Lowassa alitolewa kafara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa alitolewa kafara

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by dkn, Oct 30, 2010.

 1. d

  dkn Senior Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wana JF.

  Jana niliandika thread inayohusiana na habari ya Lowassa lakini naona moderator aliipiga chini.

  Kwa mnaokumbuka vizuri, Lowassa alikuwa kiongozi shupavu katika kazi yake ya Uwaziri mkuu na pia alikuwa na mapunguzu lakini siyo limbukeni kama JK anajua anachofanya ni mtu asiyecheka cheka na watendaji wake.

  Lowassa katika kuchagua wakuu wa mikoa, wilaya aliweka watu wake na strategy yake na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM ilikuwa ni kumtoa JK baada ya miaka mitano ya kwanza kwani CCM ilikuwa imeshaanza kuyumba mapema na kuwepo na kambi mbalimbali.

  Watu wa karibu na JK wakamtonya kuwa angalia Lowassa mshikaji wako anataka kukufanyizia na hapo ndipo issue ya Richmond ikaanza na ukiangalia kwa undani Lowassa hakuhusika sana katika mambo yaliyokuwa technical bali kutekeleza ya JK nchi ipate umeme, mengineyo kama gharama yalishapitia kwa mkaguzi mkuu wa mahesabu na wengine wengi kabla ya Lowassa..mnaweza kuhoji mbona alikubaliana lakini mwishoni mwa siku ilibidi kuwajibika na hii ilikuwa either yeye akatae kujiuzulu na kujiosha, JK na CCM wakaona wamdanganye kuwa ajiuzulu na immediately watamshafisha na hiki hakikufanyika labda tu spika alijaribu kumsafisha.

  Sasa mkae mkijua CCM imeoza na viongozi na wakongwe, wastaafu kama kina Mkapa wanampiga chenga kwani wanajua kichwani ni SIFURI na habebeki na chama chao kiko kwenye wakati mgumu. Pia Kikwete mwenyewe anajua uozo uliopo na ndiyo maana aliwekwa chini na CC kuwa chama kimekuwa na taswira mbaya sana na itabidi abebe jukumu kwa sasa…Kikwete personally ni mtu mzuri na kama angekuwa anagombea yeye kama yeye basi idadi kubwa ya waTZ ingempa kura, sasa hawezi kusema anawatimua baadhi ya viongozi kwani wao ndiyo wamemweka madarakani…support za kifedha kutoka kwa mafisadi kama Mramba zinaenda kwenye kampeni za CCM.

  Vijana tuchague kiongozi makini kama Dr. Slaa, Prof. Lipumba tunahitaji mabadiliko sasa.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Sasa mbona Lowassa huwa anasema "Mimi na JK hatukukutana barabarani"?

  Tafakari Mkuu.
   
 3. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,785
  Likes Received: 6,277
  Trophy Points: 280
  Hapa ni sawa. Naunga mkono hoja

  Hii imekaa kitetesi tetesi zaidi na haihusu kwa sasa.
   
 4. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Well, whatever the case, kura zote kwa Dr. Slaa ili kuondoa mfumo huu mkongwe uliojiita katika jamii yetu. Kwa kumchagua Slaa tutapata mabadiliko na maendeleo ya haraka, kinyume cha hapo, tutaambulia patupu.
   
Loading...