Lowassa afunguka miaka miwili nje ya CCM

Lowassa afunguka miaka miwili nje ya CCM

Busara hizi huwezi kuziona kwa Magumu,kule Magu ni vijembe,lugha ngumu na ukakasi tu,halafu maombi ya sala!!! Unagawa Taifa huku unasema hubagui!!!!
 
Akiwa anapata fursa kama hizi angalau kupitia vyombo vya habari jamii itanufaika kusikia neno la busara kutoka kwake ambalo linakonga nyoyo.

Na kwa wale mnaosema huyu mzee ni zilipendwa hatofaa kugombea tena, kipimo ni uchaguzi wa Kenya mmemsikia yuko mlengo gani, kwahiyo majibu ni baada ya uchaguzi wa Kenya kumalizika.
 
Tehe tehe tehe mbona anataka kuwabania wengine wanaowania hiyo nafasi kusimamishwa kugombea urais!
 
Inakusaidia nini?
Inanisaidia kuboresha ubongo wenu ili muweze kuona picha kubwa (big picture) ya masuala ya nchi yetu inavyotakiwa kuongozwa.
------------
Tena kasisitiza kuwa
Kuhusu Chadema, alisema chama hicho kikuu cha upinzani kinakua haraka, kinaongeza idadi ya wanachama na viongozi wengi, hivyo akasema kinachotakiwa ni kujenga uwezo wao.
Alisema uzoefu huo hauwezi kuja kwa siku moja, bali kwa muda mrefu kama ilivyo kwa CCM.
 
Lowassa ni nani tena siku hizi? Anasema kura zinazidi wakati watu wanajuta kumjua?

Yanayotokea Monduli na Hai hajaona?

Kweli siasa ni kiinimacho!!!!!!!!!!
 
Huyu mzee size yake JK tu, hawa wengine anawaonea.
Akiwekwa huyu na Ngosha kwenye mdahalo Ngosha anaweza tupa ngumi kwa jinsi alivyoachwa mbali kiuongozi na busara.

Kosa la EL ni CV yake wakati akiwa CCM its agift that kees on giving..,negatively.
 
Nimesoma yote sijaona sehemu akimkashifu mtu.. Kama yule mwingine mara wapinzani vilaza, oh sijui hako ka mbunge blah blah

Rais wa nchi anapaswa kuwa mtulivu kwa kiwango hichi cha Lowasa
 
Maneno ya busara kabisa
Jaribu kufikiri jee maswali kama hayo angepewa dereva wa Lori majibu yangekuwaje? yule ambaye hata mkewe anajuta kuongozana naye mikutanoni kwani hayakawii kumtoka maneno ya ajabu utadhani kameza betri iliyochuja?
 
Huyu muongo sana, alitudanganya akishindwa uchaguzi ataenda kuchunga ng'ombe lakini mpaka leo hajatimiza ahadi yake.
 
Tehe tehe tehe mbona anataka kuwabania wengine wanaowania hiyo nafasi kusimamishwa kugombea urais!
Kuna baadhi ya wana-chadema wameandika hata humu JF wakipendekeza 2020 chama kimsimamishe lisu kugombea urais. Lowasa anatuma ujumbe mzito kwa yeyote mwenye kuwaza urais kupitia chadema.
 
Mzee Lowassa Mungu akupe maisha marefu sana.
LA kujutia analo kwa nafasi alizoshika toka Mdogo alitakiwa baada ya kuacha uwaziri mkuu akae kimya asiwe active kwenye siasa ili awaachie jina jema wanae na wajukuu waweze kupewa nafasi Kama watoto wa jomo Kenyatta ,jaramogi odinga george bush, Ali Hassan Mwinyi, sokoine nk kawaharibia jina watoto kiasi kuwa mtu kuwa na jina lowasa mwisho unaonekana kibaka tu na huna hadhi. lowasa kaua jina kumwa la ukoo wa Lowasa. Heshima ni jina sio pesa
 
Naona anakubali kabisa utendaji wa awamu hii.

ila anataka wenzake wafanye kile yeye ambacho hakukifanya; anataka wanaohama upinzani sasa watoe sababu za kwanini wanafanya hivyo. Amesahau kuwa yeye hakutupa sababu kwanini alihama CCM baada ya kukatwa kugombea Urais, na sio kuhama kabla hata ya kuchukua fomu za kugombea Urais, au kabla hata ya kuwa Waziri Mkuu, au baada tu ya kujiuzulu Uwaziri Mkuu.
 
Back
Top Bottom