Lowassa amekata tamaa,waliomshangilia wanamkimbia!

Lowassa amekata tamaa,waliomshangilia wanamkimbia!

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,505
Reaction score
16,006
Nyota njema huonekana asubuhi, ndivyo unavyoweza kusema katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kupigwa chini na watanzania,Aliyekuwa Mgombea uraisi wa Chadema ndg.Lowassa anaitia katika wakati mgumu. Ni kama gundu la ufunguzi wa mwaka 2016 pale rafiki yake mkubwa Gwajima alipotangazia waumini wake na Dunia kuwa hakuwahi kumuunga mkono Lowassa. Kisaikolojia tulijua kitumbua kimeingia mchanga.

Muda haukupita wapiga domo wake wakuu tokea CCM, wakiongozwa na Mwapachu,Msindai na makundi mengine mamilioni yakimtosa kimya kimya yakimuacha bila kumuaga.

Makada Chadema nao wamemtosa bila kumtaarifu, hawamtembelei wala kumzungumzia kama ilivyokuwa baada ya uchaguzi. Hawataki kuhusishwa naye kwa Lolote, wamemwachia Mbowe 'zigo' la msumari.

kitu pekee kinachomliwaza ni wanahabari, angalau kwa vijisenti wanalazimika kumuandika. Vijana wa chadema Mtandaoni, wakiongozwa na Kijana Yericko Nyerere aliyewahi kujitambulisha kama Mwenyekiti wa chadema mitandaoni wamefunga midomo na vidole vyao haviandiki hekaya zozote za kumsifu kamanda Lowassa.

Ni dhahiri, pamoja na mafuriko Lowassa amechuja mapema sana kwenye vinywa vya makamanda ukilinganisha na Dr.Slaa ambaye alidumu kwenye vinywa vya makamanda miaka takribani mitano hadi pale Mbowe aliporubuniwa.

Ukweli mwingine ni kuwa atabaki hapo chadema kwani ana hati miliki lakini wale makamanda halisi wanashirikiana naye kwa kujificha ficha, hawataki jamii iwahusishe naye. Ukiacha Mbowe na Mashinji ni ngumu kukuta vijana wengine wakiwa karibu naye ili kulinda kumbukumbu zao siku za mbeleni.

Nawasilisha.
 
Leave EL in your frustrations, and stop insecurity...
 
chadema phobia, dada jitambue mwaka umeisha hamjamshauri JPM kuhusu kiwanda kipi kianze kufanya kazi zaidi ya kupambana na chadema, Kikwete kakaa pembeni ameanza kujitambua, umemsikia?! chukua hatua.
 
Hawa ndio wanategemewa na Rais kufanikisha vipau mbele vyake,ila wao masaa 24/7 wanaiwaza Chadema
 
Ndugu lopolopo fahamishwa kuwa…

Mh. Lowasa tuko naye mkuu na kwa kifupi tumeMMISS sana majukwaani, kumbuka alipotokea Bukoba kutoa pole ya tetemeko tulichanganyikiwa na kupagawa kwa furaha baada tu ya kumuona bukoba na ata CCM kwa wivu wao ulokithiri waliwaagiza Police waje watutawanye kwa mabomu ila walichelewa kwani kumuona tu tuliisha pata nafuu ya tetemeko,

Pia kwa taharifa yako hao viongozi wako wa CCM wanaopayuka ovyo ndo tushawachoka. Wakitokea ktk TV huwa nabadili station Mfano, Jana kuna libabu moja la CCM linaitwa madabida, lile liliwahi kuuza ARV fake kwa wagonjwa wa ukimwi, gafla lilipotokea ITV niliikimbia iyo channel na kuamua kumuwekuea mwanangu channel yake pendwa ya Cartoon network.
 
Ndugu Kashorobana .. Bukena sio kweli... Nani kakwambia watu walikuja kumuona Lowassa.. Watu walikuja kumuona mtu alieshinda uchaguzi
 
Ndugu Kashorobana .. Bukena sio kweli... Nani kakwambia watu walikuja kumuona Lowassa.. Watu walikuja kumuona mtu alieshinda uchaguzi

Alexism, thanx kunikumbusha Bukena na Bukeije. Kigamboni ni samaki mchele tu, uliyoyasema ni kweli uyu Mh. Lowasa leo akipata nafasi ya kuwaita watu Jangwani nadhani MACCM yatajificha. No more nakuzawadia maLIKES ya kumwaga, Thanks/ wakola kyoma
 
Naona siku huzi umehamia nyumbani kwa lowasa hadi umejua ni nini kina msibu.
 
Vijana mlikua mstari wa mbele kuleta mabadiriko ambayo kweli kila mtanzania aliyatarajia na kuyapenda... Lkn kumbuke kua mlichokua mnakitaka kulikua ni kumwaga ugari wa kundi jingine ambalo kwa kufa au kupona haukua tayari na mabadiriko hayo. . Nchi nyingi za Afrika zimejijengea mfumo ambao hauko tayari kupokea mabadiriko na ili ni moja ya kikwazo kinacholifanya bara ili kubaki nyuma
 
Lowasa yupo kwenye ilani ya CCM...!?!? Maana mda mnao upoteza kumjadili Lowasa mngeutumia kumshauri Juma Pumba Maharagwe... Vipaumbele vyake visingekua Msikiti na Uwanja wa kisasa.
 
Ukitaka ujue nguvu ya Lowasa katika siasa, mwambie huyo sijui anaitwa ******************* aruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani halafu uone watu watakavyomuunga mkono.


Kama yeye fisadi Lowasa ana nguvu anashindwa nini sasa kufanya hiyo Mikutano?
 
Back
Top Bottom