Lowassa amfagilia rais Kikwete

Lowassa amfagilia rais Kikwete

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

JUL192013

Na Swahili TV

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Edward Lowassa, amemsifia Rais Jakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata heshima katika ulingo wa kimataifa, aliyasema hayo wakati akihojiwa na Swahili TV jijini Washington DC.

Alisema kitendo cha Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama, kuja nchini na viongozi mbalimbali wa mataifa makubwa kumeonyesha Rais Kikwete anakubalika.

"Ni hivi karibuni tu Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani George W.Bush walikuwa nchini Tanzania, hii inaonyesha kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa" alisema Mheshimiwa Lowassa.

Mheshimiwa Lowassa ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi, aliongeza kwa kusema, Rais Kikwete anastahili pongezi sana kwa hilo kwani sio rahisi kwa viongozi wa mataifa makubwa kutembelea nchi zingine labda kama mko juu sana katika medani za kimataifa.

Pia alisema Rais Kikwete amekuwa akihusishwa na utatuzi au ushauri wa kutatua matatizo mbalimbali ya nchi zingine na pia ameanza kuishirikisha Tanzania katika usimamizi wa amani katika nchi mbalimbali.

Tanzania iliweka historia hivi karibuni kwa maraisi wawili wa Marekani kukutana katika nchi moja kwa wakati mmoja, Rais Barack Obama na George W.Bush walikutana jijini Dar es Salaam mwezi huu.

 
Heshima kubwa ni nyumbani bana siyo ughaibuni.


156395_547413758655490_286445152_n.jpg
 
Wanapendeleana inaonyesha Wanasameheana HAWA na kidogo kidogo Wanapeana VYEO kimya kimya...
Naona KIKWETE kaisha jua MEMBE hawezi kuongea kwenye JUA KALI...
 

JUL192013

Na Swahili TV

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Edward Lowassa, amemsifia Rais Jakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata heshima katika ulingo wa kimataifa, aliyasema hayo wakati akihojiwa na Swahili TV jijini Washington DC.

Alisema kitendo cha Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama, kuja nchini na viongozi mbalimbali wa mataifa makubwa kumeonyesha Rais Kikwete anakubalika.

“Ni hivi karibuni tu Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani George W.Bush walikuwa nchini Tanzania, hii inaonyesha kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa” alisema Mheshimiwa Lowassa.

Mheshimiwa Lowassa ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi, aliongeza kwa kusema, Rais Kikwete anastahili pongezi sana kwa hilo kwani sio rahisi kwa viongozi wa mataifa makubwa kutembelea nchi zingine labda kama mko juu sana katika medani za kimataifa.

Pia alisema Rais Kikwete amekuwa akihusishwa na utatuzi au ushauri wa kutatua matatizo mbalimbali ya nchi zingine na pia ameanza kuishirikisha Tanzania katika usimamizi wa amani katika nchi mbalimbali.

Tanzania iliweka historia hivi karibuni kwa maraisi wawili wa Marekani kukutana katika nchi moja kwa wakati mmoja, Rais Barack Obama na George W.Bush walikutana jijini Dar es Salaam mwezi huu.


Mtake msitake Kikwete ameandika Historia ya utendaji ambayo haijawahi katika awamu zote,Jk kiboko Yao,mchapakazi na mtulivu mwenye wivu atajiju Jk Hoyeeerrrrrr
 
Huo nao ni mkakati wa kutafuta urais. Baada ya kumaliza kwenye nyumba za Ibada sasa anahamia kwa viongozi. Kazi ipo. Akipita humu nchini anasema bomu la vijana kukosa kazi pamoja na udini wa elimu. Double standards.
 
ile Hatujakutana barabarani imeanza kufanya kazi hatimaye.
 
Ndege wenye rangi moja huruka pamoja

To know the enemy is half the victory"
 
EL anajua kuzichanga vizuri akipata fursa huwa hafanyi makosa.
 
Kiongozi wa nchi kamwe hawezi kupata heshima kwa kutembelewa/kusifiwa na Viongozi wa Mataifa Tajiri bali kwa utendaji wake wa kuwaletea Wananchi wake maendeleo na hatimaye nchi yake. Tumkumbuke Mobutu ambaye alikumbatiwa na Mataifa ya Magharibi lakini alikuwa ni fisadi mkubwa wa utajiri za Zaire. Fisadi Lowassa hatufai kama kiongozi wa nchi hana tofauti kabisa na janga la Taifa.
 
Back
Top Bottom