Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
Lowassa alikuwa amebebwa na watu wakawaida, wanasiasa na vyombo vya habari. Alikuwa amewekwa mabegani salama, akajitapa tapa kuwa mwaka huu ni wake. Aliaminika sana kwa vile alikuwa anaonyesha amejiandaa kwenda Ikulu tangu na 1995. Watu na vyombo vya habari vikafanya ushabiki, wakajitoa akili. Inaonyesha alikuwa hajui kwa nini amebebwa. Akajua kubebwa ni kubebwa. Akalala usingizi wa pono.
Akabebwa na hali hii mpaka ilipofika wakati wa maamuzi ya kumtangaza Mh. Magufuli kuwa ndo atasimama kugombea urais ndani ya CCM. Kukatwa kwake kuko wazi sana. Kulikuwa na ukinzani kwake ndani ya chama na kada ya wasomi nje ya chama chake wa kujiadhari na siasa la Lowassa.
Ni katika wakati huo alipopoteza nguvu na tumaini lake mpaka alipopta nguvu mpya ya kumbeba ya UKAWA. Huku akiendelea na siasa zake za makundi na kujitangaza, alikuwa anaonyesha kasi ya 100% kuingia Ikulu.
Akaanza kudondosha waliombeba!!!!
Taarifa zinaonyesha Lowassa amewavunja nguvu watu wengi kutokana na uwezo wake wa kujieleza na kueleza vitu kwa ufasaha. Ameonyesha katika uzinduzi wa kampeni zake kuwa hajajiandaa kuwa rais wa Tanzania. Ameonyesha mikoani akitumia salamu za CCM. Anaonyesha mwili ni wa UKAWA na Roho ni ya CCM. Anashindwa kukana dhamili yake ya CCM.
Imekuwa kama kasumba kwake kuongea sentesi fupi fupi zinazoshindwa kufikisha taarifa kwa watu.
Hii imesababisha watu wengi kumgeuka. Chama chake alichokwenda cha CDM kimemtelekeza kwa sehemu kubwa. Katika ziara zake za mikoani amekuwa akiandamana sana na wale wachache waliokatwa kama yeye kutoka CCM.
Vyombo vya habari vimeanza kushindwa kutoa taarifa za mikutano yake. Inawezekana ni mbinu za kufifisha habari zake kuufikia umma na kuwafumbua. Taarifa huru zinaonyesha baado anahangaika hata wakati mwingine kujisahau kam yuko UKAWA. Hii ni shida.
Idara za habari za vyama vinavyo unga UKAWA havitoi taarifa zake. Wamebaki watu baki kuleta picha za mikutano yake huko anakozunguka. Kuna kitu kuwa ametuangusha!!! Anatumia salamu za CCM katika mikutano yake. Nani ataandika haya zaidi ya kulaumu waliomleta na kumtetea?
Alitangaza kuleta watu maarufu maarufu ndani ya UKAWA, sasa inaonyesha analeta waliopita katika mikono ya kukataliwa kama yeye kule CCM.
Nimeona sasa anachangisha michango ya kusaidia kampeni. Wenye nazo wamesepa. Hawaoni kama jamaa atapata walichotaka kutoka katika safari yake.
Ukweli amewadondosha!!!
Swali la kujiuliza ni kuwa kama wamewadondosha waliombeba yeye atakuwa salama katika uchaguzu huu?
The Gaza