EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
Ujio wa Lowassa upande wa upinzani umesaidia sana kuondoa siasa za uhasama tulizo zoea kuziona wakati wa kampeni huko nyuma.
Kipindi kama hiki tulizoea kusikia polisi wakiwashikilia wafuasi au viongozi wa vyama vya upinzani kwa makosa madogo madogo sana yakiwemo ya kuzidisha muda wa kampeni kwa dk 5 tu au kwa kuandamana baada ya mkutano.
Pongezi pia kwa jeshi la polisi kwa kupunguza matumizi ya mabomu yasiyo ya lazima wakati huu wa kampeni.
Haya matukio kama yapo ni machache sana.
Binafsi sielewi sababu kuu ni nini, ila inawezekana ni ustaarabu wa mgombea wa Ukawa kwa tiketi ya Chadema Lowassa kutojihusisha binafsi kujibizana na mahasimu wake.
Shukrani kwa vyama vyote, vyombo vya dola na serikali kwa ujumla tuelewe hii nchi ni yetu sote.