Apitakujilamba
JF-Expert Member
- Sep 27, 2013
- 205
- 83
Ukidadisi jinsi mambo yalivyoenda kuanzia mwaka 2005 hadi kipindi hiki cha mwaka 2015 utagundua kuwa Lowassa alimuhofia Dr Magufuli.
Mwaka 2005, Kikwete alipochukua uraisi kwa kusaidiwa na Lowassa na pia kuahidiana kuachiana kijiti, ifikapo 2015. Lakini Lowasa kama waziri mkuu aliona mbali kwamba Dr Magufuli akiwa waziri wa Ujenzi jina lake litaendelea kukua sana na kumuathiri katika nia yake ya kuwa raisi wa JMT.
Lowassa kama waziri mkuu alimshawishi raisi Kikwete wamteue Dr Magufuli katika wizara ya uvuvi ili kumpoteza kisiasa na jina lake lisiendelee kuvuma tena.
Lakini hali haikuwa hivyo kwa kuwa jina la Dr Magufuli liliendelea kuvuma hata akiwa katika wizara isiyotegemewa kumvumisha mtu. Vile vile kwa kipindi hicho wizara ya ujenzi ilidumaa kabisa ikiwa chini ya Dr Kawambwa, miradi mingi ya ujenzi kwa wakati huo ilizorota.
Ilipofika mwaka 2010, wananchi wengi walitaka Dr Magufuli arudishwe sehemu yake na Kikwete alimrudisha maana Lowassa kwa kipindi hicho alikuwa ameshajiudhuru. Na kama Lowassa alivyohisi mpinzani wake mkuu angekuwa Dr Magufuli na kweli imekuwa hivyo