Lowassa Afunika Iringa

Abdul Mohammed

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2013
Posts
1,331
Reaction score
860
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema amechoshwa na manyanyaso wanayoendelea kuyapata wakulima hapa nchi kwa kukopwa mazao yao na kutozwa ushuru na serilkali bila ya wao kupata faida yoyote.

Lowassa alisema punde atakapochaguliwa kuongaza nchi kitu kikubwa atakachokifanya kuwasaidia wakulima ni kufuta ushuru wote wa mazao kuhakikisha wakulima wananufaika na jasho wanalolitoa wakati wa kilimo.

Lowasa ameyasema hayo leo wilayani Mufindi alipofanya mkutano wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa Shule ya Msingi Wambi, mjini Mafinga.

Lowassa alisema watu wamekuwa wakizungumza kuwa CCM ni wezi wa kura kwasababu ni wajanja sana katika kufanya michezo michafu katika chaguzi na maneno hayo si yakuyabeza wala kuyafumbia macho.

"Mimi nataka kila mtu akihifazi vizuri kichinjio chake (kadi ya kupigia kura) na siku ya kupiga kura ikifika nawaomba wanawake na wanaume wajitokeze kwenda kupiga kura ila wakina baba nawaomba mkishapiga kura fanyeni kazi ya kuzilinda kura zenu" alisema Lowassa

Katika mkutano huo, waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai alipanda jukwaani na kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini kupitia Chadema, William Mungai ambaye ni mtoto wake.

Mungai aliwahi kuwa mbunge kwa miaka 35 kupitia CCM na aliweza kuteuliwa nafasi mbalimbali za uwaziri ikiwamo Wizara ya Kilimo, Mambo ya Ndani na Wizara ya Elimu.

Mungai alisema wananchi wa jimbo hilo wanatakiwa kumchagua William Mungai kwa sababu mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo hilo hakuweza kuongoza kama alivyofanya yeye.

Source: Mpekuzi
 
Aisee, kumbe Jangwani sasa ni Iringa. Hivi uongo mtaacha lini nyie UKAWA?
 
[h=1]
[/h]







"Umati huu unajitokeza katika mikutano ya UKAWA na barabarani kupunga linawapa ccm tumbo joto" Mhe. Edward Lowassa akiwa Iringa katika viwanja vya Gagilonga leo Jumapili 30/08/2015



















 
Mleta mada amecopy kutoka kwenye blog ya mpekuzi, hivyo han kosa lolote.
 
Ukiona mtu anashabikia ccm licha ya ugumu wa maisha uliopo ujue ni miongoni mwa wale maiti ambao kenyatta alimwambia nyerere kuwa anaongoza maiti
 
Iringa haiwezi kuwa na idadi yote ya hao watu
 
Leo naona kimya .................Tutawanyoosha mjini na vijijini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…