ndiye aliyeongoza mashambulizi dhidi ya Lowassa. Maneno yake mengine yalikuwa makali kiasi kwamba wapinzani waliumizwa.
“ Kwenye uchaguzi wa safari hii, wabunge wa upinzani wakapiga kura za chuki kwake. Matokeo yake ni kwamba amekosa nafasi ya ubunge ambayo angetakiwa aipate,” alisema mbunge mmoja kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambaye alipiga kura mwaka 2012 na mwaka huu. Kwa sababu ambazo hakutaka kuziweka wazi, mbunge huyo aliomba kutotajwa kwenye habari hii.
Katika uchaguzi wa kuwania nafasi za EALA mwaka 2012, Makongoro alipata jumla ya kura 123 lakini katika uchaguzi wa safari hii, alipata kura 87 tu.
“ Funzo kubwa ambalo Makongoro anawapa wanasiasa vijana ni kwamba wanatakiwa waweke akiba ya maneno yao. Wakati anamsema Lowassa mwaka 2015, alisahau kwamba atarudi tena kuomba kura za wapinzani kwenye ubunge wake. Vijana waweke akiba ya maneno,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Nafasi ya Makongoro imechukuliwa na mwanasheria mgeni katika medani za kisiasa hapa nchini, Dk. Ngwaru Maghembe ambaye ni mtoto wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe.
Mshindi mwingine wa EALA katika uchaguzi uliopita, Adam Kimbisa, alifanikiwa kutetea nafasi yake kwa upande wa wanaume kupitia CCM Tanzania Bara.
Chanzo: Raia Mwema